Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 8 Novemba 2016

UNAIJUA THAMANI YA ULIYE NAYE?

UNAIJUA THAMANI YA ULIYENAYE?
Kamgisha brogg 1 / 10 hours ago

Dickison kamgisha

Najua wote tunajua thamani ya mapenzi na pia tunafahamu ni jinsi gani mapenzi yanatesa, yanaumiza na wakati mwingine kuua. Wengi tunafahamu jinsi mapenzi yalivyoleta umoja, undugu na urafiki ambao haukutarajiwa katika maisha yetu lakini kutokana na huyu kuoa yule na yule kuolewa na huyu tumejikuta tukiunganishwa na jambo hilo.

Licha ya kujua thamani ya mapenzi na maumivu yake lakini tumeshindwa kuilinda thamani na kuyapuuza maamuzi yake. Tumekuwa wakosaji wakubwa sana kwa wenza wetu tulionao. Tumekuwa hatutambui thamani ya tulionao mpaka pale wanapoondoka mikononi mwetu. Tumekuwa watu tusiothamini mioyo na machozi ya wenza wetu kanakwamba sisi ni wanyama.

Kwanini umlize mwanaume aliyekupenda na kukusaidia katika maisha yako? Kwanini umsaliti mwanamke aliyekupa mwili wake na moyo wake pamoja na kukupa thamani kubwa katika maisha yake? Ipi thamani ya machozi yake kwako? Ipi thamani ya mapenzi yake kwako? Kwanini uliache penzi lako lenye furaha na kwenda kwa mtu mwingine ambaye wakati mwingine anaweza asifike hata nusu ya uliyenae?

Kumbukeni mapenzi ni hisia ambayo hukaa ndani kabisa ya moyo, hisia ambazo haziwezi kupuuzwa au kutokuthaminiwa. Hisia ambazo zinauwezo wa kukubadili jina kutoka fulani na kuwa marehemu fulani.

Hisia ambazo huumiza zaidi ya kufiwa na ndugu na wakati mwingine hata wazazi wako. Mwanamke au mwanaume anapokupenda huwa amekuona wewe na
kukuchagua wewe kati ya wengi ambao amewaona.

Amekuchagua wewe kwa kuamini kuwa wewe ni faraja, furaha, liwazo na kumbatio la huba. Hakukupenda ili umsaliti na kuishusha thamani yake.. Hakukupenda ili umpange foleni na kumvunjia heshima, bali amekuoa kwa kuamini wewe ndio kila kitu katika maisha yake.

Kama ni hivyo kwanini usimtunzie heshima yake? Kwanini usiipiganie thamani yake? Mwanamke aliyekupenda kweli unaweza ukamuacha akalia? Mwanaume uliyempenda kweli unaweza kumuacha akilia? Ni ipi thamani ya upendo wenu? Ni ipi heshima ya mapenzi yenu?

Jiunge nasi  Insta@mtembezionline ,fb@mtembezionline,youtube@mtembezi tv, Bofya HAPA Ku-install App ya mtembezi Official ili usi sumbuke kuingia kwenye website.

Visit website

View comments

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni