Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa amechambua mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli tangu aingie madarakani akisema kuna mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu.
Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 aliungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema hayo jana katika andishi lake kwa vyombo vya habari.
Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008, amesema katika andishi hilo kwamba, “kile ambacho tulikisema wakati ule kwa nini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.
“Kwamba pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa, utumishi wa umma umekuwa kaa la moto.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni