Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 7 Novemba 2016

Misemo


Kwa mujibu wa Mbonde katika
kongamano la Jubilei ya Miaka 75 ya
TUKI (2005) anafafanua maana ya
methali pamoja na dhima/umuhimu
au nafasi yake katika jamii kama
ifuatavyo;
“Methali ni lugha nyepesi ipenyayo
moja kwa moja katika mioyo ya
wasikilizaji. Aidha, methali au
misemo huondoa wingu au ukungu
katika mawasiliano ya kisayansi na
ya teknolojia nzito za kitaaluma.
Pia, methali ni kielelezo cha utashi
wa uhai wa jamii husika, historia na
falsafa ya utu wa binadamu, hekima
na busara. Mwanafasihi mashuhuri
katika Afrika, Chinua Achebe, katika
kitabu chake Things Fall Apart
(1959: 7) anaandika, “Methali ni
mafuta ya mawese ambayo kwayo
maneno huliwa.” Kauli hii
ikizingatiwa barabara huyafanya
maandishi kukubalika kuwa ni fasihi,
maana, matumizi ya methali na fani
nyingine hukoleza simulizi kama tui
la nazi na viungo mbalimbali kama
vile vitunguu, nyanya, zinavyoifanya
mboga iwe na riha na ladha tamu
zaidi.
Dhima ya methali katika jamii.
Mbonde anaendelea kufafanua
dhima/umuhimu au nafasi ya
methali katika jamii “Methali ni njia
ya mkato ya kuelimisha, kuadilisha,
kukosoa na kuelekeza jamii,
hususani vijana katika kuzingatia
tunu za jadi kwa kina ndani ya
mazingira ya asili ya jamii”.
Vilevile Ngole na Honero wanafasili
kuwa “methali ni aina ya usemi mzito
na ambao unakusudiwa kusema
jambo maalumu kwa njia ya fumbo.
Usemi huu mzito mara nyingi
hukusudiwa kumuonya, kumuongoza,
na kumuadilisha mwanadamu. Kwa
umbile la nje methali huwa na
muundo maalumu, muundo wenye
baadhi (pande) mbili. Upande
mmoja wa methali huwa unaeleza
mazoea au tabia ya mtu au kitu juu
ya utendaji wa jambo; na upande
wa pili unaeleza matokeo yatokanayo
na mazoea hayo au tabia hiyo
ambayo imeelezwa katika upande wa
kwanza.
UCHAMBUZI WA METHALI ZA SHAABAN
ROBERT
1. Cha mjinga huliwa na mwerevu.
- Asiyejua mara nyingi
hudhulumiwa na mtu anayejua.
- Hutumiwa kuwatanabaisha watu
wasiojua kwamba, haki zao siku zote
hudhulumiwa na wale wanaojua,
wajanja au wasomi.
2. Cha mlevi huliwa na mgema.
(Tazama:1)
. Cha mwivuo hulishwa na mgema.
- Ubaya hubainishwa kwa wema.
- Hutumika kuelezea kuwa daima
watu wema ndiyo ambao hubainisha
maovu katika jamii.
- Cha mwovuo hulishwa na mwemao.
- Sawa na “Cha mwivuo hulishwa na
mwemao.” (tazama 3)
4. Cha nini kitu hiki kizuri? Punje
moja ya mtama bora mara elfu.
- Si kila kisifiwacho ni kizuri kwani
vipo visivyosifiwa ambavyo ni vizuri
zaidi ya hivyo vinavyosifiwa.
- Hutumiwa kuonesha kuwa vitu vizuri
(watu) siku zote havijibainishi
kwamwonekano wake au umbile lake.
- Sawa na “Wamo lakini hawavumi.”
. Cha kichwa kitamu, na cha mkia
kitamu.
- Kila mtu anafurahia nafasi yake
katika maisha.
- Hutumika kuonesha kuwa kila hali
(cheo, uchumi nk.) inauzuri wake
katika maisha.
6. Cha shina kitamu, cha kati
kitamu na cha ncha kitamu.
(tazama: 5)
7. Chachu ikichachuka, watu
watatafutana.
- Amani itapotea punde mnyonge
atakaposimama na kudai haki yake.
- Hutumiwa kwa lengo la
kuwatahadharisha wale wawanyonyao
wanyonge kuwasiku watakapotambua
haki yao hapatatosha.
8. Chafi rasilimali yake utumbo.
- Kitu chochote chenye thamani
hakiachwi/hakionekani waziwazi. Au
tunaweza kusema uzuri wa mtu si
umbo wala sura (mwonekano wa nje)
bali ni tabia.
- hutumika kuwatahadharisha wale
wanaoshadidia au kupapatikia vitu
kwa kuangalia umbile lake bila kujua
undani wake.
9. Chafi rasilimali yake matumbo.
(tazama: 8)
Chagua dogo katika maovu mawili.
- Heri kutenda kosa dogo kuliko kuliko
kutenda kosa kubwa. Au ni afadhali
kupata hasara kidogo kuliko kupata
hasara kubwa.
- Hutumika kufariji endapo mtu
anapatwa na tatizo dogo, hivyo
anambiwa methali hii ili aone
kwamba tatizo alilolipata huenda
Mungu kamwepusha na janga kubwa
zaidi ya hilo.
. Chakula bora ni ukipendacho.
- Uzuri au ubora wa kitu anaujua
mtumiaji au mlaji.
- Methali hii hutumika kueleza kuwa,
katika maisha si vizuri kumlazimisha
mtu kutenda jambo bila yeye
mwenyewe kuridhia.
Chakula bora ni ulichonacho.
(tazama:11)
Chakula ni wali, kiungo ni samli
na mke ni mwanamwali.
- Kitu chenye thamani huthaminiwa
na watu.
- Methali hii hutumika kuonesha
kwamba katika maisha daima vitu
vyenye thamani ndivyo
vinavyothaminiwa na watu. Pia hata
watu wazuri au wenye sifa nzuri
ndiyo wanaopendwa na wengi.
Chanda na pete, ulimi na mate,
uta na upote.
- Chanda: kidole; Uta: upinde wa
kupigia mshale; Upote: kamba ya
upinde.
- Kila kitu hutegemeana.
- Hukuna kitu ambacho
kimekamilika katika maisha.
Cha ndugu hakiwi chako sharti
upewe.
- Using’ang’anie vitu visivyo vyako.
- Methali hii hutumika kwa ajili ya
kuwaonya na kuwakosoa wale wenye
tabia ya kudhani kwamba kitu cha
ndugu ni sawa na chakwake. Hivyo
katika maisha haupaswi kijivunia vitu
ambavyo si mali yako hata kama ni
vya ndugu yako wa damu.
Changilizi ya chungu huua hata
nduvu.
- Changilizi: kazi ya pamoja.
- Umoja au ushirikiano wa wanyonge
huweza kufanya mapinduzi
makubwa.
- Hutumiwa kuwa hamasisha watu
hasa wa tabaka la chini (duni) kuwa
endapo wataungana na kushirikiana
wanaweza kutenda mambo makubwa
katika maisha yao.
Changu si chetu.
- Kitu ambacho ni changu
mwenyewe hakiwezi kuwa cha wote.
- Hutumika kuwa hamasisha watu
kupenda kujishughulisha katika
maisha iliwajipatie vitu vyao wenyewe
badala ya kutegemea vitu vya
wengine. Pia inawafundisha watu
kutopenda kuishi kwa kutegemea
migongo ya wengine.
Chatu anamvuto kwa mbwa na
paka kama fedha kwa mtu.
- Jinsi fedha ilivyo na mvuto vivyo
hivyo wabaya au wakorofi wana uzuri
pia kwa watu wao.
- Methali hii hutumika
kuwatanabaisha watu watambue
kwamba katika maisha hakuna mtu
asiye na rafiki hata kama mbaya
kupita kiasi.
Chawa si nzito lakini husumbua.
- Matatizo madogo madogo
yasipodhibitiwa tangu awali huweza
kusumbua na kusababisha matatizo
makubwa zaidi.
- Hutumika kuwatahadharisha wale
wenye tabia ya kudharau matatizo
madogo madogo kwani huweza
kuongezeka na kushindwa kutatulika.
- Sawa na “mdharau mwiba guu huota
tende, usipoziba ufa utajenga
ukuta.”
Cheche huzaa moto.
- Kitu kidogo huweza kuleta
madhara makubwa.
- Hutumika kuwatahadharisha wale
wanaodharau mambo madogo kwani
huweza kusababisha madhara
makubwa yasiyotegemewa.
- Sawa na “mazoea hujenga tabia”
Cheche ndiyo moto.
- Tabia ya mtu huonekana kupitia
matendo yake.
- Hutumika kuwatahadharisha watu
katika maisha wanapaswa kufanya
mambo kwa umakini kwani kupitia
kwayo huweza kutambulika haraka.
Chechema utafika wendako.
- Hata ukitembea polepole utafika
tu.
- Hutumika kuwafariji watu
waliokata tamaa katika mambo
mbalimbali kuwa na uvumilivu katika
yote kwani uvumilivu ndiyo msingi wa
mafanikio katika maisha.
Cheka uchafu, usicheke kilema.
- Usimdhalilishe binadamu
mwenzako kwa lolote lile.
- Hutumika kuwaasa watu wenye tabia
ya kuwanyanyapaa walemavu kwani
hawakupenda kuwa hivyo na hata
wao watambue kwamba wanaweza
kupata ulemavu wakati wowote.
- Usimcheke mtu mwenye shida kwani
hata wewe siku moja unaweza kupata
shida kama hiyohiyo.
Chema chajiuza, kibaya
chajitembeza.
- Siku zote kitu kizuri (watu wazuri)
hujulikana tena bila hata
kutangazwa. Lakini kitu kibaya
hulazimu kutangazwa tena hata
ikibidi kutia chuku ili kionekane
kizuri.
- Methali hii hutumika kuwaambia
watu wasio na wema katika jamii.
Chema hakikai, hakina maisha.
- Daima katika maisha kitu chema
hakidumu kwa muda mrefu.
- Hutumiwa kuwafariji wale waliofiwa
na wapendwa wao. Pia huweza
kutumika wakati watu wanazungumza
juu ya habari za mtu aliyekuwa
mwema ambaye huenda amefariki
dunia.
- Sawa na “Wema hauozi.”
Chema hakikai, hakina maisha.
- Daima kitu kizuri katika maisha
hakiwezi kuishi kwa muda mrefu.
- Hutumika kuwatia moyo na kuwafajiri
wale wote waliondokewa na ndugu,
jamaa na marafiki zao.
Chema hujiuza, kibaya
hujitembeza. (tazama: 23)
Chema hutakwa na Mungu na
watu.
- Kitu kizuri hupendeza machoni
mwa kila mtu pamoja na Mungu pia.
- Huasa watu kuwa na tabia nzuri
kwani hupendeza mbele jamii na
hata kwa Mungu pia.
Cheupe dawa, cheusi dalili hawa.
- Tabia na sifa nzuri huongeza utu na
thamani ya mtu, lakini tabia mbaya
huondoa utu na thamani ya mtu
huyo pia huondoka katika jamii.
Chini kwetu juu kwa Mungu.
- Hakuna binadamu anayeweza
kuingilia mamlaka ya Mungu.
- Huonya watu kuacha tabia ya
kuingilia mamlaka ya Mungu.
Chini ya mdogo juu ya mkubwa.
- Usijiamini kwa nafasi uliyonayo
na kujifanya wewe ndio wewe katika
maisha kwani wapo watu ambao
wamekuzidi.
- Hutolewa kwa watu ambao huringia
nafasi na vyeo walivyo navyo katika
maisha.
Chini yetu Juu ya Mungu.
(tazama: 29).
Chipukizi ndio miti.
Vijana ndio taifa la kesho.
- Hutumika katika kuelimisha watu
wasiwadharau vijana na kuwanyima
haki zao kwa sababu vijana ndio
taifa la kesho.
34. Chombo cha kuvunja (kuharibika
hakina rubani)
- Kitu au jambo lililoharibika
kamwe halina mwokozi.
- Hutolewa kwa watu wanaostaajabu
na kulaumu kwa nini jambo
limetokea na kutaka wajue kuwa
jambo likisha tokea limetokea.
35. Chombo cha mwenye kiburi
hakifiki bandarini.
- Watu wasiopokea ushauri daima
hawafanikiwi.
- Hutumika kuonya watu wasiopenda
kushauriwa ili wapende kufuata
ushauri kwani si kila ushauri ni
mbaya.
36. Chongo kwa msangu, kwa
mswahili rehema ya Mungu.
- Kitu kisicho na thamani kwako
kwa mwenzio kinathamani.
- Hutolewa kwa wale
wanaodharau vya wenzao.
Chongo kwa mnyamwezi kwa mswahili
rehema ya Mungu. (tazama: 36)
Choyo huweka mali mpaka ikaoza.
- Uchoyo husababisha
uharibifu wa mali.
- Huonya watu ambao
hawapendi kutoa vitu vyao kwa
wahitaji mapaka vinaharibika
Chuchu mpya huangua chuchu ya
zamani.
- Kitu kipya hupelekea maendeleo
ya kile cha zamani.
- huelimisha watu juu ya kutunza na
kudhamini vya zamani kuwa vyote
kwa pamoja ni sehemu ya
maendeleo.
Chombo mpya huangua chombo ya
zamani. (tazama: 39)
41. Chuki hupotoa watu.
- Daima chuki hupoteza watu mpaka
wakashindwa kuaminiana,
kupendana na hatA kushindwa
kushirikiana katika mambo
mbalimbali ya kimaendeleo.
- Hutolewa kwa watu ambao
wanachukiana na kuwatahadharisha
kuwa hali hiyo huleta athari
mbalimbali katika maisha.
2. Chuki hupotoa haki na watu.
- Chuki hupoteza haki na huleta
mfarakano baina ya watu.
- Hutumika kuwaelimisha watu juu ya
athari za chuki kuwa hupoteza haki
za watu na pia kufarakanisha watu
hao.
3. Chuma kimetawala dunua.
- Watu wenye mamlaka wametawala
dunia.
- Hutumika kuonesha kuwa watu
wenye mamlaka ndio waamuzi wa
kila kitu.
4. Chuma kipate kingali moto.
- Ni vyema kufanya mambo katika
wakati mwaafaka.
- Kuhamasisha watu kufanya mambo
katika wakati unaofaa bila kusubiri.
5. Chumvi ikizidi chakula huaribika.
- Uongo ukizidi hupoteza uaminifu.
- Huambiwa watu wapendao kusema
uongo, kutoa ahadi bila kutekeleza
(hasa kwa viongozi kuwa hupelekea
jamii au watu wanaowaongoza
kushindwa kuamini kabisa)
46. Chumvi ilihadaa watu kuja
pwani kama sukari.
- Tamaa ya mali iliwashawishi
wageni kuingia nchini mara kwa
mara.
- Hujuza watu kuhusu historia ya
uvamizi wa wageni nchini na lengo la
kuja kwao ambalo lilikuwa ni
kujipatia utajiri.
- Pia hutumika kutoa funzo
kwamba ni vyema kutafiti jambo
kabla ya kutenda.
47. Chungu huvunjika magae na mtu
huharibika asifae.
- Hakuna kitu ambacho hakina
mapungufu.
- Hujuza watu kuwa hata binadamu
anaweza kuharibika na kupoteza
thamani sawa na vitu vingine kama
chumvi. Hakuna kitu ambacho
kimekamilika.
8. Chungu kibovu kimekuwa magae.
- Kitu kilichoharibika huweza
kukosa thamani kabisa.
- Hutahadharisha watu kuwa
kilichoanza kuharibika kisipo
chukuliwa hatua huharibika zaidi.
49. Chura hushangilia mvua wala
hakina (hana mtungi).
- Watu wengi hufurahia mafanikio
fulani bila kujua sababu za
mafanikio hayo.
- Hutolewa kwa wale wote ambao
hupenda kufurahia mafanikio bila
kufuatilia hatima ya mafanikio hayo
ikiwa wao ni sehemu ya jamii hiyo.
Chururu si ndondondo.
- Jambo kubwa si sawa na jambo
dogo.
- Kuhamasisha watu ambao
wanajuhudi katika kufanya kazi
ndani ya jamii kuwa waongeze
juhudi.
. Dalili ya mpumbavu hupumbaa.
- Dalili ya mtu mwenye mienendo
mibaya huonekana kutokana na
matendo yake katika jamii.
- Hutumika kuwaonyesha watu
ambao hawajali hususani mambo
yaliyo ya msingi.
Dalili ya mvua mawingu.
- Mafanikio ya mtu katika maisha
hutegemeana nay eye mwenyewe
jinsi alivyoyaandaa.
- Hufundisha watu kuchukua
taadhari.
Dalili ya vita matata.
- Kila matatizo yanayotokea katika
jamii kuna chanzo chake.
- Tuondokane na migogoro
inayochangia vita.
Damu nzito kuliko maji.
- Ndugu ni ndugu tu hata kama
wakigombana watapatana
hawataweza kutengana kamwe.
- Hutumika kuhamasisha ndugu
kuthaminiana/kusaidiana.
Dau la mnyonge haliendi
joshi,likenda joshi ni mungu
kupenda.
- Shida au matatizo ya mtu hayawezi
kumuathiri mtu mwingine
- Hutumika kuwaonya
Dawa ya deni kulipa
- Uaminifu katika maisha ni
muhimu ili kuweza kuishi na jamii
pasipo shaka.
- Huwaonya watu wanaokopa
wanatakiwa wawe wanalipa kwa
wakati.
Dawa ya moto ni moto.
- Ubaya hulipwa kwa ubaya.
- Usimwogope kumkabili mtu.
Dawa za wakurugenzi ni mizizi na
makombe.
- Viongozi walio wengi ili waweze
kutwaa madaraka au kushika
nyadhifa, lazima wapitie katika
mambo ya kishirikina.
- Kuwakosoa watu waendekezao
imani potofu.
Dhahabu haina maana chini ya
ardhi.
- Kukosa maarifa katika kazi ni
sawa na hujafanya chochote.
- Maarifa yanahitajika katika kazi
ili uweze kufanikiwa.
Dhambi hukimbiwa ,haikimbiwi.
- Kitu chochote chenye hatari na
chenye kuleta madhara hakina
urafiki.
- Huwataadharisha watu wenye
mienendo mibaya.
Dhihaka ina ukweli nyingi.
- Si kila jambo lisemwalo kiutani
halina ukweli ndani yake.
- Tusidharau mambo yoyote
yanayokuwa yanasemwa na watu ili
baadaye tusije juta.
Dhihaka ina kweli ndani. (tazama:
62)
Dhiki hukumbusha deni la zamani.
- Unapopatwa na matatizo au shida kwa
mara nyingine lazima kukumbuka
yaliyokufika kipindi cha nyuma.
- Hukumbusha kulipa deni kabla ya
wakati ili uaminiwe zaidi.
Dini ni mali ya roho.
- Kila jambo lina wakati wake katika
kupenda ambapo husukumwa na
roho.
- Tupende vitu kutoka rohoni na
wala tusilazimishwe.
Dunia duara huzunguka kama pia.
- Usimfanyie mwenzako ubaya pasi
kutambua kwamba ipo siku huyo mtu
atakusaidia.
- Hutumika kuonyesha namna
maisha ambavyo hayatabiriki.
Dunia hadaa na walimwengu
shujaa.
- Maisha ya duniani yamejaa hila
na yanahitaji werevu na ushujaa.
- Dunia huitaji werevu na ujuzi
kuikabili.
Dunia haidawamu,hudumu nayo.
- Mambo ya duniani ni ya kupita,
hayadumu.
- Hutoa funzo kwa watu
wasihadaike na mambo ya duniani.
Dunia haishi kupambwa na
kuharibiwa.
- Wajengao ndo waharibuo au
akupendaye kwa leo kutokana na
fadhila zako kesho aweza kukua
pasipo kutegemea.
- Huonyesha namna dunia
inavyokuwa na vitu vibaya na vizuri.
Dunia haishi kupendwa na watu.
- Mambo mazuri hayaishi kupendwa
na watu na hata kuharibiwa.
- Kuwa makini na vitu vilivyoko
duniani si vyote ni dhahabu.
Dunia haishi upya ingawa ya
zamani.
- Utu uzima au uzee hauwezi ukawa
kizuizi kwa mtu kutokuwa na mawazo
yanayojenga katika jamii
(hekima,busara).
- Tuwaenzi watu wazima ili watupe
mapya.
Dunia huleta jema na ovu.
- Kila binadamu anao wema wake
na hata uovu pia.
- Tusitegemee mema maishani bali
hata mabaya.
Dunia huzunguka kama pia.
- Dunia huitaji maarifa kuikabili
na wala sio kuiamini moja kwa moja.
- Tusikurupukie mambo pasipo kuwa
na maarifa au uelewa nayo.
Dunia ikupapo soni, kila utendalo
huzuni.
- Walimwengu wakikuacha au
kukugeuzia shingo, kutoshirikiana
mambo utajisikia vibaya.
- Walimwengu twapaswa kuishi nao
vyema.
Dunia kitu dhaifu.
- Hakuna mtu aliyemkamilifu
katika dunia hii.
- Hatuna budi kusameheana katika
mapungufu na madhaifu tuliyonayo.
Dunia kubwa mtakwisha hamu na
kiu.
- Mambo ya dunia hii ni mengi
huwezi kuyamudu yaliyo yote.
- Kuwa na kiasi katika maisha kwa
kufanya uchaguzi ulio sahihi ili
kuondokana na tamaa zisizo za
lazima.
Dunia mapito haiweki alama wala
nyayo.
- Wanadamu na mambo yao yanapita
kila wakati,na siku husogea na
mambomapya huibuka.
- Watu wanapaswa kujua kwamba
hapa duniani mambo mengi
yanapita, haina haja ya kushikilia
sana yaliyopita hasa mabaya,
twapaswa kuyasahau kwani hayaweki
kumbukumbu yoyote nzuri katika
maisha yajayo.
Dunia mti mkavu kiumbe siulemee.
- Dunia inafananishwa na kitu dhaifu
kama mti mkavu ambao hauna nguvu
hivyo mwanadamu hapaswi
kutegemea sana.
- Walimwengu si watu wa kutegemea
katika maisha waweza kukupoteza.
Dunia nzito kwa mtu mjinga.
- Mambo huwa magumu kwa mtu
mjinga asiyeweza kutumia akili
katika kujikwamua kutika hapo alipo
hadi kwingineko.
- Inawafundisha watu kutumia akili
katika kufanya mambo kwa bidii ili
wasije wakalemewa na maisha .
Dunia pana msilie ngoa.
- Usilie na kuumia (wivu) unapoona
mwenzako kapata kwani kila mmoja
ana bahati yake.
- Inatupasa kutokuwa na wivu juu ya
maendeleo ya mtu bali tujifunze kwa
waliofanikiwa ili nasi tufanikiwe.
Dunia toto kwa mtaalamu.
- Hakuna mtu anayeweza
kushindana na dunia.
- Huhamasisha watu kuwa makini na
maisha ya duniani hususani katika
kuzikabili changamoto zake.
Dua la kuku halimpati mwewe.
- Dharau na kiburi haviwezi kumuathiri
mtu aliyeko juu yako katika maisha
au laana ya mnyonge na malalamiko
yake hayamtishi mwenye nguvu.
- Kulalamika sio ndio suluhisho la
matatizo.
Eda ni ada yenye faida.
- Mwanamke kukaa eda ni muhimu na
yenye mafunzo makubwa na faraja
pia.
- Kuwaasa wanawake kuwa mila na
desturi zinapaswa kuenziwa.
Eda ya mke hakuna eda yam me.
- Eda huwekwa wanawake waliofiwa
na waume zao tu na sio wanaume.
- Mwanamke anaonwa kama mlezi
mkuu wa familia hivyo anapoachiwa
jukumu la kulea anapaswa
kufundwa.
Ee huyu ana ndaro si ukali wa
tumbili.
- Mtu anayetishia na kujitapa hana
uwezo wa kufanya lolote. Mara
nyingi anayejitapa mno kabla ya
kufanya jambo hafanikiwi.
- Inatuasa kuwa ukitaka kutenda
jambo onesha kweli kwa vitendo na
sio matambo na vitisho.
Egemeo la mnyonge ni Mungu.
- Mungu ndiye muweza wa yote katika
maisha ambapo mnyonge hukimbilia.
- Tuishi kwa kufuata mienendo miema
impendezayo mungu ambaye ndiye
kama kimbilio la mnyonge.
Elekeo la moyo hushindwa na la
akili.
- Akili ndiyo hutawala na ndio
mwongozo wa kila jambo.
- Kufundisha watu kuwa twapaswa
kutumia akili kupambana na kuamua
mambo.
Elimu haina mwisho.
- Elimu haina mwisho au haina
kikomo.
- Tujielimishe pasipo kuwa na
mwisho wake.
Elimu bahari haikaushiki.
(tazama: 88)
Elimu bahari haiishi kwa kuchotwa.
- Penye maarifa na ujuzi hapaishiwi,
watu hupenda kuchota pasipo
kikomo.
- Tusitosheke kwa mambo yenye
manufaa maishani kama elimu.
Elimu bila adabu ni uharabu.
- Unapokuwa na elimu na ukaitumia
kinyume na ilivyotakiwa ni uharibifu
- Tuyatumie vizuri maarifa
tuliyoyapata.
Elimu bila adili ni ujahili.
- Elimu bila hekima ni kazi bure.
- Hutumika kuhamasisha watu
kuthamini elimu.
Elimu hushinda nguvu.
- Ukiwa na maarifa, weledi na ujuzi
katika kazi utashinda nguvu ambazo
ungezitumia.
- Tusipende kutumia nguvu nyingi katika
kazi badala yake maarifa ndiyo
yatumike.
Elimu hutaka adabu.
- Inamaana kuwa ili kufanya
jambo zuri inatakiwa kuwa na
uvumilivu.
- Tunatakiwa kuwa na nidhamu
katika kufanya mambo yenye tija.
Elimu kidogo hatari.
- Mwenye elimu ya chini mara
nyingi huwa na matatizo.
- Kuwa na kiwango fulani cha elimu
husababisha usumbufu katika jamii
hasa kwa yule aliyenayo elimu hiyo.
- Huonya wale ambao wana kiwango
fulani cha elimu kutojisikia kuwa
wao ndio kila kitu kwani wapo ambao
wamewazidi katika hilo.
- Huhamasisha watu kujipatia elimu ya
kutosha ili kuzikabili changamoto
mbalimbali za maisha.
Elimu kidogo wazimu.
- Mwenye elimu ya chini mara
nyingi huwa na matatizo.
- Kuwa na kiwango fulani cha elimu
husababisha usumbufu katika jamii
hasa kwa yule aliyenayo elimu hiyo.
- Huonya wale ambao wana kiwango
fulani cha elimu kutojisikia kuwa
wao ndio kila kitu kwani wapo ambao
wamewazidi katika hilo.
- Huhamasisha watu kujipatia elimu ya
kutosha ili kuzikabili changamoto
mbalimbali za maisha.
Elimu mwangaza
- Elimu ndio njia ya kila kitu
katika maisha.
- Huhamasisha watu kuwa na bidii
katika kutafuta elimu kwani ndio
kila kitu katika maisha.
Elimu ni nguvu kwa mwanadamu.
- Elimu ndio mkombozi katika
maisha ya mwanadamu.
- Huhamasisha watu kuthamini
elimu kwani ndio dira ya maisha.
Enda mwanakwenda usirudi tena.
- Nenda moja kwa moja usirejee
tena.
- Hutumika katika migogoro baina ya
watu huku wakijibizana lilikusisitiza
kuwa hakuna haja ya kuonana tena.
Endaye ya akhera si wa marejeo.
- Mtu ambaye amepoteza kamwe
harudi tena duniani.
- Hutumika katika kuhamasisha watu
kupunguza masikitiko na kufanya
shughuli nyingine, kwani mtu
akishafariki hawezi kurudi tena.
. Endaye hufika atakakokwenda.
- Kila mwenye juhudi ya kufikia
mafanikio fulani daima hufanikiwa.
- Kuhamasisha watu kutokata
tamaa katika harakati za maish

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni