Chelsea yamuongezea muda wa mapumziko Diego Costa
KAMGISHABLOG / 11 hours ago
Mshambuliaji Diego Costa amepewa muda zaidi wa kumpumzika na Chelsea, hatua iliyozidisha uwezekano kwamba huenda akaihama klabu hiyo majira haya ya joto.
Mhispania huyo wa miaka 28 amehusishwa na kuhaam klabu hiyo baada ya kufahamishwa na meneja Antonio Conte kwamba hayupo kwenye mipango yake.
Costa hakujiunga na wenzake kwa mazoezi Jumatatu.
"Iliafikiwa kati yake na klabu kwamba anafaa kuchukua siku zaidi kupumzika," taarifa kwenye klabu hiyo ilisema.
Costa anatarajiwa kutohudhuria mazoezi wiki hii.
Mshambuliaji huyo alikuwa mchezaji pekee ambaye hakufika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham kando na Antonio Rudiger, ambaye alijiunga na klabu hiyo Jumapili.
Costa aliwajulisha wanahabari kwamba Conte alikuwa amemwandikia ujumbe wa simu kwamba hakuwa kwenye mipango yake mwezi jana, na inaarifiwa kwamba msimamo wake haujabadilika.
Duru zimeeleza BBC kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania anakaribia kuihama klabu hiyo.
Costa alifungia Chelsea mabao 20 katika mechi 35 za Ligi ya Premia msimu uliopita na kuwasaidia kutwaa ubingwa wa ligi.
Amehusishwa na kurejea Atletico Madrid, licha ya klabu hiyo kuzuiwa kununua wachezaji wapya hadi Januari.
Costa alizaliwa Brazil na alikaa misimu minne Atletico kabla ya kujiunga na Chelsea kwa £32m mwaka 2014.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni