Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 26 Oktoba 2016

Picha za wanyama za kuchekesha zaidi 2016

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za kuchekesha na kusisimua za wanyama zilizopigwa mwaka huu, miongoni mwa picha hizi ikiwa moja ya mbweha aliyeingia kichwa kwanza kwenye theluji na nyingine ya nyati aliyegeuzwa choo na ndege mmoja.

Picha hizi zimeteuliwa kushindania tuzo ya picha za ucheshi za wanyama mwaka huu.

Shindano hili huandaliwa kuchangisha pesa na kusaidia shirika la kutetea uhifadhi wa wanyama la Wakfu wa Born Free.

Kuna jumla ya picha 40 na mshindi atatangazwa mwez Novemba.

Hapa ni baadhi ya picha hizo.

 Utaweza kuzuia tabasamu hapa?

 Master of camouflage...

 Unapofuatilia umpendaye, na hutaki akuone

 Ukifanya kazi Jumatatu baada ya starehe nyingi wikendi

 Mamako akitaka usione kitu cha kuogofya au cha 'watu wazima' kwenye TV

 Unaapojificha na kuvunja ahadi yako ya kutokula sana ili usiongeze uzani

 Siku ambayo mambo hayaendi sawa, dubu huyu anashindwa kumnasa samaki...

 Unapojaribu kumuonesha mwenzako kucha zako zilivyopambwa, mwenzako hana haja...

 Kupata lifti halisi...

 Unapojifanya huna kichwa na huoni yanayoendelea ... kama penguini hawa?

 Umewahi kukutana na sungura mwenye madoido?

 Siku inayofuata baada yako kulewa usiku kucha, na uliambia watu hutakunywa pombe tena...

 Unapokuwa na siku mbaya...ndege anakugeuza choo.

Fisi huyu utamshinda kwa kicheko?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni