Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 2 Novemba 2016

AURI WAKO NAMBA
MOJA
Mwanamke sahihi kwako ni
yule ambaye anakushauri
hasa unapokuwa katika
matatizo makubwa zaidi ya
kimaisha.
Sifa hii itaonekana tangu
mapema kabisa,
unapokutana naye ukiwa
huna furaha, ni rahisi
kukuliza kulikoni,
anakuuliza si kwa sababu
anataka kuona furaha
yako pekee bali pia
anataka kujua kama kuna
tatizo ili aweze kutoa
mchango wake wa mawazo
katika tatizo lako.
Siku zote, mwanamke
mwenye busara na
anayekupenda, ni wazi
kwamba atapenda kujua
tatizo lako na kulichukulia
kama lake, ili aweze
kukushauri namna ya
kutatua kwa namna moja
ama nyingine.
KUJITOA KWA KILA HALI
Mwanamke anayekupenda
kwa dhati, atajitoa kwako
kwa kila hali. Unajua,
kuna mambo ambayo si
rahisi kufanyiwa na kila
mtu, yapo ambayo
yanafanywa kwa watu
wanaopendana tu.
Huyu atajitoa kwako,
atafanya mambo muhimu
ambayo si rahisi
kuyafanya kwa mtu
mwingine. Atakupa
vipaumbele kwenye mambo
yake yote kwa kukueleza
mipango yake (hata ile ya
siri) na kukufanya wa
kwanza kujua
kinachoendelea katika
maisha yake.
Lazima ujiulize na
uangalie, je, wewe ni moja
ya vipaumbele vyake? Je,
wewe unakuwa wa kwanza
kujua mambo yake kabla
ya rafiki zake? Je, uzito
anaochukulia kwako ukiwa
na tatizo, ndiyo
anaouchukua pia kwa
rafiki zake ama ndugu
zake? Lazima kuwe na
tofauti. Siku zote,
umuhimu wako hauwezi
kuwa sawa na mfanyakazi
mwenzake ofisini.
WIVU
Ingawa si lazima awe na
wivu lakini inaelezwa
kwamba wivu ni moja ya
alama ambazo unatakiwa
kuziangalia wakati
ukimchunguza kama
anakupenda kwa dhati.
Wivu ni ladha ya mapenzi.
Ni kama ndimu kwenye
mchuzi au kitunguu
swaumu kwenye pilau.
Wivu ni afya ya uhusiano,
kwamba lazima aoneshe
wasiwasi na wewe, atilie
mashaka simu yako,
achunguze email yako,
blog na hata ukurasa wako
wa Facebook. Hana nia
mbaya, lakini anachotaka
kujua, ni kama kweli yupo
peke yake au la.
PESA SI KILA KITU
Kama anakupenda, hawezi
kuithamini sana pesa. Hiyo
itakuwa kama sehemu ya
uhusiano wenu lakini si
kitu anachokipa
kipaumbele kwa asilimia
kubwa.
Kama anaomba sana pesa,
anazungumzia sana pesa,
matatizo yake makubwa ni
ya fedha, basi ujue
kwamba penzi lake lina
hati hati.
Mwenye mapenzi ya kweli,
pesa ni matokeo tu, lakini
si kukufanya wewe
kitegauchumi au sehemu
ya kutatua matatizo yake.
WASIWASI NA USALAMA
WAKO
Baadhi ya wanawake
wanaweza kusema mengi
lakini wasiwasi kwa ajili ya
usalama wa mtu
unayempenda ni muhimu
sana. Hii ni moja ya njia
ya kujua kama mwanamke
anakupenda. Anapenda
kujua uko wapi, unafanya
nini na utarudi nyumbani
muda gani.
Si rahisi kufanya hivyo kwa
mwanaume ambaye hana
mapenzi naye. Anafanya
kwako, kwasababu
anakupenda na anajali
usalama wa maisha yako,
na si maisha yako pekee,
bali kuna jambo kubwa na
zito zaidi. Anajali usalama
wa penzi lake maana
hataki kukupoteza na
kulipoteza penzi hilo.
ANAKUSIKILIZA
Kusikilizwa na mwanamke
si tabia mpya au ya
kujifunza, ni agizo la
moja kwa moja kutoka kwa
Mungu mwenyewe. Kwa
meneno mengine, kama
mwanamke wako atakuwa
hakusikilizi, mpinzani,
mkaidi, mkali, mkorofi,
maana yake anapingana
na maagizo ya Mungu
moja kwa moja.
Kupingana na agizo hilo,
ambalo ni stahili yake, ni
wazi kwamba hata mambo
mengine ya kibinadamu
ambayo atatakiwa
kujifunza yeye mwenyewe
kwa nia ya kuonesha
heshima kwako wewe
mumewe mtarajiwa,
atashindwa.
Sipo hapa kuhubiri dini,
lakini kuna mahali
maandiko yameagiza,
mwanaume ampende sana
mke wake na mwanamke
amheshimu/amtii mumewe.
Hapo kila kitu kipo wazi,
kwahiyo katika hali ya
kawaida, kama mwanamke
wako atashindwa kukutii,
kukuheshimu na
kukusikiliza kama kiongozi
wake, basi ni dhahiri
kwamba, atakuwa tatizo
katika maisha yenu ya
baadaye, hasa mkiwa
tayari mmeshaingia
kwenye kifungo cha ndoa.
ANAWAPENDA NDUGU ZAKO
Ndugu zako ni cheni katika
maisha yako. Ndiyo watu
wako wa karibu. Ndiyo
wanaokusaidia/
watakaokusaidia pindi
utakapokuwa na matatizo.
Unapotaka kuingia kwenye
uhusiano wa kimapenzi na
mwanamke, hasa kuingia
katika hatua kubwa zaidi
ya ndoa, unapaswa
kufikiria mara mbili juu ya
hawa wanaoitwa ndugu.
Ni tatizo kubwa sana,
kama mwanamke
unayetarajia awe mkeo,
akawa hawapendi,
anawadharau au
anawachukia ndugu zako
kwa sababu zake
mwenyewe.
Mfano; kama mwanamke
wako hamheshimu mama
yako mzazi, baba yako,
kaka na dada zako ni
tatizo. Inakuwa tatizo kwa
sababu hawa ni watu
ambao unatakiwa
kushirikiana nao katika
mambo mengi ya kijamii,
hasa unapokuwa katika
matatizo. Kwakuwa
unawapenda ndugu zako,
pia utakuwa na mapenzi
na mwanamke wako,
lazima kutakuwa na
mgawanyiko maana pande
hizi mbili ni muhimu
kwako.
Hapa namaanisha
kwamba, inawezekana
kabisa ukajikuta
unaegemea aidha kwa
ndugu zako zaidi au kwa
mwanamke wako na hapo
ndipo mkanganyiko
mkubwa wa kiuhusiano
unapoweza kutokea.
Mwanamke wako akiwa na
upendo na ndugu zako ni
wazi kwamba yote hayo
niliyoeleza hapo juu
hayatajitokeza na hivyo
kuishi kwa amani.
HOME
MAHUSIANO
DALILI 7

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni