Chanzo cha saratani ya matiti
KAMGISHA BLOG / 10 hours ago
Hakuna kitu kingine kizuri kama mwili wa mwanamke kwakuwa unaweza kuleta kiumbe binadamu kingine.
Mwili wa mwanamke unazo ovari ambazo hutengeneza mayai na homoni maalumu ambazo hudhibiti mwili wake wakati wa ujauzito kuanzia wakati yai linaporutubishwa mpaka mwishoni mwa wastani wa miezi tisa (wakati wa kujifunguwa).
Mfumo huu maalumu huanza kazi mara mwanamke anapoanza mzunguko wake wa uzazi (mzunguko wa hedhi). Kwa wastani kila siku 30 ovari zake zitazarisha yai na kuliweka katika mfumo wake wa uzazi likisubiri kurutubishwa.
Wakati yai hili limetolewa, mwili wake utaanza kujiandaa kwa uwezekano wa kupata mtoto.
Mfuko wa uzazi (uterus) utaanza kubadili uundwaji wake wa seli kwa kuandaa uwezekano wa kukishikilia kijusi (fetus) baada ya yai kurutubishwa. Wakati yai litakapokuwa limerutubishwa ovari zake (mwanamke) zitachukuwa majukumu ya mwili wake na kuhakikisha kuwa kijusi kinapata kile kinachokihitaji ili kuishi.
Ubongo wa mwanamke pia huathiriwa kutokana na kutolewa kwa homoni hizi maalumu wakati wa ujauzito. Hii ndiyo sababu wanawake hupata mabadiliko ya kihisia (moody) na huwa walioamka zaidi kuliko wanaume wakati wa ujauzito. Wakati mwingine bila hata sababu wanawake wote wanaweza kuonekana kama wenye huzuni, hulia, hupiga mayowe na lisaa limoja baadaye kuwa wakicheka, wakitabasamu na kuwa tayari kusonga mbele.
Hali yake pia katika tendo la ndoa huweza kubadilika sababu ya kutolewa kwa homoni hizi. Wanawake wapo katika mfadhaiko zaidi kuliko wanaume kwa sababu siku hizi wanawaku siyo tu husimamia watoto, bali pia wanalisha familia zao na kuwaangalia waume zao. Wanawake huhofia zaidi afya za familia zao na masuala ya fedha. Siku hizi Wanawake pia ni waajiriwa kamili (full time employees).
Mfadhaiko (stress) unaweza kumgharimu mwanamke yeyote siku hizi sababu ya kukosa muda wa ziada: nenda tu, nenda, fanya kazi, kazi kazi, hakuna muda, hakuna muda. Mwili wa mwanamke unaweza kuzitoa homoni zitakazomuwezesha kuendelea kwa kukopa kile inachohitaji toka sehemu nyingine ya mwili kuiwezesha sehemu nyingine mhimu zaidi kuendelea kufanya kazi zake kawaida. Hii ndiyo sababu wanawake huishi zaidi ya wanaume.
Katika safari hii ya kukopa ikiwa sehemu iliyokopwa haikurudishiwa vitu vyake kwa muda muafaka mwili wake (mwanamke) huanza kufeli na sasa ataanza kupata baadhi ya aina ya matatizo (kuugua).
Mfadhaiko wa kwanza mwili wa mwanamke unapaswa kushughurika nao ni mzunguko wake wa uzazi (reproductive cycle). Miili yao huitoa homoni iitwayo prolaktini (prolactin) kuuwezesha mwili kuhimili mabadiliko hayo.
Mwili wa mwanamke pia utaitoa homoni punguza maumivu (pain killer) iitwayo ‘endorphins’. Mwanamke anaweza kuhimili zaidi maumivu kuliko awezavyo mwanaume sababu ya endorphins nyingi alizonazo sababu ya kupewa jukumu la kujifunguwa mtoto.
Wakati mzunguko wa uzazi umeanza homoni huzarishwa toka katika ubongo (hypothalamus) ikiyaambia matiti kujiandaa kwa ajili ya kutengeneza maziwa kwa ajili ya mtoto mtarajiwa. Kwahiyo tishu za matiti lazima zibadilike na hivyo kusababisha uwezekano wa kutokea kwa homa, kuvimba na kujisikia kuongezeka uzito wa matiti..
Wakati seli za mafuta za matiti zinaanza kubadilika, huhitaji mzunguko zaidi wa damu unaozipelekea vitamini mhimu, madini, asidi amino na maji yenye elektrolaiti. Kwahivyo matiti yatakuwa na uwezo wa kusaidia mahitaji yote ya mtoto katika kutengeneza maziwa. Maziwa ya matiti ya mama yatamruhusu mtoto kukuwa na kubaki katika afya kwa mwanzoni mwa miezi ya kwanza ya uhai wake mpaka hapo atakapoweza kuanza kula vyakula vigumu.
Kansa ya matiti inaweza kuanza wakati tishu hii au mzunguko umechanganywa kama matokeo ya kupewa ishara zinazogongana, tishu inaanza kuandaa seli za mafuta kwa ajili ya maziwa kutengenezwa na wakati huo huo inaamriwa kusimama, kuanza upya au kuanzia pale iliposimamia wakati mwingine uliopita.
Ishara hizi (homoni) mbaya zinazogongana zinaweza kusababishwa na:
Kutumia vidonge vya kuzuia ujauzito kwa miaka mingi.
Kunywa alikoholi (pombe) kupita kiasi
Kunywa kahawa au vinywaji vyenye kafeina kupita kiasi
Kutumia viongeza utamu vya kutengenezwa (artificial sweeteners).
Ikiwa tezi ya pituiatari au ‘hypothalamus’ katika ubongo inakosa lishe kamili, inaweza kutoa homoni isiyotakiwa au kutoa homoni wakati ambao haikutakiwa na hivyo kuzipelekea seli za matiti kufeli na hivyo kuleta seli zisizo za kawaida za matiti kutengenezwa (kansa)..
Katika baadhi ya wanawake, kitendo cha kula vyakula ambavyo vina homoni ndani yake vinaweza kutuma ishara (ujumbe) kuharibu jozi ya maagizo yaliyokwisha tolewa tayari na hivyo kupelekea kutokea kwa vivimbe au hata kuzarishwa kwa seli zisizo za kawaida ziwezavyo kugeuka kuwa kansa ya matiti.
Baadhi ya madawa ya hospitalini yana madhara hasi yawezayo kuvuruga ishara (homoni). Ikiwa damu ya mwanamke inakosa vitamini au madini mhimu, basi baadhi ya seli hizo za mafuta hazitaweza kubadilika kabisa kuwa seli zinazoweza kutengeneza maziwa, hupumuzishwa na zingine mpya kutengenezwa kuchukuwa nafasi. .
Ikiwa kinga ya mwili iko bize sana (kuondoa) kula seli mbovu, basi inaweza kuweka uzio (fence) kuzunguka seli hizo mbovu mpaka itakapozila kwa mara ya pili (recycle and eat up the bad cells). Seli hizo mbovu zilizozungushiwa uzio ndizo tunazoziita vivimbe katika matiti na katika hali nyingi baada ya miaka kadhaa vitapotea kadiri kinga ya mwili inavyorudi na kuvirudia kuvila tena.
Ikiwa seli hizi za mafuta zimekuwa mbaya sababu ya kuwa na asidi iliyozidi sababu ya kukosa maji na kupokea ishara zinazogongana nyingi na asidi hii inakula katika fungu la maagizo (blue print) katika DNA, itabadilisha maagizo (code) na hivyo utapata kutengenezewa seli mafuta za matiti zisizo za kawaida (kansa) na zinaweza kukuwa na kusambaa mwili mzima.
Vifundo limfu nyuma ya mikono vitaziteka seli hizi zisizo za kawaida mpaka limfu itakaposhindwa kuzishikilia zaidi na kisha sasa zinaweza kutembea kwa uhuru wote kwenda sehemu nyingine ya mwili.
Wanyama wengi tuwalao siku hizi (kuku,ng’ombe n.k) wanalishwa homoni kurekebishwa kijenetiki ili kuharakisha kukuwa kwao na kuongezeka uzito kwa haraka. Homoni hizi na mabadiliko yao kijenetiki vimo katika nyama na vinapoliwa vinaweza kuathiri tishu za matiti au ogani za uzazi kwa baadhi ya wanawake.
Moja kati ya madhara makubwa ya kula kiasi kingi cha mafuta ya mboga mboga (polyunsaturates) ni kuhusika kwake na kansa. Katika tafiti toka kliniki ya Mayo, iligundulika kuwa watu wanaosumbuliwa na kansa ya matiti walikuwa pia na ongezeko la mafuta yatokanayo na mboga mboga katika tishu za matiti yao kama ilivyojitokeza katika plasma ya damu zao.
Soya na baadhi ya maharage vinaweza pia kuwa na homoni zinazoweza kuathiri baadhi ya matiti ya wanawake (mfumo wa uzazi). Ninashauri kwa nguvu zote wanawake wote kusoma kitabu kilichoandikwa na Dr Carolyn De Marco kiitwacho “Take charge of your body” kinachozungumzia zaidi mambo haya na zaidi.
Ni mhimu zaidi kwa wanawake kufanya zoezi binafsi la kuchunguza matiti yao, wakiangalia kila titi kwa kufuatisha zoezi rahisi la vidole vitatu. Kwanza katika duara kisha katika wima, kukaguwa kwa ajili ya mabadiliko yeyote ya kifiziolojia, vivimbe, mkazo au mabadiliko ya rangi, ikihusisha kuvuja kwa chuchu, saizi na rangi.
Mazoezi haya rahisi yanapatikana katika intaneti na maonyesho mengine, yanaonyesha namna gani ya kufanya zoezi la kujikagua kwa kutumia video rahisi.
Ikiwa mabadiliko yeyote yatagundulika, tafuta ushauri wa kidaktari mapema kadili iwezekanavyo.
Kuna umhimu wa uchunguzi wa matiti kwa eksirei?
Uchunguzi wa matiti kwa eksirei (mammograms) mara nyingi imedhaniwa kama ‘’mwokozi wa maisha’’, namna ya kuskrini kansa inayohusika kupunguza vifo vitokanavyo na kansa kwa wastani wa asilimia 15 mpaka 25. lakini faida hizi zilizolipotiwa zinaegemea tafiti zilizopitwa na wakati zilizofanyika miongo iliyopita.
Mwezi Septemba 2010, the New England Journal of Medicine, moja kati ya majarida ya afya yanayoheshimika duniani, lilichapisha taarifa ya kwanza ya utafiti wa hivi karibuni ulioangalia ufanisi wa mammograms, na majibu yao yapo tofauti sana na yale maofisa wengi wa afya na wanafizikia wangekufanya uamini.
Hitimisho lake lilikuwa kwamba mammograms ingekuwa imepunguza vifo vitokanavyo na kansa kwa wastani wa vifo 0.4 kwa wanawake 1000—idadi ambayo ni ndogo sana ambayo inaweza kuwa hata 0. Ukiacha hilo, wanawake 2,500 watatakiwa kuwa wameskriniwa kwa zaidi ya miaka 10 kwa kifo kimoja cha kansa ya matiti inayolengwa kuepukika.
Ni jambo linalojulikana wazi kuwa uionishaji miale huongeza mabadiliko ya ki-seli ambayo hupelekea kansa—na mammograms inalenga zaidi dozi inayoenda moja kwa moja katika matiti yako, kitu kinachoongeza hatari ya kupata kanza!.
Kwanini lazima ungetaka kufanya hivi?
Mammograms huuweka mwili wako katika miale inayoweza kuwa mikubwa mara 1000 kuzidi ile ya eksirei ya kifua, ambayo tunajuwa huongeza uwezekano wa kutokea kansa. Teknolojia ya kutumia picha za miale kukaguwa vivimbe vya kansa pia huyabana matiti yako kwa nguvu na mara nyingi ikiambatana na maumivu ambayo yanaweza kupelekea kuongezeka mauti yatokanayo na seli za kansa.
Dr. Charles B. Simone, mshirika wa awali katika elimu ya kinga za maradhi (immunology) na taaluma za madawa (pharmacology) Taasisi ya Taifa ya Kanza (ya marekani), amewahi kusema: “uchunguzi wa kansa ya matiti kwa kutumia miale huongeza hatari ya kupatwa na kansa ya matiti na kuongeza hatari ya kusambaza au kueneza sehemu zingine hiyo iliyopo inayoendelea kukua.”
Uchunguzi wa kansa ya matiti kwa eksirei hubeba kiasi chanya cha uongo wa mpaka asilimia 6.
Dr. Shahla Masood, mkuu wa patholojia (sayansi ya magonjwa) katika chuo kikuu cha madawa cha Florida Marekani katika Jacksonville, amewahi kuliambia Gazeti la The New York Times: ‘’kuna tafiti zinaonyesha kuwa madhara ya kuchunguza vivimbe kwa mammograms huja kuwa chini ya upande wa pili wa sarafu’’
Uchunguzi au matibabu ya kanza ya matiti kwa kutumia miale (Mammograms) hakutakufanya usipatwe na kansa ya matiti, na tafiti mpya kabisa za mwisho zinaonesha mammograms husaidia kidogo sana nafasi ya wewe kuendelea kuishi. Njia zenye ufanisi za kuskrini kansa ni mhimu ziwepo, lakini kuskrini kansa kwa miale ya eksirei (mammography) SI jibu.
Nini kingine unaweza kufanya
Zipo njia zingine za kuchunguza kanza ya matiti ambazo haziwezi kusababisha kanza. Moja ya njia hizo ni tibajoto ya matiti (breast thermograph).
Tibajoto ya matiti hutumia teknolojia ya kamera ya miale isiyoonekana (infrared technology) ambayo hugunduwa mabadiliko katika tishu za matiti kupitia mkondo wa joto. Kompyuta huibadilisha mikondo hiyo katika rangi mbalimbali na katika rangi nyeupe na nyeusi (black and white). Daktari sasa ataweza kuona ikiwa kuna tofauti yoyote katika ulinganifu wa joto kutoka sehemu moja ya mwili na nyingine na tofauti yoyote katika mkondo wa mishipa ya damu. Ni njia salama kwa asilimia 100, haitumii miale na haileti maumivu bila madhara. Inaweza kutumika kwa watu wa umri wowote.
Tafadhari jifunze umhimu wa madini joto (iodine). Wanawake wengi nchini Japani hawapati kansa za matiti kwa sababu ya matumizi yao makubwa ya madinijoto, madini joto yanapatikana kwa wingi katika vyakula vya baharini.
Maji, mazoezi na lishe sahihi (kula kwa afya) ni mhimu kwa kina mama wa siku hizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni