Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Yako Ndogo Na Ikakutoa Kimaisha
kamgisha blog / 7 minutes ago
Je unawazo la kuanzisha biashara yako, lakini hujui aina ya biashara itakayokutoa kimaisha? hapa chini kunanjia muhuimu zitakazokusaidia ili uweze kuanzisha biashara yako ndogo itakayokuwezesha kusonga mbele kimaisha.
Huenda ukawa umegundua kuwa kuna mawazo au aina milioni moja za biashara, lakini ukachagua wazo moja tu, ambalo hilo utakuwa umefanya maamuzi magumu na yapekee kulipa kipaumbele. Japokuwa haina haja ya kulipa kipaumbele wazo moja tu na kuliona ndilo la pekee katika kuanza biashara yako ndogo.
Wazo lolote lile la biashara ulilochagua, ningependa kukushauri kuwa usianzishe biashara ambayo ni maarufu kwa wakati huo, biashara ambayo inafanywa kwa kiasi kikubwa na wafanya biashara walio wengi. Ukifanya hivyo utawanufaisha wafanya biashara wakubwa kwanza halafu wewe utakuwa wa mwisho. Hapo chini ni mbinu au njia chache zitakazokusaidia ili uchague wazo (idea) zuri la kuanzisha biashara yako ndogo.
Wazo lako la kuanzisha biashara yako, ni lazima litokane na sehemu ya shughuli zako ambazo tayari ni sehemu ya maisha yako, shughuli mbazo tayari unazifurahia kuzifanya kila kukicha. Unapaswa kufanya kitu unachokipenda kutoka moyoni, kitu ambacho kinakufurahisha kila kukicha. Kwa mfano, mimi mwenyewe tofauti na kazi yangu, tumechukua muda na kutengeneza blog hii, kwasababu hutufanya tujisikie wenyefuraha tunapoifungua kila siku na kuandika kitu kikasomwa na watu wengi sana kwa siku.
Pia unatakiwa kujifunza mengi zaidi kuhusiana na wazo lako la biashara uliloliteua. Lifanyie utafiti wakutosha, kwani unavyozidi kujifunza mengi, ndivyo unazidi kuwa mzoefu katika kuanzisha biashara yako. Ukifanya hivyo utaanza biashara yako ukiwa na uzoefu wa hali ya juu na mafanikio yatakuwa upande wako siku zote.
Kitu muhimu: Wazo lako la kuanzisha biashara lazima liendane na mahitaji ya wateja au wanunuzi. Endapo kama haliendani au kukidhi mahitaji ya watu, basi hakuna mtu atakaye kuja kununua bidhaa yako au huduma yako. Hivyo fanya kwanza utafiti kabla ya kuanza. Hakikisha unafanya utafiti wa mahitaji ya wateja, hata ikiwezekana waulize watu wa eneo hilo mahitaji wanayohitaji kununua ndipo uanzishe biashara yako.
Mwisho kabisa, katika dunia hii asikwambie mtu, biashara ni matangazo, bila matangazo ni sawa na bidhaa bila mnunuzi. Fanya hima tangaza biashara yako katika vyombo mbali mbali vya habari, utaona manufaa ya kazi yako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni