JPM awaoneshea KidoleWASOMI.KAMgisha BLOG / 4 hours ago
Rais John Magufuli amewashangaa wasomi wa nchi hii na kuhoji ni namna gani elimu yao inaisaidia Tanzania.
Ameyasema hayo leo (Jumatatu) baada ya kupokea ripoti ya pili ya kamati ya mchanga wa madini.
Amesema wasomi hao wameshindwa kusimamia sheria na kuifanya Tanzania kupoteza kiasi kikubwa cha fedha za kodi.
Amesema ni lazima serikali ichukue maamuzi magumu bila kujali yanamhusu nani.
“Pale Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuna Phd 17, tuna wanasheria wengi wamefundishwa na Profesa Kabudi lakini wamefundishwa nini? Wakirudi huku wanapindisha sheria tu,” amehoji.
Ameongeza; “This is the country, tumelogwa na nani, basi mkatuombee wachungaji kama ni mapepo yakaondoke.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni