Rasmi, Okwi Ametua Dar Kusaini Mkataba Simba
KAMGISHA BLOG / 33 minutes ago
Hatimaye ametua Simba. Baada ya kutajwa kwa muda mrefu kwenye vyombo vya habari kama tetesi za kurejea tena mitaa ya Msimbazi, Emanuel Okwi amewasili Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini mkataba wa kucheza Simba kuanzia msimu ujao.
Okwi amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa usiku wa Juni 24, 2017 akitokea Uganda akiwa ameambatana na mke wake na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu.’
Katikati ya juma hili Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe alionekana kwenye picha akiwa na Okwi jijini Kampala, Uganda wakifanya mazungumzo kwa ajili ya kumrejesha tena Okwi nchini.
Inatajwa Okwi atasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba kisha atarejea tena kwao Uganda kabla ya kurejea tena baadae kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara 2017-2018 pamoja na michuano ya kimataifa (Caf Confederation Cup).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni