Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 26 Oktoba 2016

Man City kumweka Mourinho njia panda

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho
BAADA ya kutofanya vizuri kwa takribani michezo mitatu kwenye Ligi Kuu ya England, Manchester United ikiongozwa na Jose Mourinho wapo kwenye kibarua kingine leo kwa kuwakaribisha mahasimu wao Manchester City katika mchezo wa mzunguko wa pili wa kombe la ligi utakao pigwa leo.

Mchezo wa mwisho timu hizo kukutana ni mwezi moja uliopita kwenye ligi hiyo katika Uwanja wa Old Trafford na Manchester City iliibuka ana ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Katika mchezo wa leo Manchester United inaingia ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Chelsea baada ya kupata kipigo cha mabao manne kwa nunge huku Mourinho akiwa katika hali ya sintofahamu baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya na kiwango kibovu.

Manchester City itaendelea kukosa kiungo wao mshambuliaji Kevin De Bruyne ambaye yupo majeruhi kwa muda sasa na kukosa michezo kadhaa, huku Manchester United itamkosa beki wake wa kati raia wa Ivory Coast, Erick Baily baada ya kupata maumivu na kushindwa kuendelea na mchezo huo.

Katika hali nyingine ya kushangaza baada ya kuwa na matokeo mabovu, kiungo mkongwe wa klabu hiyo Roy Kean amendelea kumtupia lawama mshambuliaji wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic ambaye haonekani kusikitishwa baada ya timu kupoteza mchezo dhidi ya Chelsea. Ibrahimovic alionekana akicheka na huku akibadilishana jezi kwa furaha.

Endapo timu yoyote itapoteza mchezo huu wa mzunguko wa pili wa kombe la ligi, basi itakuwa imetoka rasmi katika kombe hilo hivyo mchezo huu unatazamiwa kuwa na mvuto wa aina yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni