Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 13 Desemba 2016

Je, umekosea Tumaini

Je, Umekosa Tumaini La Kufanikiwa? Jifunze Kupitia Mambo Haya
KAMGISHA BLOG / 19 minutes ago

Kipo kipindi katika safari yako ya mafanikio kutokana pengine na changamoto za kimaisha, unajikuta unakata tamaa na matumaini yote yanapotea.

Katika kipindi hiki, kila unachokifanya kinakuwa hakileti matokeo na mbele yako unakuwa unaona giza na hakuna hata njia wala mwanga wa matumaini. Je, kwa hali  kama hii inapokutokea unafanyaje?

Kwa mfano, tuchukulie umeanzisha mradi fulani, lakini umejitahidi sana ili ukuletee angalau faida imeshindikana, hapo inapokuwa hivyo unawaza nini au unachukua hatua gani?

Najua kuna mambo mengi yanakuwa yanapita kichwani mwako, ikiwa nia pamoja na kuachana kabisa na kitu hicho ambacho sasa unaona hakifai tena na hakina manufaa kwako.

Lakini leo hapa kwa kupitia makala haya, naomba nikushirikishe mambo ya msingi ya kujifunza hasa inapotokea pale umekata tamaa na kukosa matumaini  kwa kile unachokifanya.

Jambo la kwanza unalotakiwa kujifunza na kulitambua  ni kwamba hakuna mafanikio ya mara moja. Hapa hii yote inatuonyesha ili tuweze kufanikiwa inatakiwa tujaribu tena na tena hadi kufikia mafanikio.

Inapotokea unaona kama umekosa tumaini unaonyeshwa kwamba sasa huu sio wakati wa kutulia na kujiona mnyonge uliyopotezakila kitu, bali ni wakati wa kunyanyuka tena na kujaribu njia zingine za kukupa mafanikio yako.

Jambo la pili unalotakiwa kujifunza ni kwamba katika maisha hakuna kukata tamaa. Ni kweli, unakuwa unajiona umekosa matumaini na huna chako tena, lakini ni wakati wako wa kijiamini tena na kushikiria ndoto yako mpaka kufanikiwa.

Hata kama unaona dunia na kila hali kama imekutenga, jifunze hapo ulipo sio ndio mwisho wa mafanikio yako ipo nafasi ya kufanya tena na ukafanikiwa sana kuliko unavyofikiri.

Jambo la tatu la kujifunza hasa pale unapokosa matumaini tena ni panga mipango yako upya. Hiki hasa ndicho kitu ambacho unachokuwa uanaambiwa na maisha.

Badala ya kukaa chini na kulia na kunza kulalamika kwa kushindwa kwako kufanikiwa, lakini unachoambiwa na maisha panga mipango yako upya, tafuta njia nyingine na tumia akili yako vizuri hadi ufanikiwe.

Tambua ili kufanikiwa inatakiwa ujue hakuna mafanikio ya mara moja, hakuna kukata tamaa na inabidi kila wakati kupanga mipango upya.  Hayo ndiyo mambo ya msingi  unayotakiwa ujifunze hasa pale unapokata tamaa na kukosa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni