Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 26 Aprili 2019

Jinsi ya kutengeneza App ya Android kwa kutumia Smartphone

Jinsi ya Kutengeneza App ya Android kwa Kutumia Smartphone

Kwa kutumia njia hii utaweza kutengeneza app ya Android yenye kufanya kazi

by Amani Joseph
about a year ago
5.2k Views 30 Comments

Katika ulimwengu huu ambao simu za mkononi zinatumika kwenye kila kitu ni wazi kuwa, baadhi ya vitu sasa vinawezekana kufanyika bila kutumia kompyuta. Kwa siku ya leo tutaenda kujifunza jinsi ya kutengeneza programu za Android kwa kutumia simu yako ya mkononi.

Kwa kuanza basi ili kuweza kufanikisha hili unaitaji simu yoyote ya Android pamoja na bando angalau MB 500 au zaidi, hii ni muhimu sababu ni lazima ujaribu kila sehemu ili uweze kupata kile unacho hitaji kwenye app yako hivyo ni muhimu kuwa na bando ya kutosha.

Kama tayari una bando la kutoka basi twende tukaanze somo letu la leo, lakini awali ya hapo labda nikuonyeshe picha za programu ambayo nimetengeneza kwa kutumia simu yangu ya mkononi, unaweza kudownload app hii HAPA ili kujionea mwenyewe.


Kwa kuanza basi ingia kwenye kisakuzi cha Google chrome kisha ingia kwenye tovuti ya www.andromo.com kishanga utapelekwa kwenye ukurasa maalum, bofya kitufe chenye mistari mitatu kilichoko juu upande wa kulia kisha bofya sehemu iliyo andikwa Sign Up, baada ya hapo utaletewa fomu yenye sehemu ya kujaza, jaza fomu hiyo ili kujiunga na tovuti ya Andromo na hakikisha unatumia barua pepe (email) sahihi.

Baada ya kuhakiki barua pepe yako na kuruhusiwa kuingia kwenye tovuti hiyo, sogea chini kidogo kisha utaona sehemu imeandikwa Create New App, bofya hapo kisha chini ya Project name andika jina la App unayotaka kutengeneza kisha bofya Create.

Baada ya hatua hiyo utaletwa kwenye ukurasa unao anza na Settings kutoka upande wa kushoto, bofya hapo kisha shuka chini kidogo mpaka mahali palipo andikwa Target Market, hapa ni vyema kuwa makini sababu app hii unayo tengeneza sasa utaweza kutuma Play Store sababu mpaka sasa hii ni akaunti ya bure unayo tumia, hivyo kwenye sehemu ya Target Market ni vyema kuchagua Samsung Apps au  Amazon Appstore kwani huko ndipo utaweza kutuma app yako.

Baada ya kuchagua Target Market shuka chini kidogo kwenye Category kisha chagua aina ya App ambayo unataka kutengeneza, chini yake kwenye sehemu ya Description hapa utajaza maelezo yoyote kuhusu App yako na kama huna malezo yoyote basi unaweza kuacha wazi. Baada ya kumaliza kuweka maelezo ya App yako shuka chini kidogo hadi sehemu iliyoandikwa App Icon.

Sehemu hii ni muhimu kwani hii ndio picha ya App yako hivyo kama tayari unayo picha ya App yako sasa ndio wakati wa kuiweka na uta bofya sehemu iliyo andikwa Choose File kisha chagua picha unayotaka ndani ya simu yako, hakikisha picha yako ina ukubwa wa 512×512 na iwe na format ya png. Baada ya kumaliza hatua hiyo shuka mpaka mwisho kabisa wa ukurasa huo kisha bofya kitufe cha Save Changes.

Kisha rudi juu kabisa mwa ukurasa kisha bofya Theme, hapo utaweza kuchangua rangi ya App yako, changua rangi zote mbili zifanane kati ya Primary Color na Accent Color, baada ya hapo shuka chini kidogo hadi sehemu iliyo andikwa  Body Style chagua kati ya Material Light kupata rangi nyeupe kwenye App yako na Material Dark kupata rangi nyeusi kwenye App yako. ukisha maliza shuka mpaka mwisho wa ukurasa huo na bofya Save Changes.

Baada ya hapo rudi tena juu kabisa kisha bofya sehemu iliyo andikwa Navigation, Shuka chini kidogo hadi sehemu iliyoandikwa Title kisha andika jina la App yako kisha sehemu ya Subtitle andika msemo wa App yako kwa ufupi kwa mfano “pepsi dare for more”, baada ya hapo chini ya Upload a Header Image bofya Choose File na weka picha unayotaka ionekana juu kabisa kwenye app yako, ukimaliza shuka mpaka mwisho wa kurasa hiyo alafu bofya Save Changes.

Baada ya hapo rudi juu kabisa ya ukrasa kisha bofya Dashboard, hapa ni vizuri kuwa makini shuka mpaka sehemu iliyoandikwa Startup Mode kisha chagua Show first activity(no dashboard) kisha bofya Save Changes. Kisha kama kawaida rudi juu kisha chagua sehemu ya Activities kisha bofya sehemu ya Add an Activity kisha fuat

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni