RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 1 & 2
Ningependa Kukushukuru Mpenzi Msomaji,
Uliyekuwa Nasi Katika Simulizi Ya Kwanza Ya
Mwanafunzi Mchawi.
Hiyo Riwaya bado inaendelea na ndo kwanza
imefikia patam. Wakati tukiendelea na
Riwaya hiyo, tumeona tusikuache mtupu,
tukaamua kuja na hii mpya huku ukiendelea
na ile ya mwanzo ambayo huwekwa kila
baada ya siku moja.
***************
Mtunzi:kamgisha
Ni siku ya jumamosi kama kawaida
wanafunzi wote wa shule tunayosoma
tunakwenda viwanjani kucheza michezo
mbali mbali kama mpira wa miguu na
michezo mingine ambayo wanacheza
wasichana waliopo katika shule yetu ambayo
niya bweni yenye mchanganyiko wa
wasichana na wavulana kuanzia kidato cha
kwanza hadi cha sita na nishule ya mtu
binafsi(PRIVET SCHOOL) iliyopo katoka mkoni
Arusha.
Kama kawaida yangu ya kuwa shabiki wa
timu ya darasa langu la kidato cha tano
ninachosoma ninaendelea kutazama mechi
tunayocheza na kidato cha tatu hadi wakati
huu tumeshafungwa goli mbili kwa moja huku
dakika zikiwa zinakimbia kuelekea ukingoni
huku mashabiki wa kike wa kidato cha tano
wakiendelea kuwapa moyo wachezaji wetu
waliopo uwanjani
“Oya Eddy mcheki yule manzi pale”
“Yupi?”
“Yule aliyevaa sweta jeupe”
“Ana nini?”
“Cheki alivyo bomba majamaa kibao
wamemtokea wamepigwa chini”
“Yupo kombi gani?”
“HKL”
“Ndio maana angekuwa huku tulipo sisi wala
asingekuwa mzuri”
“Hembu acha pumba zako Eddy”
“Kweli John unadhani angekuwa science
unadhani angekuwa hivi wewe si unawaona
wakina Matha walivyo kauzu class hadi
kuwatongoza mtu unashindwa”
Tukajikuta tukikatisha mazungumzo baada
ya mchezaji wetu mmoja kufunga bao la
kukomboa jambo lililoturudishia furaha hata
ya kuwepo uwanjani.
Kabla hata ya dakika mbili mbele mchezaji
wetu yule yule akafunga bao jingine kupitia
mpira wa kona uliopigwa na akaudumbukiza
nyavuni kwa kichwa na kuamsha shangwe za
wanafunzi wote wa kidato cha tano na
kuwafanya mashabiki baadhi kuingia
uwanjani huku wakishangilia kwa furaha
kwani tayari dakika zilisha kwisha.
Mimi na rafiki yangu John tukabaki nje ya
uwanja huku sura zetu zikiwa na furaha
kupita maelezo
“Wee dada jamaa anakuita hapa”.John
alimuita yule msichana tuliyekuwa
tunamjadili dakika kadhaa zilizopita.
Akatuangalia kwa dharau yeye na rafiki
zake kisha wakaongea maneno ya
kunong’onezana na kuanza kucheka kicheko
kilichotufanya tuwe kimya kama
tumemwagiwa maji ya baridi.
Safari ya kurudi shuleni ikaanza kwani
kiwanja chetu cha mpira kipo eneo la nje ya
eneo la shule.Tukiwa tumeongozana na kundi
la wasichana wa kidato chetu wakiimba
nyimbo za ushindi mimi na John tukawa na
kazi ya kumfwatilia yule msichana ambaye
kusema la ukweli amejaliwa uzuri unaweza
kusema alipewa siku yake ya pekee katika
uumbwaji wake
Tukafika hadi kwenye duka la shule ambapo
yule msichana alikwenda na rafiki yake
ambaye kidogo naye anavutia japo si
sana.Kutokana hatukuwa na lengo la kufika
katika duka hilo kwa aibu tukajikuta
tukinunua mifuko miwili ya pipi za Big boom
“Claudia ile hela siioni” Yule msichana
alizungumza huku akiwa anajipapasa papasa
kwenye mifuko ya sketi yake huku
akionekana kuwa na wasiwasi wa hali ya juu
kwani tayari walishakunywa soda pamoja na
kula keki za watu
“Hebu tazama vizuri”
“Kweli si unaona mifuko yote haina hela
jamani sijui imeangukia wapi”
Nikawatazama kwa huruma kisha nikatoa
waleet yangu mfukoni iliyotuna kwa wingi wa
pesa nikamuuliza muuza duka ni kiasi gani
cha pesa anachowadai akaniambia
nikawalipia na chenchi iliyobaki
nikamwambia muuza duka awapatie.
Tukaanza kuondoka kabla hatujafika mbali
Claudia akatuita na tukasimama wakaja
katika lile eneo tulilosimama huku rafiki
yake ambaye ndio aliyetufanya twende pale
dukani kwa kumfatilia akaawa analia
“Samahani kaka zangu tunawashukuru”
“Haina shida vitu vya kawaida,Eddy twende
zetu”
“Ngojeni kwanza”
Claudia alizungumza huku akimshika John
beda aliyeanza kugeuka na kutaka kuanza
kuondoka katika eneo tulilo kuwepo
“Mbona huyo mwenzako analia”
“Amepoteza pokety money yake ndio
kwanza ametoka kuipokea leo mchana
kwenye basi”
“Mmmm poleni”
John alizungumza kwa maringo na kuanza
kuondoka ikanilazimu mimi kubaki kwani
roho ya huruma ilianza kunitawala huku
wakati wote nikimtazama yule msichna
ambaye bado sikulitambua jina lake
“Amepoteza sh ngapi?”
“Eti Salome umepoteza shii ngapi?”
“Elfu themanini na tano”
Nikakaa kimya kama dakika mbili nikifikiria
nini nifanye,nikajikuta nikiitoa wallet yangu
mfukoni na kuesabu noti tisa za elfu kumi
kumi kisha na kuzitoa na kumpa Salome
taratibu akazipokea huku akiwa haamini
tukio linalo tendeka kwa wakati huo.
“Zitakusaidia saidia siku mbili tatu”
“Asante sana kaka yangu”
“Powa ukiwa na shida utakuja darasa la PCB
ndio ninaposoma”
Nikawapa na mfuko wa pipi nilio nunua kisha
nikaondoka huku moyoni mwangu nikijifariji
kuwa tayari nimesha fanikiwa katika hatua
ya kwanza ya kumpata mtoto mzuri.
Tukafika bwenini tukaoga kujiandaa na
sikukuu ya wanafunzi ambayo hufanyika kila
mwisho wa mwenzi wakati wa usiku katika
ukumbi wa shule.
Sikukuu hii hutoa fursa ya wanafunzi
kuonyesha vipaji vyao mbali mbali.Tukapitia
katika cantin ya shule na tukanunua
chakula kisha tukaelekea kwenye ukumbi
uliojaa wanafunzi kuanzia kidato cha
kwanza ahadi cha sita
Shughuli zikaanza huku wanafunzi mbali
mbali wakionyesha vipaji vyao huku
wakishangiliwa na wanaofanya vibaya
huzomewa.Ukumbi ukakaa kimya huku
tukiwasubiria washiriki wa shindano la umiss
wa shule kupita mbele yetu huku majaji
wakiwa ni waalimu wetu wa michezo pamoja
na wanafunzi baadhi.
Wakaanza kuingia mmoja mmoja huku
wakiwa wamependeza,nikajikuta
ninanyanyuka kwa furaha huku nikipiga
makofi hii ni baada ya kumuona Salome
akiwa katika msururu huo wa mamisi
waliochanganyika vidato mbali mbali.
Wakajipanga mbele ya majaji na kuanza
kuulizwa maswali mmoja baada ya mwingine
kwa lugha ya kingereza.Ikafika zamu ya
Salome kuulizwa swali wanafunzi wote
wakakaa kimya kumsikiliza atakacho kijibu
“SALOME CAN YOU TELL US WHAT IS
LOVE?”(Salome unaweza kutuambia upendo
ni nini?)
“Love is force of nature however much we
may want to,we can not command,demand
or disapper love,any more than we can and
in adition love cannot be bought,sold or
trade.You cannot make some one to love
you.Thanks”(Upendo ni hali ya msukumo wa
kihalisia kwa jinsi tunavyo hitaji.Hatuwezi
kulazimisha,kukomalia au kutawanya upendo
kwa kadri tunavyoweza na kwa kuongezea
Upendo hauwezi kununuliwa kuuzwa au
kubadilishana.Hauwezi kumfaya mtu
kukupenda wewe.Asante”)
Ukumbi mzima ukapiga makofi kasoro mimi
kwani nikajikuta sentensi ya mwisho ya
Salome ikijirudia rudia akilini mwangu “YOU
CAN CANNOT MAKE SOMEONE TO LOVE
YOU”(Huwezi kumfanya mtu
kukupenda).Wakatoka ukumbini kwa wimbo
walio ingilia kupisha mambo mengine
kuendelea huku tukisubiri matokeo kutoka
kwa majaji wetu.
Muda wa matokea ukawadia huku washiriki
waote wakisimama mbele yatu.Jaji mmoja
akaanza kutangaza nafasi kuanzia ya tatu
na ya pili huku nafasi ya kwanza
akimkabidhi mgeni rasmi ambaye ni mmiliki
wa shule kuitangaza huku wakiwa wamebakia
washiriki wanne.Tukakaa kimya kusubiria ni
nani atakaye nyakua taji kwa mwaka huo
“NA MSHINDI WETU NI……………………..SALOME
ALEX EDWARD”
Ukumbi mzima ukanyanyuka na kuanza
kupiga makofi ikiwemo mimi huku John
akinisukuma sukuma kila wakati huku
akinionyeshe jinsi Salome alivyopendeza na
kuzidi kuvutia kwenye macho ya
wengi.Akaanza kuvalishwa vitu wanavyo
valishwa mamisi pale wanapashinda huku
akikabithiwa uwa kubwa na mgaeni rasmi.
Muongoza shindano MC akamuomba Salome
amchague mtu wa kwenda kucheza naye
mziki kwa dakika tano.Salome akachukua
kipaza sauti na sote tukakaa kimya
kumsikiliza ni nani atapata bahati hiyo ya
kuitwa mbele ya ukumbi huo.Salome
akatizama tizama na macho yake akaelekea
sehemu tuliyokaa sisi.Akanyoosha kidole
chake watu wote wakaangalia tulipo sisi
“Eddy hichi kidole ni chako”.John
alizungumza huku akinisukuma sukuma kwa
kutumia bega lake.Nikanyanyuka kidogo ila
Salome akatingisha kidole chake kwamba si
mimi ni jamaa aliyekaa kiti cha nyuma yetu
ambaye ni kaka mkuu wetu.
Jamaa akanyanyuka kwa furaha huku
wezake nyuma wakimtuma akamchezee
Salome hadi alainike.Mimi na John tukabaki
kama watu wasio amini huku mimi roho
ikianza kuniuma kupita maelezo na
kumfanya John kuachia msunyo mkali adi
watu wa pembeni yetu wakamtazama na
kuanza kucheka
“Mademu wengine bwana was**e kama nini”
John alizungumza huku akiendelea kutoa
misunyo.Jamaa kama alivyoagizwa na wezake
akawa anazidi kumshika shika Salome mwili
wake huku wanafunzi wakishangilia kwa
furaha na kuzidi kunifanya niichukie
sikukuu hiyo
“John twende zetu tukalale” Tukanyanyuka
kwenye viti vyetu kutokana na mlango wa
kutokea upo mbele tukalazimika kupita mbele
ya ukumbi huku macho yangu yaliyojaa
hasira yakimtazama Salome ambaye naye
alinitazama kwa sekunde kadhaa kisha
akayapeleka macho yake sehemu
nyingine.Tukashuka kwenye ngazi za ghorofa
lenye ukumbi wa shule.Kabla hatujafika
chini mwanafunzi mmoja akatuita.
==>Endelea nayo <<kwa kubofya hapa>
Tafuta katika Blogu Hii
Jumatatu, 31 Oktoba 2016
Riwaya ya:sorry madam iko hewan
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni