Nukuu (Quotes) 50 Zitakazokuhamasisha Maishani Mwako
B
Bujibuji
Yale tunayoyawaza na kuyatafakari kwenye fikra zetu yana nafasi kubwa sana kwenye maisha yetu. Ikiwa tunataka kufanikiwa basi ni lazima tufikiri na kutafakari juu ya kufanikiwa.
“Tunakuwa kile tunachofikiri”
Earl Nightingale
Vivyo hivyo ikiwa tunahitaji kuhamasika kufanya mambo mbalimbali maishani, ni lazima tusome, tusikilize, tutazame na hata tutafakari vitu vitakavyotuhamasisha.
Karibu nikufahamishe nukuu 50 (quotes) ambazo zitakuhamasisha katika maswala mbalimbali unayoyafanya maishani mwako.
“Chochote ambacho akili ya binadamu inaweza kuumba na kufikiri, inaweza kukikamilisha pia.”
Napoleon Hill
“Njia ya kuanza ni kuacha kuzungumza na kuanza kutenda.”
Walt Disney
“Usiruhusu jana itawale sana leo.”
Will Rogers
“Kama unafanyia kazi kitu kinachokusisimua na unachokijali kweli, hauhitaji kusukumwa. Maono yako yatakusukuma.”
Steve Jobs
“Kufahamu haitoshi, ni lazima tuweke kwenye matendo, Kutamani haitoshi, ni lazima tufanye.”
Johann Wolfgang
“Tunatengeneza hofu tunapokaa bila kufanya kitu. Tunaishinda hofu kwa matendo.”
Dr. Henry Link
“Ikiwa unafikiri unaweza au huwezi, uko sahihi.”
Henry Ford
“Mtu mwenye kujiamini ndani yake, anapata kujiamini kwa wengine.”
Hasidic Proverb
“Fanya kile unachoweza kwa vyote ulivyonavyo, popote ulipo.”
Theodore Roosevelt
“Akili ni kila kitu. Unavyofikiri ndivyo unavyokuwa.”
Buddha
“Muda mzuri wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita. Lakini muda mwingine mzuri wa pili ni sasa.”
Chinese Proverb
“Muda wako ni mdogo, usiupoteze kuishi maisha ya mtu mwingine.”
Steven Jobs
“Kushinda siyo kila kitu, lakini kutaka kushinda ni kila kitu.”
Vince Lombardi
“Huwezi kuvuka bahari kama huna ujasiri wa kuacha kuona ufukwe.”
Christopher Columbus
“Kisasi kizuri ni mafanikio makubwa.”
Frank Sinatra
“Kuna njia moja tu ya kuepuka kukosolewa: usifanye kitu, usiseme kitu na usiwe chochote.”
Aristotle
“Anzia ulipo. Tumia kile ulichonacho. Fanya kile unachokiweza.”
Arthur Ashe
“Anguka mara saba simama mara ya nane.”
Japanese Proverb
“Mlango mmoja wa furaha ukifungwa, mwingine unafunguliwa, lakini mara nyingi tunautazama sana ule uliofungwa na kushindwa kuona ule uliofunguliwa kwa ajili yetu.”
Helen Keller
“Kila kitu kina uzuri wake, lakini siyo kila mtu anaweza kuuona.”
Confucius
“Changamoto zinafanya maisha yavutie na kuzishinda ni kufanya maisha kuwa na maana.”
Joshua J. Marine
“Kama unataka kujiinua mwenyewe juu, mwinue mwingine juu kwanza.”
Booker T. Washington
“Ili kufanikiwa, shauku yako ya mafanikio ni lazima iwe kubwa kuliko hofu yako ya kushindwa.”
Bill Cosby
“Kila siku ninajitahidi kufanya vizuri zaidi kuliko nilivyo fanya jana.”
Reginald Mengi
“Mtu ambaye hajawahi kufanya kosa hajawahi kujaribu kitu chochote.”
Albert Einstein
“Mtu anayesema hawezi kufanya hatakiwi kumwingilia mtu anayesema ninaweza kufanya.”
Chinese Proverb
“Haujachelewa kuwa ambaye ungeweza kuwa.”
George Eliot
“Unakuwa kile unachoamini.”
Oprah Winfrey
“Jenga ndoto zako wewe mwenyewe, la sivyo mtu mwingine atakuajiri kujenga zake.”
Farrah Gray
“Ota ndoto kubwa na dhubutu kushindwa”
Norman Vaughan
“Badili kufikiri kwako na utakuwa umebadili ulimwengu.”
Norman Vincent Peale
“Andika kitu chenye manufaa kusomwa au fanya kitu chenye manufaa kuandikwa.”
Benjamin Franklin
“Njia pekee ya kufanya kazi nzuri ni kupenda kile unachokifanya.”
Steve Jobs
“Ikiwa unaweza kuliota, unaweza kulifanikisha.”
Zig Ziglar
“Ndoto zetu zote zinaweza kutokea ikiwa tuna ujasiri wa kuzifuata.”
Wale Disney
“Usilie juu ya kile ambacho huna; tumia vizuri kile ulichonacho.”
Reginald Mengi
“Mambo mazuri huja kwa watu wanaosubiri, lakini mambo bora huja kwa wale wanaoondoka na kwenda kuayachukua.”
Hajulikani
“Fursa hazitatokea, unatakiwa kuziunda.”
Chris Grosser
“Usijaribu kuwa mtu wa mafanikio, bali jaribu kuwa mtu wa thamani.”
Albert Einstein
“Akili kubwa hujadili mawazo, akili ya wastani hujadili matukio, akili ndogo huzungumzia watu.”
Eleanor Roosevelt
“Ikiwa hauthamini muda wako, hata wengine hawatauthamini. Acha kupoteza muda na vipaji vyako sasa – anza kuvifanyia kazi”
Kim Garst
“Mtu mwenye mafanikio ni yule anayeweza kujenga msingi imara kwa kutumia matofali yaliyotupwa na wengine.”
David Brinkley
“Usiinue sauti yako, boresha hoja yako.”
Hajulikani
“Ninaamini kwamba ujasiri pekee mtu yeyote anaouhitaji ni ujasiri wa kufuata ndoto zako mwenyewe.”
Orarah Winfrey
“Fursa zina aibu, zinakusubiri uzikimbilie.”
Reginald Mengi
“Ubunifu unatofautisha kati ya kiongozi na mfuasi.”
Steve Jobs
“Hofu ni mojawapo ya adui mkubwa kwa mafanikio.”
Reginald Mengi
“Wengi wetu hatuishi ndoto zetu kwa sababu tunaishi hofu zetu.”
Less Brown
“Hatua ya mwanzo ya mafanikio yoyote ni matamanio.”
Napoleon Hill
“Baadaye inamilikiwa na wale wote wanaoamini kwenye uzuri wa ndoto zao.”
Eleanor Roosevelt
Naamini umehamasika na kufurahia nukuu hizi za hamasa. Ni wazi kuwa kila kitu kinaanza kwenye fikra zetu – tunavyowaza ndivyo tunavyokuwa.
L
lucas mobutu
Uzi mzuri. Angalau tusahau nyuzi za mapenzi na za kuwalalamikia wadada wa JF
M
Madame B
Wazungu waongo tu
L
lucas mobutu
Naona namba 15 jamaa aliongea kitu kizuri
M
m.k
nimeipenda hii
S
Sokoro waito
Wazungu waongo tu
kwani hizo nukuu zote ni za wazungu mkuu? mbona zimo za waafrika kama Mengi, zimo za wajapani, zimo za wachina n.k
Nimezipenda maana zina ukweli unaofuatwa na wachache.
M
Madame B
kwani hizo nukuu zote ni za wazungu mkuu? mbona zimo za waafrika kama Mengi, zimo za wajapani, zimo za wachina n.k
Nimezipenda maana zina ukweli unaofuatwa na wachache.
Ohhhhh
Basi mie nimeangalia mwanzo kati na mwisho nikanua hawa wazungu tu
S
Sokoro waito
Ohhhhh
Basi mie nimeangalia mwanzo kati na mwisho nikanua hawa wazungu tu
okay pole kwa hilo Madame B, hujambo lakini?
D
dagii
Ndefu sana soma mwenyewe
S
shushushu VIP
Nukuu nzur hizo
M
Mother Confessor
"Maarifa ni bora kuliko Hazina"
~Mother Confessor ~
K
Khaligraph Jordan
Ahsante kwa kunipunguzia machungu
M
Madame B
okay pole kwa hilo Madame B, hujambo lakini?
Asante mpendwa.
Mimi sijambo Sokoro, za kwako
S
Sokoro waito
Asante mpendwa.
Mimi sijambo Sokoro, za kwako
nzuri tu mkuu, amani kwako.
M
Madame B
nzuri tu mkuu, amani kwako.
Mia mia....mie niko kamshange, full kundonda.
Hainaga mbaya mkuu
T
The Icebreaker
Wazungu waongo tu
Ukweli ni upi?
S
Sokoro waito
Mia mia....mie niko kamshange, full kundonda.
Hainaga mbaya mkuu
sijakuelewa hapo kwenye bold mkuu
M
MIXOLOGIST
Mkuu, wapi wahenga wa zamani? mambo ya:
ndondondo si chururu
ngaagaa na upwa ali wali mkavu
kila mtoto ana riziki yake
Hawa wahenga wetu wahawakuwa wamejipanga?
M
Madame B
sijakuelewa hapo kwenye bold mkuu
Hapo ni kwamba niko mzima, sina wasi, niko poa tu.
Salamu za vijana wa Dar hizi
S
Sokoro waito
Hapo ni kwamba niko mzima, sina wasi, niko poa tu.
Salamu za vijana wa Dar hizi
teh teh nimekupata mkuu
Get involved!
Here you can only see a limited number of comments. On JamiiForums you see all comments and all functions are available to you.TO THE THREAD
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni