Kanisa la mlima wa moto Assemblies of God la Mikocheni B Dar es salaam, linatarajiwa kuwalipia faini jumla ya wafungwa 43 katika gereza la Dodoma, ikiwa ni muendelezo wake wa kufanya hayo kwa wafungwa walioshindwa kulipa faini ndogondogo ikiwa ni kuanzia kiasi cha shilingi 50,000 mpaka 300,000.
Akizungumza na waandishi wa habari Mchungaji wa kanisa hilo Dkt. GETRUDE LWAKATARE, amesema awamu hiyo ya kwanza mkoani Dodoma itashuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya PAROLE, Augustine Mrema, ijumaa wiki hii huku tayari kanisa hilo likiwa limewalipia wafungwa hao takribani shilingi milioni 6.8.
Katikati ya mwaka huu kanisa la mlima wa moto, liliwalipia na kuwatoa jumla ya wafungwa 78 katika magereza ya Ukonga na Segerea kwa gharama ya shilingi milioni 25.
Dkt. Lwakatare amesema pamoja na kulipia faini hizo, kipaumbele kwa wafungwa watakaonufaika ni wanawake wanaonyonyesha, wagonjwa, wazee pamoja na wale walioonyesha tabia nzuri gerezani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni