Sababu za wachezaji wa Tanzania kukosa nafasi nje ya nchi, Samatta ameeleza
KAMGISHA BLOG / 23 hours ago
Licha ya wachezaji wa kitanzania kuwa na vipaji vikubwa ambavyo vinaweza kuwafanya wakacheza soka la kulipwa nje ya Tanzania na Afrika lakini bado imekuwa ngumu kwa wachezaji hao kupata nafasi.
Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta amezungumzia ugumu uliopo katika kupata nafasi za kutoka nchini na kucheza soka la kulipwa.
“Wachezaji wengi wa kitanzania wana vipaji vikubwa na vya kuvutia,ni vigumu kuvipata sehemu nyingine labda unaweza ukataja nchi kama Brazil lakini hatukuanza nyuma.”
“Mababu zetu huko nyuma hawakutupa njia nzuri ya kutufanya leo hii sisi tujidai. Hata kama tusingekuwa na wachezaji wengi Ulaya lakini tungekuwa na historia kwamba walishawahi kupita wachezaji wengi waliovuma Ulaya kutoka Tanzania ingekuwa ni rahisi kwa mchezaji wa kitanzania kupata nafasi Ulaya na tungekuwa na idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza nje kuliko tuliyonyo sasa hivi.”
“Wachezaji wanavipaji lakini njia imekuwa ngumu na kama unavyojua, nchi zamani haikuwa na wachezaji wengi Ulaya hata mawakala nao inakuwa ni vigumu kuja kuangalia vipaji, ila taratibu nadhani tutafanikiwa.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni