Hebu jiulize unaelewaje juu ya msamaha? Umewahi kuomba, kuombwa au kusamehe? Kuna faida zozote za kuomba msamaha? Mada hii itakupa majibu ya mswali haya na utaona thamani kubwa ya msamaha.
Kwanza kabisa msamaha ni nini? Ni neno dogo, maarufu sana katika jamii yetu ambalo kwa hakika hutumiwa na watu wengi, lakini lina maana kubwa zaidi ya litumiwavyo.
Ni kawaida sana kumsikia mtu akisema: “Nisamehe bwana, nisamehe mshkaji wangu” kirahisi tu, mtu anazungumza,Hata hivyo, Wanasaikolojia wanasema asilimia 60 ya wanaoomba msamaha huwa hawaombi kutoka mioyoni mwao.
Matokeo hayo yalipatikana kutokana na utafiti uliofanywa ukiwahusisha ndugu na wapenzi waliokoseana, Aidha, inaelezwa kwamba, asilimia 30 ya wanaokubali kusamehe, hawasamehi moja kwa moja kutoka mioyoni mwao.
Yaani anakubali usoni lakini moyoni kuna kitu tofauti na
kinachoonekana machoni mwa mhusika, Msamaha sahihi ni ule ambao muombaji anapoomba kusamehewa anakuwa anaamaanisha anachozungumza, ni rahisi kusoma hilo katika mboni za macho yake, lakini pia hata yule anayesamehe ni vyema kama atakubali kusamehe kwa moyo wake. Huo ndiyo msamaha wa kweli rafiki zangu.
Hata katika uhusiano wako au ndoa, samahani ni neno lenye hadhi kubwa sana litumie kukufanya mwenye furaha siku zote za maisha yako, naamini mada hii imekuwa dawa tosha katika uhusiano wako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni