Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 9 Julai 2017

Mzee cheyo awavaa sumaye na lowassa

Mzee Cheyo awavaa Sumaye naLowas KAMGISHA BLOG / 2 hours ago

Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo maarufu kama `Bwana Mapesa’ amesema jukumu la viongozi wastaafu ni kuwaweka pamoja watanzania na siyo kuwafarakanisha kwa tofauti za kisiasa, kidini na uchama.

Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam wakati akitambulisha ofisi za chama hicho zilizohamia Mwananyamala A, Cheyo amesema anashangazwa na mawaziri wakuu wastaafu ambao walihamia upinzani na kuanza kutoa kauli ambazo kwa namna moja au nyingine zinaharatarisha amani.

“Upinzani sio kupinga kila jambo, wastaafu jukumu lao ni kufanya mambo ya kutuweka pamoja na sio kutufarakanisha,” amesema Cheyo.

Mh Cheyo amesema kuingiza mambo ya dini katika siasa ni kutafuta mfarakano baina ya  wananchi na kwamba kwa maoni yake kiongozi ambaye ameshika nafasi kubwa kama Waziri Mkuu hatarajiwi kuliingiza taifa katika mafarakano.

“Maendeleo hayana vyama, Rais tuliye naye anafanya mambo na yanaonekana tumuunge mkono tuachane na itikadi za vyama, au wanataka tusubiri mpaka chama fulani kiingie madarakani ndipo tupate maendeleo?” alihoji Mh Cheyo.

Hata hivyo Mh Cheyo amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Rais wa awamu ya tano, Mh Dkt. John Magufuli na kuijenga Serikali imara, yenye kulinda maslahi ya nchi na ustawi wa watu wake.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu wa mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa aliitaka Serikali kuwaachia huru mashehe wa Uamsho wanaoshikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni