Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Uvccm Arusha walitaka Jeshi la Polisi limkamate Lema

Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Arusha mjini Martin Munisi amelitaka jeshi la polisi  kumkamata Mara moja mbunge wa jimbo la Arusha mjini Chadema God bless Lema kwa kitendo chake cha kusema Mh raisi atakufa kabla ya 2020 kama hatawasikuliza wao chadema Mwenyekiti Martin Munisi ameyasema hayo jioni hii wakati akihojiwa na Radio Sun Rise ya jijini Arusha

Eidha mwkt Munisi amelitaka jeshi la polisi kutoa ufafanuzi wa mikutano iliyokatazwa na inayotakiwa maana lema anafanya mikutano ya chadema na siyo mikutano ya mbunge mikutano ya mbunge hulenga kuzungumzia ahadi za mbunge alizotekeleza atakazotekeleza na kuhamasisha maendeleo ila kinyume chake Lema yeye anasema wananchi wataingia barabarani maana hali ni mbaya mara raisi takufa kabla ya 2020

haya ni maneno yasiyovumilika hata kidogo kwenye jamii iliyostaharabika nivizuri jeshi letu likamhoji lema kuhusu kumzushia au kutabiri kifo Kwa mwkt wetu wa chama taifa na na rais wetu .Nakwavile Lema hana agenda nalitaka jeshi la polisi kuzuia mikutano yake kama wasipozuia sidhani kama vijana wa ccm na wananchi wapenda nchi yao watakuwa tayari kuvumilia matusi ya lema kwa Mh rais, wetu mpendwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni