Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 11 Julai 2017

Rais Magufuli Awaonya Wakuu wa Wilaya na Mikoa

Rais Magufuli Awaonya Wakuu wa Wilaya na Mikoa

Udaku Special Blog / 18 hours ago

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kote nchini na kuwataka kuwa na nidhamu ya pesa na kutumia fedha za serikali vizuri.

Rais Magufuli amesema hayo leo wilayani  Chato mkoani Geita alipokuwa akihutubia wananchi katika makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa, ambapo mbali ya kushukuru kwa msaada huo Rais Magufuli alizungumzia juu ya tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kuiba fedha za wananchi na kutumia katika mambo yao wenyewe nje ya malengo ya serikali.
"Hapa penyewe Chato kuna fedha zaidi ya bilioni moja za pembejeo zimeliwa na viongozi, hivyo natoa wito kwa viongozi wote wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kote nchini kuwa na nidhamu na fedha za serikali, tujifunze kutumia fedha vizuri  za serikali asitokee mchwa huko kula pesa za serikali. Maana hili lililotokea hapa Chato najua limetokea sehemu nyingi na hivyo saizi tunaanza kufanya ukaguzi kila sehemu" alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka wananchi wa hali ya chini kuwa na amani kwani katika kipindi chote ambacho yeye atakuwa madarakani hataki kuona wala kusikia wananchi wa hali ya chini wakinyanyaswa sababu na yeye ametokea katika maisha hayo hivyo anatambua jinsi wanavyopata shida watu wa kipato cha chini.

"Serikali haiwezi kufanya biashara na masikini, inawaacha matajiri inawasumbua masikini, mimi nimekuwa katika maisha ya shida nimechunga ng'ombe, nimeuza maziwa kwa hiyo najua maisha ni nini. Najua Tanzania watu wengi wanaishi maisha ya chini na katika kipindi changu sitaki kuona watu wa hali ya chini wanapata shida, wanapata taabu ndiyo maana tunajitahidi kuhangaika kuleta maendeleo ili wanufaike na wao" alisisitiza Magufuli

Rais Magufuli akuziacha taasisi ambazo zimekuwa zikitetea wanafunzi kupata mimba na kusema yeye taasisi hizo hazipendi na ameziwekea kizingiti kuwa ikiwezekana zisipewe msaada bali taasisi zinazofanya mambo ya kimaendeleo kama taasisi ya Mkapa Foundation ndiyo zinatakiwa kupewa msaada sana kwa kuwa zinarudi kuleta maendeleo kwa wananchi.

Visit website

VideoFUPI: List ya wachezaji 25 wa Everton wanaokuja Tanzania Rooney akiwemo

VideoFUPI: List ya wachezaji 25 wa Everton wanaokuja Tanzania Rooney akiwemo

millardayo.com / Rama Mwelondo TZA / 7 hours ago

Usiku wa July 11 2017 kikosi cha kwanza cha timu ya Everton ya England kimeanza safar ya kuja Tanzania kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Bingwa wa SportPesa Super Cup Gor Mahia ya Kenya, Everton ambao watawasili asubuhi ya July 12 wametaja majina ya wachezaji 25 wanaokuja Tanzania. Katika List ya majina ya wachezaji wa […]

Visit website

Diwani Arusha aitosa Chadema akieleza anamuunga mkono Rais Magufuli

Diwani Arusha aitosa Chadema akieleza anamuunga mkono Rais Magufuli

KAMGISHA / 4 hours ago

Diwani wa Ngabobo (Chadema), Solomon Laizer ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na CCM kwa maelezo anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Laizer ni diwani wa tano katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kutoa sababu kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Christopher Kazeri amethibitisha jana  (Julai 11) kupata taarifa za kujiuzulu kwa Ngabobo.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema kujiuzulu kwa diwani huyo ni mchezo mchafu akidai  amenunuliwa.

Amesema tayari walipata taarifa za diwani huyo kushawishiwa kujiuzulu na kwamba, alifuatwa na viongozi wa wilaya na kanda wa chama hicho aliowaeleza kuwa ameshawishiwa.

"Baadaye alieleza hataondoka lakini naona wamefanikiwa kumshawishi, tunashangaa viongozi wa Serikali badala ya kufanya kazi za maendeleo wanafanya kazi za kushawishi madiwani wa upinzani kuhama," amesema.

Hata hivyo, madiwani wanaohama wanapinga kuwa wameshawishiwa kufanya hivyo.

Hadi sasa madiwani watano wa Chadema waliojiuzulu ni Credo Kifukwe wa Kata ya Murieti jijini Arusha.

Wengine waliojiuzulu katika Jimbo la Arumeru Mashariki na kata zao kwenye mabano ni Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya (Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu).

Visit website

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya July 12

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya July 12

KAMGISHA BLOG/ 5 minutes ago

Visit website

Mwanamke amuawa Mumewe kwa Kisu,. Mwanza

Mwanamke amuawa Mumewe kwa Kisu,. Mwanza

KAMGISHA BLOG / 11 hours ago


Mwanamke mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumchoma mumewe na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa ni kisu na kumsababisha kupoteza maisha tukio lililotokea Julai 10 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Jenifer Shedafa (32) mkazi wa Magaka aliyemchoma mumewe Hosea Makoye (45) ambaye ni mfanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco Jijini Mwanza ambapo inasemekana kuwa wawili hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara ndani ya ndoa yao, hali ambayo iliyopelekea mwanamke kuwa na tamaa ya kutaka kurithi mali.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alitenda tukio hilo wakati wakiwa wamelala ndipo mwanamke alipoamka na kuanza kumvizia muwewe kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni na kisha kujipanga kwa ajili ya kutoroka eneo la tukio.

Inasemekana kuwa wakati Jenifer anatekeleza tukio hilo majirani walisikia kelele za kuomba msaada hali iliyopelekea kwenda eneo la tukio na kuweza kumkamata mwanamke huyo wakati anata kutoroka kisha wakatoa taarifa kituo cha polisi na kuweza kushirikiana na wananchi kumkimbiza marehemu Hospitali ya Rufaa ya Bugando lakini baadaye marehemu alifariki kipindi akiendelea kupatiwa matibabu.

Pamoja na hayo, DCP Msangi amesema kuwa polisi wapo katika mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.

Kwa upande mwingine, Msangi amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

UKWELI NA UCHUNGU

UKWELI MCHUNGU

Hakuna chochote katika maisha cha kupigania!

Nguo zako zile bora kabisa kuna mtu kwake ni matambara tu.

Akiba yako kwenye akaunti ya Benki ni sawa na mchango wa mtu katika sherehe tu.

Boyfriend au Girlfriend wako au  mchumba ni Ex wa mtu!

Hivyo ni nini hasa cha kujivunia?

Maisha ni mafupi sana na madogo mno kujisikia kuwa mkubwa ama bora kuliko mtu wengine.

"Tupo sote uchi hadi kufa" aliwahi kusema Steve Jobs. Gwiji muanzilishi wa iPhone(ambaye kwa sasa kifo kimemchukua kwa maradhi ya Cancer)

"Hakuna kitu kinachoweza kutuokoa sote Kukabiliwa na kifo".

Naumia kuona watu ambao hujivunia utajiri, uzuri, akili, kiwango cha elimu, umaarufu na vitu vingine vya tamaa za kimwili, kwani hakuna jambo umefanya la mafanikio katika maisha yako ambamo halijafanywa na mtu mwingine ama kupitia

Cheo unachomiliki ofisini leo kilikuwa kinamilikiwa na mtu mwingine kabla na kitatwaliwa na mtu mwingine baadaye, wala hujui  mtu huyo anaweza kuwa nani

Kuna jambo moja tu  la thamani la  kujivunia ambalo ni "MAISHA ndani ya Mwenyezi MUNGU Muumba".

HIVYO ni vema kuwa mwema kwa Jamaa zako na daima tengeneza Marafiki!

Daima kumbuka kwamba watu unaowakanyaga wakati ukiwa njiani kukwea ngazi kwenda juu huenda wakawa ni walewale utakaowakuta kwenye safari yako ya kuteremka ngazi

Hivyo jitahidi usiwe tatizo kwa watu wengine au kufanya maisha magumu kwa mwingine kwa kutumia nafasi yako, kwa sababu kwa wewe kufanya hivyo ipo siku watu hao hao wanaweza kuwa kikwazo kwako siku moja mbeleni.

Kumbuka,hata jani la mgomba wa ndizi kuna siku litanyauka na kuwa majani makavu yasiyo na ukijani tena!

Tafadhali usiwe na Ubinafsi, Wajulishe  marafiki wengine kuwa  sote tupo njia moja.

Kama siku moja utajisikia  kulia, niite. Sina ahadi ya kukufanya ucheke lakini naweza kulia na wewe.

Kama siku moja unataka kukimbia kwenda mbali usiogope simu yangu.Niite nami nakuahidi kukimbia bega kwa bega na wewe!

Lakini, kama siku moja utapiga simu yangu na haina majibu basi njoo kwangu, Huenda nakuhitaji wewe.      

Siku moja, mmoja wetu hatutakuwa naye hapa tena na utasikitika juu yake lakini ukiwa umechelewa kwani hutokuwa na nafasi hiyo tena!
Machozi yanaweza kukutoka!,lakini  itakuwa umechelewa. Kwa hiyo, mkumbushe na kumwambia kila mtu kama vile ambavyo mimi nimefanya!

Tuma kwa marafiki zako na wapendwa bila kujali mara ngapi unazungumza nao  au ukaribu wenu

Hebu fanya marafiki wa zamani wajue hujawasahau na marafiki wapya wajue hutowasahau kamwe.
🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾

Jumatatu, 10 Julai 2017

Chelsea yamuongezea muda wa mapumziko Diego Costa

Chelsea yamuongezea muda wa mapumziko Diego Costa

KAMGISHABLOG / 11 hours ago

Mshambuliaji Diego Costa amepewa muda zaidi wa kumpumzika na Chelsea, hatua iliyozidisha uwezekano kwamba huenda akaihama klabu hiyo majira haya ya joto.

Mhispania huyo wa miaka 28 amehusishwa na kuhaam klabu hiyo baada ya kufahamishwa na meneja Antonio Conte kwamba hayupo kwenye mipango yake.

Costa hakujiunga na wenzake kwa mazoezi Jumatatu.

"Iliafikiwa kati yake na klabu kwamba anafaa kuchukua siku zaidi kupumzika," taarifa kwenye klabu hiyo ilisema.

Costa anatarajiwa kutohudhuria mazoezi wiki hii.

Mshambuliaji huyo alikuwa mchezaji pekee ambaye hakufika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham kando na Antonio Rudiger, ambaye alijiunga na klabu hiyo Jumapili.

Costa aliwajulisha wanahabari kwamba Conte alikuwa amemwandikia ujumbe wa simu kwamba hakuwa kwenye mipango yake mwezi jana, na inaarifiwa kwamba msimamo wake haujabadilika.

Duru zimeeleza BBC kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania anakaribia kuihama klabu hiyo.

Costa alifungia Chelsea mabao 20 katika mechi 35 za Ligi ya Premia msimu uliopita na kuwasaidia kutwaa ubingwa wa ligi.

Amehusishwa na kurejea Atletico Madrid, licha ya klabu hiyo kuzuiwa kununua wachezaji wapya hadi Januari.

Costa alizaliwa Brazil na alikaa misimu minne Atletico kabla ya kujiunga na Chelsea kwa £32m mwaka 2014.

Je Lukaku ni usajili sahihi, Sanchez atabaki au ataondoka – maswali 6 yanayohusu timu 6 za juu EPL

Je Lukaku ni usajili sahihi, Sanchez atabaki au ataondoka – maswali 6 yanayohusu timu 6 za juu EPL

ShaffihDauda / Aidan Charlie / 4 hours ago

Msimu wa 2017-18 wa Premier League unaanza mwezi mmoja kutoka sasa. Huku dirisha la usajili likizodi kushika kasi na pre season zikiwa zimeanza tuangalie maswali 6 makubwa kwa kila timu iliyoshika nafasi 6 za juu katika EPL msimu uliopita. 

1. Chelsea: Je Conte atapata wachezaji anaowataka


Mwendo pole, mbinu ya kuingia kwenye soko la usajili taratibu imetoa matokeo mabaya, hasa wiki hii, baada ya mashabiki wa Manchester United kuwazidi ujanja na kumsaini Romelu Lukaku kutoka Everton. Mshambuliaji huyu alikuwa chaguo la kwanza la Antonio Conte kumbadili Diego Costa, hivyo kumkosa inamanisha inabidi Chelsea kurudi nyuma kuangalia options nyingine ili kutimiza mahitaji yao ya mshambuliaji. 

Kuelekea kurudi kwa Conte katika maandalizi ya msimu mpya Wiki hii, usajili pekee ambao wameufanya Chelsea ni wa Antonio Rudiger na Willy Caballero. Tiemoue Bakayoko anatarajiwa kusajiliwa pia, lakini uhamisho wake unachukua kuda mrefu kuliko ilivyotegemewa.. Conte mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na inaonekana hatofanya hivyo mpaka atakapopata kikosi anachokitaka. Presha sasa ipo kwa wakurugenzi Marina Granovskaia Michael Emenalo kutimiza mahitaji ya kocha wao. 
2. TOTTENHAM: Je Kyle Walker ataondoka?


Katika ukimya wa soko la usajili mpaka sasa, swali pekee la kujiuliza ni wapi Kyle Walker atakuwa akicheza soka itakapofika September. Manchester City wanataka kumsaini beki huyu wa kulia wa England. 

Walker ana mkataba wa muda mrefu na Spurs, na klabu hiyo ya kaskazini mwa London haina haraka ya kumuuza mchezaji yoyote kwenye kikosi chao labda Moussa Sissoko. Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy ni mfanyabiashara mgumu kwenye kuuza wachezaji. Uhamisho huu unategemea kwenda mpaka mwisho wa usajili. 
3. LIVERPOOL: Je Liverpool wataweza kushindana kwa usajili huu waliofanya? 


Katika siku yao, Liverpool inaweza kumfunga timu yoyote. Ilithibitika msimu uliopita, kikosi cha Jurgen Klopp kina rekodi bora dhidi ya timu 6 za juu za Premier League. Walipoanza vyema walianza kupewa nafasi kubwa ya kutwa ubingwa kabla ya majeruhi kuanza kuwa mengi na mchanganyiko wa ratiba na kutokuwa na reserves imara ya kulivuruga mipango yao.  
Walifanikiwa kumaliza ndani ya Top 4, hivyo watacheza mchezo mmoja wa Play Off ili kuingia hatua ya makundi ya Champions League. Ulaya ndio sehemu ambayo Liverpool wana rekodi bora zaidi, lakini Mohamed Salah ndio usajili pekee waliofanya katika dirisha la usajili. Klopp anabidi aongeze wachezaji kukidhi mahitaji ya kikosi chenye ushindani nyumbani na ulaya.

4. MAN CITY: Guardiola atafanyaje kikosi chake kiwe na furaha? 


Ikiwa City watapata wachezaji wote wanaowataka katika dirisha hili la usajili ukiunganisha kikosi kizuri kilichopo chenye washambuliaji  Sergio Aguero, Gabriel Jesus, Leroy Sane na Raheem Sterling na bado Pep Guardiola anamtaka Alexis Sanchez. Nyuma ya washambuliaji hao kuna viungo  Bernardo Silva, David Silva, Kevin De Bruyne, Ilkay Gundogan, Yaya Toure na Fernandinho.

Guardiola atakuwa na kikosi chenye nguvu, kitakachokuwa na uwezo wa kushindana katika Premier League na Champions League, lakini wengi wa wachezaji wana uwezo wa kucheza kwenye maeneo mengi kwenye dimba lakini wapo wataokuwa wanakosa furaha kutokana na kutokucheza maeneo ambayo wanayamudu zaidi. 
5. ARSENAL: Je Sanchez atabaki au ataondoka? 


Soko la usajili limeanza vyema kwa usajili wa Alexandre Lacazette, lakini mafanikio kwenye soko hili la usajili yatakuwa kuwabakisha waliopo. Alexis Sanchez bado hajasaini mkataba mpya na huenda akafosi kuondoka, jambo ambalo litaiweka Arsenal kwenye sehemu ngumu. Je wachukue mshiko kwa kumuuza mchezaji wao bora au wamlazimishe amalize mkataba wake ambao umebakia mwaka mmoja kabla ya kumpoteza kwa uhamisho wa bure?

Ikiwa klabu ipo serious na suala la kushindania ubingwa msimu ujao, basi kumbakisha Sanchez ni jambo lisilohitaji mjadala. Arsenal pia wana suala kama hili kwa Mesut Ozil, lakini kiungo huyo mjerumani anaenda kwenye mwaka mwisho wa mkataba wake japokuwa hana timu nyingi zinazomwania, jambo ambalo linawapa Arsenal urahisi wa kumbakisha. 
6. MAN UNITED: Je Lukaku ni usajili sahihi? 


Jose Mourinho ameweka imani yake kwa Romelu Lukaku kufunga magoli ya kuipeleka timu yake katika mbio za ubingwa. Wakiwa wamefunga magoli 54 katika mechi 38. United hawakufunga magoli ya kutosha msimu uliopita, wakiwa na Zlatan Ibrahimovic. Sasa ameondoka na Mourinho ameweka matumaini yake kwa Lukaku kuongoza safu ya ushambulizi. 
Hii itakuwa hatua kubwa kwa mshambuliaji wa Kibelgiji. Kufunga dhidi ya zenye hadhi ndogo katika Premier Keague, jambo ambalo amelifanya mara nyingi, lakini itakuwa jambo tofauti kabisa kufunga katika Champions League. Akiwa na miaka 24, Lukaku anatoa picha ya kuwa ataimarika zaidi, itakuwa ni kazi yake na Mourinho kuwathibitishia vinginevyo watu wenye mashaka dhidi ya Lukaku. 

Visit website

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya July 11

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya July 11

KAMGISHA BLOG/ 29 minutes ago

Visit website