Mbao Fc yachezea kichapo cha magoli 21
KAMGISHABLOG / 3 hours ago
Timu ya Mbao FC ya Dodoma imekubali kichapo cha mbwa mwizi baada ya kufungwa mabao 21 dhidi ya timu ya Panama FC kwenye mchezo wa Kombe la Ng’ombe mjini Dodoma.
Kichekesho zaidi kama sio rekodi ni mshambuliaji wa Panama FC, Dulla Mjengwa aliibuka kinara wa mabao 13 lakini hakuambulia zawadi ya mpira wowote kama inavyotakiwa.
Mechi hiyo ilipigwa jana Jumamosi kwenye Uwanja wa Mtekelezo uliopo katikati ya mji, ambapo ilishuhudiwa timu hiyo ya Mbao ikitokota tangu mwanzo mbele ya Panama kwani hadi mapumziko ilikuwa imeshakula bao 10 na kuruhusu bao zingine 11 kipindi cha pili.
Mratibu wa ligi hiyo, Rashid Nyoka baada ya kuulizwa sababu za kutotoa zawadi ya mpira kwa mfungaji huo alisema, walishindwa kumpatia mpira mfungaji huyo kutokana na ligi hiyo kutokuwa kanuni zao kutoweka kipengele cha zawadi hiyo.
Kipigo hicho kiliwafanya viongozi wa timu hiyo ya Mbao wasizungumze lolote ambapo wengine walidai timu hiyo ilikata tamaa kutokana na kufungwa mechi zilizopita na kukosa nafasi ya kutinga robo fainali huku wengine wakiwashtumu viongozi wao kuwa walipanga kikosi dhaifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni