Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 10 Julai 2017

Je Lukaku ni usajili sahihi, Sanchez atabaki au ataondoka – maswali 6 yanayohusu timu 6 za juu EPL

Je Lukaku ni usajili sahihi, Sanchez atabaki au ataondoka – maswali 6 yanayohusu timu 6 za juu EPL

ShaffihDauda / Aidan Charlie / 4 hours ago

Msimu wa 2017-18 wa Premier League unaanza mwezi mmoja kutoka sasa. Huku dirisha la usajili likizodi kushika kasi na pre season zikiwa zimeanza tuangalie maswali 6 makubwa kwa kila timu iliyoshika nafasi 6 za juu katika EPL msimu uliopita. 

1. Chelsea: Je Conte atapata wachezaji anaowataka


Mwendo pole, mbinu ya kuingia kwenye soko la usajili taratibu imetoa matokeo mabaya, hasa wiki hii, baada ya mashabiki wa Manchester United kuwazidi ujanja na kumsaini Romelu Lukaku kutoka Everton. Mshambuliaji huyu alikuwa chaguo la kwanza la Antonio Conte kumbadili Diego Costa, hivyo kumkosa inamanisha inabidi Chelsea kurudi nyuma kuangalia options nyingine ili kutimiza mahitaji yao ya mshambuliaji. 

Kuelekea kurudi kwa Conte katika maandalizi ya msimu mpya Wiki hii, usajili pekee ambao wameufanya Chelsea ni wa Antonio Rudiger na Willy Caballero. Tiemoue Bakayoko anatarajiwa kusajiliwa pia, lakini uhamisho wake unachukua kuda mrefu kuliko ilivyotegemewa.. Conte mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na inaonekana hatofanya hivyo mpaka atakapopata kikosi anachokitaka. Presha sasa ipo kwa wakurugenzi Marina Granovskaia Michael Emenalo kutimiza mahitaji ya kocha wao. 
2. TOTTENHAM: Je Kyle Walker ataondoka?


Katika ukimya wa soko la usajili mpaka sasa, swali pekee la kujiuliza ni wapi Kyle Walker atakuwa akicheza soka itakapofika September. Manchester City wanataka kumsaini beki huyu wa kulia wa England. 

Walker ana mkataba wa muda mrefu na Spurs, na klabu hiyo ya kaskazini mwa London haina haraka ya kumuuza mchezaji yoyote kwenye kikosi chao labda Moussa Sissoko. Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy ni mfanyabiashara mgumu kwenye kuuza wachezaji. Uhamisho huu unategemea kwenda mpaka mwisho wa usajili. 
3. LIVERPOOL: Je Liverpool wataweza kushindana kwa usajili huu waliofanya? 


Katika siku yao, Liverpool inaweza kumfunga timu yoyote. Ilithibitika msimu uliopita, kikosi cha Jurgen Klopp kina rekodi bora dhidi ya timu 6 za juu za Premier League. Walipoanza vyema walianza kupewa nafasi kubwa ya kutwa ubingwa kabla ya majeruhi kuanza kuwa mengi na mchanganyiko wa ratiba na kutokuwa na reserves imara ya kulivuruga mipango yao.  
Walifanikiwa kumaliza ndani ya Top 4, hivyo watacheza mchezo mmoja wa Play Off ili kuingia hatua ya makundi ya Champions League. Ulaya ndio sehemu ambayo Liverpool wana rekodi bora zaidi, lakini Mohamed Salah ndio usajili pekee waliofanya katika dirisha la usajili. Klopp anabidi aongeze wachezaji kukidhi mahitaji ya kikosi chenye ushindani nyumbani na ulaya.

4. MAN CITY: Guardiola atafanyaje kikosi chake kiwe na furaha? 


Ikiwa City watapata wachezaji wote wanaowataka katika dirisha hili la usajili ukiunganisha kikosi kizuri kilichopo chenye washambuliaji  Sergio Aguero, Gabriel Jesus, Leroy Sane na Raheem Sterling na bado Pep Guardiola anamtaka Alexis Sanchez. Nyuma ya washambuliaji hao kuna viungo  Bernardo Silva, David Silva, Kevin De Bruyne, Ilkay Gundogan, Yaya Toure na Fernandinho.

Guardiola atakuwa na kikosi chenye nguvu, kitakachokuwa na uwezo wa kushindana katika Premier League na Champions League, lakini wengi wa wachezaji wana uwezo wa kucheza kwenye maeneo mengi kwenye dimba lakini wapo wataokuwa wanakosa furaha kutokana na kutokucheza maeneo ambayo wanayamudu zaidi. 
5. ARSENAL: Je Sanchez atabaki au ataondoka? 


Soko la usajili limeanza vyema kwa usajili wa Alexandre Lacazette, lakini mafanikio kwenye soko hili la usajili yatakuwa kuwabakisha waliopo. Alexis Sanchez bado hajasaini mkataba mpya na huenda akafosi kuondoka, jambo ambalo litaiweka Arsenal kwenye sehemu ngumu. Je wachukue mshiko kwa kumuuza mchezaji wao bora au wamlazimishe amalize mkataba wake ambao umebakia mwaka mmoja kabla ya kumpoteza kwa uhamisho wa bure?

Ikiwa klabu ipo serious na suala la kushindania ubingwa msimu ujao, basi kumbakisha Sanchez ni jambo lisilohitaji mjadala. Arsenal pia wana suala kama hili kwa Mesut Ozil, lakini kiungo huyo mjerumani anaenda kwenye mwaka mwisho wa mkataba wake japokuwa hana timu nyingi zinazomwania, jambo ambalo linawapa Arsenal urahisi wa kumbakisha. 
6. MAN UNITED: Je Lukaku ni usajili sahihi? 


Jose Mourinho ameweka imani yake kwa Romelu Lukaku kufunga magoli ya kuipeleka timu yake katika mbio za ubingwa. Wakiwa wamefunga magoli 54 katika mechi 38. United hawakufunga magoli ya kutosha msimu uliopita, wakiwa na Zlatan Ibrahimovic. Sasa ameondoka na Mourinho ameweka matumaini yake kwa Lukaku kuongoza safu ya ushambulizi. 
Hii itakuwa hatua kubwa kwa mshambuliaji wa Kibelgiji. Kufunga dhidi ya zenye hadhi ndogo katika Premier Keague, jambo ambalo amelifanya mara nyingi, lakini itakuwa jambo tofauti kabisa kufunga katika Champions League. Akiwa na miaka 24, Lukaku anatoa picha ya kuwa ataimarika zaidi, itakuwa ni kazi yake na Mourinho kuwathibitishia vinginevyo watu wenye mashaka dhidi ya Lukaku. 

Visit website

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni