Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 5 Machi 2017

Kwako wewe Mwanamke ambaye huko kwenye mausiano

Kama wewe ni mwanamke na haujaolewa na upo kwenye mauhusiano na mwanaume ambaye haujafunga naye ndoa  basi zingatia haya walau, yanaweza kukusaidia na kukupa nuru nzuri ya ndoa bora yenye tija katika maisha yako ya mahusiano.

Daima chagua mwanaume bora kwa kutizama utashi wake na mawazo yake chanya, mwanaume bora ni yule aliyekuzidi utashi, tabia nzuri pamoja hekima na busara na mwenye mapenzi ya dhati kwako.

Mwanaume anayekufaa ni yule  anayekujali  na kukuheshimu, mwanaume bora ni yule anayekupa leo mawazo ya kesho, mwanaume anayekufaa ni yule anayekufuta machozi na asiyekuliza kila siku, na aonapo chozi lako basi huwa anaumiaa sana.

Dada yangu tafuta mwanaume ambaye ni kichwa ili wewe uwe shingo sababu hakuna kichwa pasipo shingo.

Tengeneza mwanaume wako bora, anza naye kwenye maisha ya chini mkipeana faraja na matumaini ya kutengeneza ndoa bora na yenye mafanikio ya kipesa, na mauhisiano yenye afya yaliyo na mapenzi matamu na bora, usipende wanaume wa wanawake wenzio mtengeneze handsome wako.

Dada yangu achana na mabrothermen wanaopaka poda, wanaotembea na selfiestick  hawana tija, mwanaume bora havai mlegezo (sag trouser).

Mwanaume bora hata kama hana pesa daima huwa na hazina ya mawazo na ndoto zenye matumaini ya kuwa na future nzuri baadae.

Achana na wanaume maarufu,   wengi wao hawana mapenzi ya dhati japo si wote. Wanapenda kuwatumia wanawake kwa tamaa zao za mwili.

Dada yangu mimi nakupenda na natamani uwe na ndoa bora na uchague mpenzi bora, mpende mpenzi wako kwa moyo wote achana na zile kauli za wanaume wote wanafana.

Muombe Mungu akupe mume bora na wewe uwe mke bora sababu mke mwenye mapenzi ya dhati huwa anabeba baraka za mafanikio ya mume wake ... Tafakari mauhusiano yako yapoje ....!

Wakati ni sasa sio kesho acha kuwa na idadi kubwa ya wanaume, chagua mwanaume wako mmoja na aliye bora, pia achana na utamaduni wa kuchati na ma ex wako .

Tengeneza mume wako bora achana na wanaume wadhaifu na wasio na tija kwako chagua mwanaume bora kwa sifa za ndani na sio kwa ubora wa nje.

You know what...!?
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
"If a girl ever steals your man, there’s no better revenge than letting her keep him. Real men can’t be stolen."

Share

Like Page

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni