Rais Magufuli Awaonya Wakuu wa Wilaya na Mikoa
Udaku Special Blog / 18 hours ago
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kote nchini na kuwataka kuwa na nidhamu ya pesa na kutumia fedha za serikali vizuri.
Rais Magufuli amesema hayo leo wilayani Chato mkoani Geita alipokuwa akihutubia wananchi katika makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa, ambapo mbali ya kushukuru kwa msaada huo Rais Magufuli alizungumzia juu ya tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kuiba fedha za wananchi na kutumia katika mambo yao wenyewe nje ya malengo ya serikali.
"Hapa penyewe Chato kuna fedha zaidi ya bilioni moja za pembejeo zimeliwa na viongozi, hivyo natoa wito kwa viongozi wote wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kote nchini kuwa na nidhamu na fedha za serikali, tujifunze kutumia fedha vizuri za serikali asitokee mchwa huko kula pesa za serikali. Maana hili lililotokea hapa Chato najua limetokea sehemu nyingi na hivyo saizi tunaanza kufanya ukaguzi kila sehemu" alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka wananchi wa hali ya chini kuwa na amani kwani katika kipindi chote ambacho yeye atakuwa madarakani hataki kuona wala kusikia wananchi wa hali ya chini wakinyanyaswa sababu na yeye ametokea katika maisha hayo hivyo anatambua jinsi wanavyopata shida watu wa kipato cha chini.
"Serikali haiwezi kufanya biashara na masikini, inawaacha matajiri inawasumbua masikini, mimi nimekuwa katika maisha ya shida nimechunga ng'ombe, nimeuza maziwa kwa hiyo najua maisha ni nini. Najua Tanzania watu wengi wanaishi maisha ya chini na katika kipindi changu sitaki kuona watu wa hali ya chini wanapata shida, wanapata taabu ndiyo maana tunajitahidi kuhangaika kuleta maendeleo ili wanufaike na wao" alisisitiza Magufuli
Rais Magufuli akuziacha taasisi ambazo zimekuwa zikitetea wanafunzi kupata mimba na kusema yeye taasisi hizo hazipendi na ameziwekea kizingiti kuwa ikiwezekana zisipewe msaada bali taasisi zinazofanya mambo ya kimaendeleo kama taasisi ya Mkapa Foundation ndiyo zinatakiwa kupewa msaada sana kwa kuwa zinarudi kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni