Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 31 Desemba 2016

SORRY MADAM SEHEMU YA 1$2

SORRY MADAM -Sehemu ya 1 & 2 (Destination of my enemies)
Kamgisha/ 1 week ago

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Televishen pamoja na Tv zote nchini Tanzania, zipo hewani, kuweza kuyanyakua mazungumzo ya moja kwa moja ya Raisi Praygod Makuya, kwenye uteuzi wa mawaziri wapya, hii ni kutokana na waziri mkuu kuweza kujiudhulu, kwa kusumbuliwa na matatizo ya kiafya yaliyo mchukua kipindi kirefu kukaa nje ya ofisi pasipo uwepo wake. Kama kanuni na taratibu za nchi ya Tanzania, inamlazimu raisi kuweza kufanya hivyo punde tu waziri mkuu anapokuwa ameachia kiti hicho kinacho tamaniwa na kila kiongozi aliyopo serikalini.
 
Raisi akaanza kutaja majina ya mawaziri wapya watakao chukua nafasi za mawaziri walio punguzwa kwenye wizara mbalimbali. Masikio ya wananchi wengi wa Tanzania, ni kwenye wizara ya ulinzi, ambayo katika siku za hivi karibuni imetokea kuyumba, hadi wananchi kuanza kupoteza imani na serikali yao pamoja na jeshi zima la polisi. Majina kadhalika ya mawaziri wapya na wazamani walio badilishwa wizara ya kaendelea kutajwa, ikafikia kwenye wizara ya ulinzi ulinzi, hapa raisi akanyamaza kidogo na kumeza fumba la mate huku akizikodolea kamera zilizopo mita chache kutoka katika sehemu aliyo simama.
 
“Katika wizara ya ulinzi, nimeweza kufanya mabadiliko makubwa sana, ambayo ninaamini yatakwenda kufurahiwa na wananchi walio wengi. Kwa maana katika kipindi changu cha utawala nimeweza kupokea malalamiko mengi sana kuhusiana na uhalifu katika jamii inayo tuzunguka.”
“Wizara hii nimeweza kuweka watu hodari, wanao weza kuhakikisha wanafuta hofu yote iliyo jengeka katika mioyo mingi ya wananchi”
 
“Basi hapa waziri wa wizara hii, anaitwa Eddy Godwin, makamu wake atakuwa Bernad Ngoswe”
Wananchi wengi wakabaki wakiwa wameshangazwa na jina hilo kwani, hawajawahi kulisikia kwenye serikali tangu raisi Praygod kuingia madarakani.
“Hivi huyo Eddy Godwin ni nani?”
Mchaga mmoja alisikika akiwauliza wezake walio kusanyika katika duka lake la kuuza tv, redio na vitu vingine vya majumbani, lililopo maeneo ya Kariakoo.
“Hata mimi simfahamu”
“Hawa watakuwa wanagawiana, kwanini wasimpe yule….yule nani….”
“Chande?”
“Hapana yule, ambaye wamekwenda kumtupia kwenye kilimo”
 
“Ahaaaa Masele”
“Ehee huyo huyo, yule jamaa anaonekana yupo fiti sana”
“Yaani wee acha. Ila baadaye si wanaapishwa, tutakuja kumcheki huyo jamaa mwenyewe”
“Etieee”
“Naye asije akatuletea ufala kama huyu mwenzie aliye pita Haki ya Mungu, naye tutamuombea mabaya”
“Hahaaa maswawe punguza munkari bwana”
“Sio munkarti chalii yangu, yaani waziri akiwa ovyo hata hawa watendaji wake huku chini wote wanakuwa mambumbu,  hembu nenda pale sentral kaseme unatatizo uone kama hawata taka rushwa”

Nazungumzo ya watu mbalimbali katika mitaa tofauti ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam, yalikuwa ni kuhusiana na huyo waziri mpya waliye msikia jina lake likitajwa. Wengi wao hawakuonyesha imani yoyote kwa waziri huyo, wanaamini naye atafanya madudu kama aliyo yafanya waziri aliye pita, kwa kuweza kuwapa polisi, uhuru ulio ptiliza, hadi inafikia hatua kwamba wananchi wa maisha ya chini wananyimwa haki zao za msingi, na wenye pesa ndio waliweza kupata haki zao na kuwakandamiza wale wasio kuwa nacho.
                                                                                            ***
“Mume wangu utaweza, au ndio majukumu mazito uliyo kabidhiwa?”
Phidaya alimuulimuuliza mumewe, huku akimfunga tai vizuri kwenda kwenye sherehe ya wao kuapishwa inayo fanyikia kwenye viwanja vya ikulu muda wa jioni ya siku hii,waliyo tangazwa kama mawaziri wapya.
 
“Mungu ni mwema nitaweza tu”
“Eddy mume wangu usije ukaenda ukaboronga huko ikawa ni mamatizo, mengine. Napenda tuishi kwa amani”
“Baby wewe ndio mtu wa kunipa mimi moyo, ila si mtu wa kunikatisha tamaa”
“Sio kama nakukatisha tamaa mume wangu, kumbuka kwamba tumepitia shida nyingi sana, hadi leo tumepata hii amani, ninaona kwamba tutaipoteza amani hii”
“Never, nitahakikisha amani ya familia yangu kwanza, haiyumbi kisha nitahakikisha imani ya wananchi wangu, pia inapatikana”
“Sawa mume wangu mimi ninakuombea kila laheri, ila usisahau kwamba ninakupenda sana Eddy wangu, kupota maelezo”
“Nakupenda pia mke wangu”
Taratibu Phidaya akambusu mume wake mdomoni, akamuweka vizuri koti la suti aliyo ivaa. Wakatoka nje ya chumba chao na kuanza kushusha ngazi za gorofani hadi wakafika sebleni, walipo wakuta Shamsa na Junio wakitazama tv.
 
“Badilisheni chaneli muda si mrefu mutaniona nikiwa nimetokelezea kwenye kideo, nitaringaje”
Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka na kuwafanya watoto wake wote kucheka.
“Mungu wangu…!! Hapa hawajapata waziri”
Phidaya alizungumza huku akicheka kicheko, kilicho mfanya hadi machozi ya furaha kumwagika.
“Weee, waziri wameupata, yaani varangati nitakalo kwenda kulianzisha ni kama shehe aliye lishwa nguruwe pasipo kujua, sasa akagundua, hiyo movie yake nitawaadisia nikirudi”
“Hembu nenda huko muda ujue unakwenda, ngoja uvuliwe huo uwaziri wako uone kama utazunguka zunguka tena”
“Nani anivue, subutuu nitampiga ngumii moja tuu, hadi aimbe haleluya”
 
“Dady usisahaku kuniletea zawadi?”
“Mwanangu, huko ikulu kuna zawadi gani”
“Eddy nenda bwana unachelewa, weee jizungushe zungushe kama tiara”
Eddy akambusu mke wake, akafungua mlango na kutoka nje na kumkuta dereva wa gari la serikali akiwa anamsubiria kwa ajili ya kumpeleka ikulu kwenye sherehe hiyo.
“Shikamoo muheshimiwa?”
Eddy hakuitikia salamu hiyo zaidi ya kuingia ndani ya gari na dereva huyo naye akaingia ndani ya gari, akawasha gari taratibu wakatoka kwenye geti kubwa la jumbu hili la Eddy alilo linunua siku chache baada ya kutoka katika mapumziko ya harusi yao yeye na mke wake Phidaya.
 
“Samahani ndugu yangu”
“Bila samahani muheshimiwa?”
“Wewe una miaka mingapi?”
“Arobaini na tano”
“Sasa mbona umenisalimia, wakati mimi bado kijana mdogo hata miaka thelethini bado sijainusa”
“Ahaa ujajua shida hizi mdogo wangu, ndio zinazo pelekea haya yote kutokea”
“Ahaaa basi, kuanzi leo nitakuwa ninakusalimia mimi, hata kama mim ni bosi wako. Naanza kwa kusema Shikamooo bwana nani…….”
“Selema Mbogo”
“Ahaa itikia basi salamu yangu, au hutaki”
“Marahabaa. Unajua pale nilivyo ona hujaitikia salamu yangu nikahisi kwamba ni mtu ambaye hupendi mazoea na mtu, kumbe ni mcheshi kiasi hichi”
“Kaka Mbogo, yaani mimi ni mcheshi sana, huwa sipendi kumkera mtu, hata kama nina kitu chochote kwenye maisha yangu”

Mazungumzo yao yaliendelea hadi wakafika ikulu, wakaruhusiwa kupita na kuingia, dereva akasimamisha gari kwenye maegesho yaliyopo hapo ikulu. Eddy akashuka na kupokelewa na wadada walio wekwa kwa kazi hiyo ya kuwapokea wageni wanao wasili kwenye viwanja hivyo, na moja kwa moja akapelekwa hadi kwenye viti maalumu walivyo andaliwa mawaziri wanao apishwa kwenye sherehe hizo. 

Karibia vyombo vyote vya habari nchini Tanzania, wakawa wameweka kambi ikulu, ili kuweza kurusha matangazo hayo yanayo ruka moja kwa moja kutokea ikulu.
Karibia viongozi waliopo ndani ya serikali macho yao mara kadhaa wakawa wanayatupia kwa Eddy, ambaye anaonekana ni kijana mdogo kupita viongozi wengine wote waliopo katika viwanja hivi
 
“Huyu si yule kijana wa waziri mkuu?”
Mzee mmoja alimuuliza mwenzake huku wakiwa wememkodolea mimacho Eddy
“Ndio huyu”
“Si alikufa, au emefufuka?”
“Mimi wala sijui mwenzangu, ila mama yake  si yupo tutamuuliza kimetokea nini”
“Ila huyu kijana wala sidhani kama anastahili kuwa kiongozi kwenye wizara ya ulinzi”
“Watakuwa wamepeana peana tu”
Maneno yote waliyo kuwa wanazungumza wazee haya Eddy aliyasikia vizuri, ikabidi awageukie na kuwatazama, nao wakajikausha na kujifacha kama si wao walio kuwa wakizungumza maneno kama hayo, mbaya zadi ni miongoni mwa mawaziri walio pigwa chini kwenye wizara walizo kuwa waklizitumikia kiuvivu uvivu. Eddy akatabasama na kuwakonyeza kisha akageukia mbele.
 
“Huyu mtoto mpumbavu kweli, anaonekana ana dharau sana”
“Anatukonyeza sisi, tumekuwa mademu zake”
“Ngoja tutamuonyesha, anadhani hii serikali ni rahisi kama anavyo fikiria na akili zake za asubuhi”
Eddy alibaki kucheka, kwani maneno wanayo yazungumza wazee hao yanaonekana ni maneno ya wakosaji kwani walipewa nafasi na wakashindwa kuzitumia katika muda muafaka.
 
Haikuchukua muda, raisi akaanza kazi ya kuwapisha mawaziri wake wapya ambao aliwateua majira ya asubuhi na kuwatangazia taifa kwa kupitia vyombo vya habari. Ikafikia zamu ya jina la Eddy kuitwa, Akanyanyuka na kujiweka vizuri, kwa mwendo wa kujiaminai akatembea hadi akafika mbele, alipo simaa raisi pamoja na majaji. Akakabidhiwa biblia kama misingi ya viapo vinavyo tumiwa kwenye kipindi hichi cha kuapishwa na kama ni dini ya uislam, wanatuma msaafu na kama huna dini basi unanyoosha mkono wako bila kushika chochote.
 
“Mimi Eddy Godwin, ninaapa kwamba nitaitumikia katiba ya nchi hii, kwa kuilinda na kuitunza. Ehee Mungu nisaidie”
Watu wakapiga makofi, hadi raisi mwenye akaonekana kupiga makofi kuashiria kumkubali kijana huyu mdogo aliye mkabidhi majukumu yaliyo washinda wazee walio dumu kwenye serikali kwa miaka mingi sana. Eddy akapeana mikono na muheshimiwa raisi pamoja na majaji walio kuwepo katika eneo la hapo mbele kisha akarudi kuketi kwenye kiti chake.
                                                                                               ***
Msunyo mkali ukasikika ukitokea kwenye kundi la watu walio jikusanya kwenye mgahaw huu maarufu ulipo katika jiji la Nairobi, hadi watu walio kuwemo ndani ya mgahawa huu wakageuza shingo zao kumtazama mtu huyo aliye achia msunyo mmoja mkali. 

Wengi wao hawakushangaa sana kuona sura ya mtu huyo anaye onekana ni wamakamo kiasi, wanaamini watu wakisha fikisha umri kama huo mara nyingi huwa na matatizo ya akili, na wanafanyaga mambo ambayo mara nyingi yanapaswa kuweza kufanywa na watoto wadogo. Kila mmoja akaendelea na shuhuli yiliyo mpeleka hapo, huku baadhi yao wakiyapeleka macho yao kwenye tv. Inayo onyesha majirani zao nchi ya Tanzania wakiwaapisha mawaziri wao.
 
“Eddy nilazima nikuue kwa mikono yangu mwenyewe, hata kama umepewa uwaziri ni lazima nikuue tuu”
Mzee Godwin alizungumza huku akiachia msunyo mwengine ulio wafanya watu wote kumgeukia na kumshangaa, baadhi yao wakaanza kuzungumza maneno ya chini chini, wakimuhusisha na imani za kishirikina.

SORRY MADAM(2)  (Destination of my enemies)

Mzee Godwin akanyanyuka na kuacha noti ya shilingi elfu moja ya Kikenya na kuiweka kwenye meza kwa ajili ya chakula alicho kipata, moja kwa moja akelekea kwenye hoteli aliyo fikizia. Akaingia chumbani kwake na kujirusha kitandani huku hasira kali ikiwa imemtawala sana. Akanyanyuka kitandani, akatoa simu yake mfukoni na kupiga namba aliyo iandika kwa jina la ‘My M’. Simu ikaita baada ya muda ikapokelewa upande wa pili.
 
“Upo wapi?”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti nzito, iliyo endelea kujazwa uzito kwa hasira kali iliyo tawala moyoni mwake.
“Jamani baby hata salamu?”
“Nasamu sio muhimu sana, nijibu swali langu”
“Bado nipo Somalia”
“Ninakuhitaji kesho mchana uwe umesha fika hapa Nairobi?”
“Jamani Godwin kuna nini, mbona hahe hahe hivi, unadhani nitamuagaje huyu mume wangu”
“Mery nimekuambia kesho ninakuhitaji hapa Nairobi ukifika nipigie nikuambie nipo wapi unifwate sawa”
 
“Sawa mpenzi wangu”
“Ole wako kesho ipite pasipo kuzileta hizo pua zako nitakufanya kile ambacho hujawahi kufanyiwa”
“Godwin hayo nayo yametokea wapi, si nimekuambia kwamba nitakuja”
“Fanya hivyo”
Mzee Godwin akakata simu na kuitupia kitandani, akaanza kuzunguka zunguka ndani ya chumba hichi, huku kila alilo kuwa akilifikiria kichwani mwake akaona halipangiki, akapiga simu kwa muhudumu aweze kuletewa mzinga wa pombe kali aina ya whisky inayo itwa ‘Brandy’yenye kiwango cha alcohol(kilevi) asilimia stini(60%). Muhudumu aliye pokea oda hiyo akafanya kama alivyo agizwa na kuupekeka mzinga mpya kabisa pamoja na glasi. Akamkabidhi mzee Godwin, aliye fungua mlango na kumzuia muhudumu huyuo kuingia ndani ya chumba chake. Akatoa noti mbili za shilingi elfu kumi za Kikenya na kumkabidhi muhudumu.
 
“Chenchi chukua”
Mzee Godwin akafunga mlango baaya ya muhudu huyo kupokea pesa hiyo aliyo pewa kwani ni mara mbili ya bei ya mzinga huo, hata mshahara wake si wa kiwango hicho. Akaondoka kwa haraka, kuhofia mzee Godwin kufungua mlango wa chumba chake akahairisha kwa yeye kuchukua chechi iliyo bakia.
Mzee Gowdwin akaanza kufakamia mafumba ya pombe hiyo, iliyo tengenezwa katika mfumo wa Spirit, ambayo ni kali sana pele unapo idumbukiza mdomoni mwako, hususani kwa mtu ambaye hajawahi kuitumia pombe hiyo.
 
***
    Baada ya sherehe kumalizika, Eddy akamfwata mama yake aliye kuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wapya serikalini.
“Jamani huyu ni kijana wangu, ninaamini kwamba mumesha mfahamu”
“Tumemfahamu muheshimiwa”
“Jamani ninawaomba mumuunge mkono na mumuonyeshe njia kama vile mulivyo nipa mimi ushirikiano”
“Sawa muheshimiwa, tutahakikisha kijana anayooka”
Eddy akaendelea kutambulishwa kwa viongozi walio kuwa wakifanya kazi na mama yake katika kipindi chote alipo kuwa madarakani kama waziri mkuu. Ikawa ni moja ya hatua ambayo Eddy hakuitegemea sana kwenye maisha yake, na wala hakuwazia kama ipo siku atakuja kuwa kiongozi serikali.
 
“Eddy mwanangu”
“Naam mama”
“Nafasi ni hii, nakuomba nakuomba mwangu. Ufanya kazi vizuri, usije ukanidhalilisha hapo baadaye.”
“Siwezi kufanya hivyo mama yangu”
“Mimi nakuombea kwa maana ninafasi ya kipekee uliyo pata kuwa waziri pasipo kupitia ubunge”
“Sawa mama, nitajitahidi ninafanya kazi vizuri pale nitakapo kuwa ninahitaji msaada wako mama nitakujulisha”
Eddy alizungumza na mama yake wakiwa wamesimama kwenye moja ya bustani, iliyopo eneo la ikulu
“Vipi lakini kija Junio hawajambo?”
“Hawajambo wanaendelea vizuri”
“Kesho, nitatuma dereva aje kumchukua. Alafu anaanza lini shule?”
 
“Nataka nimpeleke bording school”
“Kwa nini?”
“Akakae huko”
“Sitaki mtoto aende bording akiwa bado mdogo, subiri asome afike lasaba ndio umpeleke bording”
“Nimekuelewa mama”
“Sawa naona wezako wanajipanga kwa kupiga picha ya pamoja na raisi, Nenda na wewe ukajumuike nao”
“Powa mama”
“Weee hiyo lugha za powa, naomba uziache ukisikiwa na hao mapaparazi utaonekana muhuni”
Eddy akaondoka huku akicheka, akajumuika na mawaziri wezake katika kupiga picha hivyo ya pamoja wakiwa na riasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani bwana Praygod Makuya.
                                                                                           ***
    Vyombo vingi vya habvari asubuhi iliyo fwata, stori kubwa ikawa ni kwa huyu waziri wa Ulinzi bwana Eddy Godwin, wengi wao waliingiwa na mashaka wakidai kwamba bwana Eddy alisha fariki miezi kadhaa ya nyuma, ila wengine walidai ni miongoni mwa wanasiasa wapya kuwahi kujitokeza kwenye serikali ya Tanzania pasipo kujinadi kwa wananchi.
 
Kila aliye kuwa akiitazama picha ya Eddy kwenye gazeti hakukosa cha kuzungumza huku wengine wakidai kwamba hato wajibika kama wanavyo hitaji wao awajibike. Wengine wakidai kwamba bwana Eddy Godwin amependelewa kutokana mama yake alikuwa ni waziri mkuu.
“Yaani hii nchi, imejaa ukiritimba sana”
Mwanafunzi mmoja wa chuo cha Mlimani alizungumza huku akipitia macho yake kwenye gazeti la G NEWS
”Kwa nini?”
Mwenzake aliye kaa naye kwenye kochi moja lililo tengenezwa na saruji, kwa ajili ya kujisomea alimuuliza mwenzake.
“Huyu waziri wa ulinzi kumbe mama yake alikuwa ni huyu mama waziri mkuu aliye jiudhuru”
 
“Ahaaa!!”
“Wewe shangaa tu, utasoma hapo hadi makalio yaote sugu, ila kuna watu kiulaini wanajichukulia vyeo serikalini”
“Daaaaa yaani hii nchi mbona inapelekwa kizembe hivi, hivi kwa nchi za wezetu ni lazima mtu awe na vigezo vya kielimu ndio awe waziri tena waulinzi. Sasa huyu mimi sijui hata kama ana cheti cha form six”
Wote wakacheke huku wakiendelea kutazama picha kadhaa, zikimuonyesha Eddy akiwa na mawaziri wezake pamoja na muheshimiwa Raisi. Mijadala ya kumjadili Eddy Godwin, ilizidi kusambaa kila kona ya nchi ya Tanzania huku wengine wakijipa matyumaini ya kumpa muda waziri huyu, huku wengine wakiukosoa uamuzi wa raisi kumteua mtu asiye fikia hata robo ya sifa ya kuwa waziri tena wa ulinzi.
 
    ***
    Haikuwa siku ngumu kwa Waziri Eddy Godwin, jambo la kwanza baada ya kukabidhiwa ofisi yake, akafunga mlango wa ofisini kwake na kubaki peke yake, taratibu akapiga magoti chini na kuanza kusali
“Ehee Mungu, ninatambua una makusudi na mimi ya kuniweka kwenye hii ofisi, yenye sifa ya kuwashinda wengi na kupelekea malalamiko ya wananchi kwamba wanateseka. Ninakuomba uniopngoze na kunilinda, hadi mwisho wa kazi hii. AMEN”
 
Eddy akasimama, na kufungua mlango wake, kumruhusu sekretari wake kuingia.
“Muheshimiwa nimekuja kama ulivyo nihitaji”
“Ohhhh ulisema jina nani vile?”
“Stella”
“Stella nani?”
“Stella Msulwa”
“Ahaaa sasa fanya hivi, ninakuomba uwatumie Fax, wakuu wote wa polisi nchi nzima. Kesho waambie nina kikao muhimu nao”
“Sawa muheshimiwa, je utahitaji kahawa?”
“Hapana nipo vizuri”
“Asante mkuu”
Stella akatoka ofisini mwa Eddy na kurudi katika sehemu yake ya uwajibikaji wa kazi. Eddy akaanza kukagua faili moja baada ya jengine, huku akipitia baadhi ya madai yanayo toka kwenye jeshi la polisi wakiomba kuweza kulipwa madeni yao yanayo endelea kulimbikizwa na serikali pasipo sababu ya msingi.
 
“Bilioni thelethini, mmmmmm…….!!”
Eddy alishangaa deni hilo wanalo daiwa serikali na jeshi la polisi. Akachukua mafaili mengine kutazama mambo mengine yanayo husiana na wizara yake. Simu yake ya mezani ikaita, akaichukua taratibu na kuiweka sikioni mwake.
“Bosi kuna wageni wawili wamefika hapa wanahitaji kuonana na wewe”
“Ni wanawake au wanaume?”
“Mmoja ni mwana mama na mwengine ni mwanaume”
“Wamesema wametoka wapi?”
“Mwanaume ni kwenye moja ya kanisa, na mwanamke kwenye taasisi ya kusaidia watoto yatima”
“Po….ahaa, sawa waruhusu”
Eddy akairudisha simu yake kwenye sehemu alipo itoa, sekunde kadhaa mlango wa ofisisini mwake ukafunguliwa na wakaingia wageni wake walio kuwa wakimuhitaji. Mwanaume akawa amebeba brufcase nyeusi na mwana mama akiwa amebeba pochi kubwa, ambalo ni wamama wengi wa mjini ndio mikoba yao ya kisasa.
“Karibuni mukae wazee wangu”
“Asante muheshimiwa”
 
“Kwanza shikamoni, pili niwasaidie nini?”
Eddy alizungumza huku akiwatazama kwa umakini, kwa mbali akiachinia tabasamu dogo ili kuufuta umakini wake juu ya uso wake, ili wageni wake wasigundue hilo.
“Mimi ninaitwa mchungaji Mandingo, nimetokea kwenye kanisa la G.W.C”
“Mimi ni Madam Glory, ni mmiliki wa kituo cha kulele yatima kule Arusha kinaitwa M.C.C”
“Ahaaa nashukuru kuwafahamu, sasa twende kwenye mada husika iliyo waleta humu ofisini”
“Muheshimiwa sisi tulikuja kukupa kapongezi kadogo tu, kwa maana ni vijana wachache sana ambao wanapata nafasi ndogo kama hii”
Madam Grory alizungumza kwa kujichekesha chekesha
“Kamaa alivyo tangulia kusema mwenzangu, tumeona tuje leo ofisini mwako tukupe japo vijisenti kidogo kama pongezi”
Mchungaji Mandingo, akafungua brufcase yake na kuiweka juu ya meza, akaifungua, macho ya Eddy yakatua kwenye vibunda vipatavyo kumi na tano vya shilingi elfu kumi kumi, kisha macho yake akayahamishia kwa mchungaji Mandingo na Madam Glory.
 
“Ni shilingi hizi?”
“Ahaa muheshimiwa hizo ni vijisenti tu, vichache tu”
“Hujanijibu swali langu, ni shilingi ngapi?”
“Milioni hamsini tu”
“Ahaaa, sawa nashukuru kwa hilo, ila ngona niende hapo nje ya ofisi yangu mara moja kuna kitu nikachukue”
“Sawa mheshimiwa”
Eddy akasimama kwenye kiti chake na kujiweka vizuri shati lake jeupe alilo livaa, akapiga hatua hadi mlangoni mwake, akashika kitasa na kuufungua mlango. Akapiga hatua hadi walipo askari wanao linda ofini mwake. Akawanong’oneza kisha akarudi ofisini mwake na kuwakuta mchungaji Mandingo na Madam Mery wakiwa wanajichekesha chekesha, huku brufcase ikiwa bado wazi na vibunda vyake vikiwa kama alivyo viacha.
 
”Samahani jamani kwa kuchelewa”
“Usijali mtoto wetu, ila kuna makubaliano kidogo tungeomba utusaidie muheshimiwa”
“Makubaliano gani?”
“Sisi japo tunadili na jamii, ila kuna vijibiasahara vidogo vidogo tunavifanya. Tungeomba ulinzi wako muheshimiwa”
“Ahaaa ni biashara gani wazee wangu, ina bidi tuwekane wazi hata siku likitokea la kutokea tunalindana”
Mchungaji Mandingo na Madam Grory wakatabasamu, huku wakitazamana. Eddy naye akafwatisha tabasamu lao, taratibu Madam Grory akajivuta mbele kidogo na kumsogelea Eddy 
 
“Madawa ya kulevya na viungo vya albino”
Madam Grolry akajirudisha taratibu huku akiwa na tabasamu lake lile lile alilo kuwa ameloweka hapo awali, Mchungaji Mandingo naye akalisindikiza tabasamu lake kwa kutingisha kichwa akishiria kwamba, msaada wao ndio huo. Eddy hakuonekana kustuka sana, alicho kifanya ni kujikooholesha kidogo kama mtu anaye hitaji kulisafisha koo lake ili aendelee na mazungumzo hayo ambayo ni nyeti sana kwa Madam Grory pamoja na Mchungaji Mandingo.
Kundi la askari wapatao wanne wakiwa na silaha zao mikononi, wakaingia ofisini mwa waziri Eddy, baada ya kusikia sauti ya kujikoholesha, ambayo Eddy aliwaashiria vijana wake kwamba atafanya hivyo, na wao wausubirie mguno huo nje ya mlango.
 
“Ahaaa wazee wangu, tutakuja kuzungumza vizuri mukiwa polisi au mahakamani, Sawa wazee wangu?”
Mchungaji Mandingo na Madam Grory wakabaki wakiwa wameshangaa, miili yao ikaanza kutetemeka, kila mmoja akaanza kupata fukuto la mwili, ambalo hajawahi kulipata tangu alivyo zaliwa, japo kuwa ndani ya ofisi hii, hewa safi ya kijiubaridi(AC), iliendelea kupenya kwenye kila mwili wa mtu aliyomo ndani ya ofisi hii, ila wao hawakuihisi kabisa juu ya ngozi zao.
“Mu…muhe…eees…himi…wa”
Mchungaji Mandingo alipata kigugumizi cha gafla, ila Eddy hakujali kubabaika kwake, alicho kifanya ni kuwaamrisha vijana wake kuweza kuwanyanyua na kuwapiga pingu wahalifu hao, huku brufcace yao, wakiwa wameibeba wao wenyewe.
 
“Niwakute kituoni, pamoja na udhibitisho wao huo”
“Sawa mkuu”
“Byeee”
Eddy akawaaga, huku akitabasamu. Waalifu wake wakatolewa nje ya ofisi yake, akabaki peke yake, akafungua vifungo viwili vya shati lake na kuilegeza tai yake, kisha taratibu akajiegemeza kwenye kiti chake.
‘Ahaa kumbe hawa ndio wanao waumiza walala hoi na kuwatesa walemavu wa ngozii’
Eddy alizungumza huku akiendelea kuzunguka zunguka kwenye kiti chake.
                                                                                        ***
    Mlio wa simu, ukamkurupusha Mzee Godwin, kutoka kwenye usingizi wake mzito, ulio sababishwa na msongamano mkubwa wa mawazo pamoja na pombe kali aliyo ifakamiaa jana usiku. Kwa macho yaliyo jaa usingizi, akalitazama jina lililo jitokeza kwenye simu yake, ila akaiona namba ngeni. Taratibu akaiipokea na kuiweka sikiono mwake.
 
“Haloo”
Alizungumza kwa sauti nzito aliyo jaa, usingizi mkubwa.
“Baby jamani mbona unanifanyia hivyo, napiga simu kwa namba yangu hupokei, hadi nimeazimisha namba ya mtu mwengine”
Sauti ya malalako ya Madam Mery ilisikikika upende wa pili wa simu.
“Nilikuwa nimelala”
“Sawa niambie upo hoteli gani?”
Mzee Godwin akamtajia Madam Mery, hoteli aliyopo. Madam Mery akaahidi kufika baada ya masaa kadhaa katika eneo hilo.
Baada ya dakika kadhaa kama alivyo kuwa ameahidi Madam Mery, akafika kwenye hoteli aliyo ambiwa na Mzee Godwin, moja kwa moja akaeelekea kwenye chumba cha mzee Godwin. Akagonga mara kadhaa na mlango ukafunguliwa na mzee Godwin.
“Karibu ndani”
“Asante”
Mzee Godwin akafunga mlango  kwa ndani, Madam Mery akapiga hatua hadi kwenye kitanda na kujitupa, hii ni kutokana na uchovu wa safari kutokea Somalia hadi Nairobi Kenya.
 
“Eheee mbona jana umenipigia simu ya hae hae vile?”
“Nina mazungumzo na wewe, hivi una habari gani kuhusiana na Eddy?”
“Kwakweli sina ni muda mrefu sijaonana naye, nahisi atakuwa amekufa”
Madam Mery alizungumza huku akihitaji kujua ni kitu gani kinacho endelea baina ya Godwin na Eddy
“Yule mshenzi amepewa uwaziri wa ulinzi Tanzania?”
“Mungu wangu………ana sifa gani za yeye kuwa waziri?”
“Ndio hivyo. Yaani laiti ningejua huyu mchenzi ningemuua tangu tukiwa ndani ya ndege ninaamini kwamba tusinge kuwa tunazungumza mazungumuzo ya kumuuhusu huyu kibwengo mtu”
“Kwa nini usimuue?”
“Mazingira hayakuruhusu, alipelekea kunipa shida ya kutafutwa hapo bendeni kwa hayati Mzee Madiba”
“Ulitokaje tokaje ndani ya ndege?”
Swali la Madam Mery likamfanya Mzee Godwin kurudisha kumbukumbu zake nyuma kwa haraka hadi siku aliyo toka kupambana na Eddy ndani ya ndege na taratibu akaanza kusimulia.
  
==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia kamgisha blogger  
Visit website

Chanzo cha saratani ya matiti

Chanzo cha saratani ya matiti
KAMGISHA BLOG / 10 hours ago

Hakuna kitu kingine kizuri kama mwili wa mwanamke kwakuwa unaweza kuleta kiumbe binadamu kingine.

Mwili wa mwanamke unazo ovari ambazo hutengeneza mayai na homoni maalumu ambazo hudhibiti mwili wake wakati wa ujauzito kuanzia wakati yai linaporutubishwa mpaka mwishoni mwa wastani wa miezi tisa (wakati wa kujifunguwa).

Mfumo huu maalumu huanza kazi mara mwanamke anapoanza mzunguko wake wa uzazi (mzunguko wa hedhi). Kwa wastani kila siku 30 ovari zake zitazarisha yai na kuliweka katika mfumo wake wa uzazi likisubiri kurutubishwa.

Wakati yai hili limetolewa, mwili wake utaanza kujiandaa kwa uwezekano wa kupata mtoto.
Mfuko wa uzazi (uterus) utaanza kubadili uundwaji wake wa seli kwa kuandaa uwezekano wa kukishikilia kijusi (fetus) baada ya yai kurutubishwa. Wakati yai litakapokuwa limerutubishwa ovari zake (mwanamke) zitachukuwa majukumu ya mwili wake na kuhakikisha kuwa kijusi kinapata kile kinachokihitaji ili kuishi.

Ubongo wa mwanamke pia huathiriwa kutokana na kutolewa kwa homoni hizi maalumu wakati wa ujauzito. Hii ndiyo sababu wanawake hupata mabadiliko ya kihisia (moody) na huwa walioamka zaidi kuliko wanaume wakati wa ujauzito. Wakati mwingine bila hata sababu wanawake wote wanaweza kuonekana kama wenye huzuni, hulia, hupiga mayowe na lisaa limoja baadaye kuwa wakicheka, wakitabasamu na kuwa tayari kusonga mbele.

Hali yake pia katika tendo la ndoa huweza kubadilika sababu ya kutolewa kwa homoni hizi. Wanawake wapo katika mfadhaiko zaidi kuliko wanaume kwa sababu siku hizi wanawaku siyo tu husimamia watoto, bali pia wanalisha familia zao na kuwaangalia waume zao. Wanawake huhofia zaidi afya za familia zao na masuala ya fedha. Siku hizi Wanawake pia ni waajiriwa kamili (full time employees).

Mfadhaiko (stress) unaweza kumgharimu mwanamke yeyote siku hizi sababu ya kukosa muda wa ziada: nenda tu, nenda, fanya kazi, kazi kazi, hakuna muda, hakuna muda. Mwili wa mwanamke unaweza kuzitoa homoni zitakazomuwezesha kuendelea kwa kukopa kile inachohitaji toka sehemu nyingine ya mwili kuiwezesha sehemu nyingine mhimu zaidi kuendelea kufanya kazi zake kawaida. Hii ndiyo sababu wanawake huishi zaidi ya wanaume.

Katika safari hii ya kukopa ikiwa sehemu iliyokopwa haikurudishiwa vitu vyake kwa muda muafaka mwili wake (mwanamke) huanza kufeli na sasa ataanza kupata baadhi ya aina ya matatizo (kuugua).

Mfadhaiko wa kwanza mwili wa mwanamke unapaswa kushughurika nao ni mzunguko wake wa uzazi (reproductive cycle). Miili yao huitoa homoni iitwayo prolaktini (prolactin) kuuwezesha mwili kuhimili mabadiliko hayo.

Mwili wa mwanamke pia utaitoa homoni punguza maumivu (pain killer) iitwayo ‘endorphins’. Mwanamke anaweza kuhimili zaidi maumivu kuliko awezavyo mwanaume sababu ya endorphins nyingi alizonazo sababu ya kupewa jukumu la kujifunguwa mtoto.

Wakati mzunguko wa uzazi umeanza homoni huzarishwa toka katika ubongo (hypothalamus) ikiyaambia matiti kujiandaa kwa ajili ya kutengeneza maziwa kwa ajili ya mtoto mtarajiwa. Kwahiyo tishu za matiti lazima zibadilike na hivyo kusababisha uwezekano wa kutokea kwa homa, kuvimba na kujisikia kuongezeka uzito wa matiti..

Wakati seli za mafuta za matiti zinaanza kubadilika, huhitaji mzunguko zaidi wa damu unaozipelekea vitamini mhimu, madini, asidi amino na maji yenye elektrolaiti. Kwahivyo matiti yatakuwa na uwezo wa kusaidia mahitaji yote ya mtoto katika kutengeneza maziwa. Maziwa ya matiti ya mama yatamruhusu mtoto kukuwa na kubaki katika afya kwa mwanzoni mwa miezi ya kwanza ya uhai wake mpaka hapo atakapoweza kuanza kula vyakula vigumu.

Kansa ya matiti inaweza kuanza wakati tishu hii au mzunguko umechanganywa kama matokeo ya kupewa ishara zinazogongana, tishu inaanza kuandaa seli za mafuta kwa ajili ya maziwa kutengenezwa na wakati huo huo inaamriwa kusimama, kuanza upya au kuanzia pale iliposimamia wakati mwingine uliopita.

Ishara hizi (homoni) mbaya zinazogongana zinaweza kusababishwa na:

Kutumia vidonge vya kuzuia ujauzito kwa miaka mingi.
Kunywa alikoholi (pombe) kupita kiasi
Kunywa kahawa au vinywaji vyenye kafeina kupita kiasi
Kutumia viongeza utamu vya kutengenezwa (artificial sweeteners).
Ikiwa tezi ya pituiatari au ‘hypothalamus’ katika ubongo inakosa lishe kamili, inaweza kutoa homoni isiyotakiwa au kutoa homoni wakati ambao haikutakiwa na hivyo kuzipelekea seli za matiti kufeli na hivyo kuleta seli zisizo za kawaida za matiti kutengenezwa (kansa)..

Katika baadhi ya wanawake, kitendo cha kula vyakula ambavyo vina homoni ndani yake vinaweza kutuma ishara (ujumbe) kuharibu jozi ya maagizo yaliyokwisha tolewa tayari na hivyo kupelekea kutokea kwa vivimbe au hata kuzarishwa kwa seli zisizo za kawaida ziwezavyo kugeuka kuwa kansa ya matiti.

Baadhi ya madawa ya hospitalini yana madhara hasi yawezayo kuvuruga ishara (homoni). Ikiwa damu ya mwanamke inakosa vitamini au madini mhimu, basi baadhi ya seli hizo za mafuta hazitaweza kubadilika kabisa kuwa seli zinazoweza kutengeneza maziwa, hupumuzishwa na zingine mpya kutengenezwa kuchukuwa nafasi. .

Ikiwa kinga ya mwili iko bize sana (kuondoa) kula seli mbovu, basi inaweza kuweka uzio (fence) kuzunguka seli hizo mbovu mpaka itakapozila kwa mara ya pili (recycle and eat up the bad cells). Seli hizo mbovu zilizozungushiwa uzio ndizo tunazoziita vivimbe katika matiti na katika hali nyingi baada ya miaka kadhaa vitapotea kadiri kinga ya mwili inavyorudi na kuvirudia kuvila tena.

Ikiwa seli hizi za mafuta zimekuwa mbaya sababu ya kuwa na asidi iliyozidi sababu ya kukosa maji na kupokea ishara zinazogongana nyingi na asidi hii inakula katika fungu la maagizo (blue print) katika DNA, itabadilisha maagizo (code) na hivyo utapata kutengenezewa seli mafuta za matiti zisizo za kawaida (kansa) na zinaweza kukuwa na kusambaa mwili mzima.

Vifundo limfu nyuma ya mikono vitaziteka seli hizi zisizo za kawaida mpaka limfu itakaposhindwa kuzishikilia zaidi na kisha sasa zinaweza kutembea kwa uhuru wote kwenda sehemu nyingine ya mwili.

Wanyama wengi tuwalao siku hizi (kuku,ng’ombe n.k) wanalishwa homoni kurekebishwa kijenetiki ili kuharakisha kukuwa kwao na kuongezeka uzito kwa haraka. Homoni hizi na mabadiliko yao kijenetiki vimo katika nyama na vinapoliwa vinaweza kuathiri tishu za matiti au ogani za uzazi kwa baadhi ya wanawake.

Moja kati ya madhara makubwa ya kula kiasi kingi cha mafuta ya mboga mboga (polyunsaturates) ni kuhusika kwake na kansa. Katika tafiti toka kliniki ya Mayo, iligundulika kuwa watu wanaosumbuliwa na kansa ya matiti walikuwa pia na ongezeko la mafuta yatokanayo na mboga mboga katika tishu za matiti yao kama ilivyojitokeza katika plasma ya damu zao.

Soya na baadhi ya maharage vinaweza pia kuwa na homoni zinazoweza kuathiri baadhi ya matiti ya wanawake (mfumo wa uzazi). Ninashauri kwa nguvu zote wanawake wote kusoma kitabu kilichoandikwa na Dr Carolyn De Marco kiitwacho “Take charge of your body” kinachozungumzia zaidi mambo haya na zaidi.

Ni mhimu zaidi kwa wanawake kufanya zoezi binafsi la kuchunguza matiti yao, wakiangalia kila titi kwa kufuatisha zoezi rahisi la vidole vitatu. Kwanza katika duara kisha katika wima, kukaguwa kwa ajili ya mabadiliko yeyote ya kifiziolojia, vivimbe, mkazo au mabadiliko ya rangi, ikihusisha kuvuja kwa chuchu, saizi na rangi.

Mazoezi haya rahisi yanapatikana katika intaneti na maonyesho mengine, yanaonyesha namna gani ya kufanya zoezi la kujikagua kwa kutumia video rahisi.

Ikiwa mabadiliko yeyote yatagundulika, tafuta ushauri wa kidaktari mapema kadili iwezekanavyo.

Kuna umhimu wa uchunguzi wa matiti kwa eksirei?
Uchunguzi wa matiti kwa eksirei (mammograms) mara nyingi imedhaniwa kama ‘’mwokozi wa maisha’’, namna ya kuskrini kansa inayohusika kupunguza vifo vitokanavyo na kansa kwa wastani wa asilimia 15 mpaka 25. lakini faida hizi zilizolipotiwa zinaegemea tafiti zilizopitwa na wakati zilizofanyika miongo iliyopita.

Mwezi Septemba 2010, the New England Journal of Medicine, moja kati ya majarida ya afya yanayoheshimika duniani, lilichapisha taarifa ya kwanza ya utafiti wa hivi karibuni ulioangalia ufanisi wa mammograms, na majibu yao yapo tofauti sana na yale maofisa wengi wa afya na wanafizikia wangekufanya uamini.

Hitimisho lake lilikuwa kwamba mammograms ingekuwa imepunguza vifo vitokanavyo na kansa kwa wastani wa vifo 0.4 kwa wanawake 1000—idadi ambayo ni ndogo sana ambayo inaweza kuwa hata 0. Ukiacha hilo, wanawake 2,500 watatakiwa kuwa wameskriniwa kwa zaidi ya miaka 10 kwa kifo kimoja cha kansa ya matiti inayolengwa kuepukika.

Ni jambo linalojulikana wazi kuwa uionishaji miale huongeza mabadiliko ya ki-seli ambayo hupelekea kansa—na mammograms inalenga zaidi dozi inayoenda moja kwa moja katika matiti yako, kitu kinachoongeza hatari ya kupata kanza!.

Kwanini lazima ungetaka kufanya hivi?
Mammograms huuweka mwili wako katika miale inayoweza kuwa mikubwa mara 1000 kuzidi ile ya eksirei ya kifua, ambayo tunajuwa huongeza uwezekano wa kutokea kansa. Teknolojia ya kutumia picha za miale kukaguwa vivimbe vya kansa pia huyabana matiti yako kwa nguvu na mara nyingi ikiambatana na maumivu ambayo yanaweza kupelekea kuongezeka mauti yatokanayo na seli za kansa.

Dr. Charles B. Simone, mshirika wa awali katika elimu ya kinga za maradhi (immunology) na taaluma za madawa (pharmacology) Taasisi ya Taifa ya Kanza (ya marekani), amewahi kusema: “uchunguzi wa kansa ya matiti kwa kutumia miale huongeza hatari ya kupatwa na kansa ya matiti na kuongeza hatari ya kusambaza au kueneza sehemu zingine hiyo iliyopo inayoendelea kukua.”

Uchunguzi wa kansa ya matiti kwa eksirei hubeba kiasi chanya cha uongo wa mpaka asilimia 6.

Dr. Shahla Masood, mkuu wa patholojia (sayansi ya magonjwa) katika chuo kikuu cha madawa cha Florida Marekani katika Jacksonville, amewahi kuliambia Gazeti la The New York Times: ‘’kuna tafiti zinaonyesha kuwa madhara ya kuchunguza vivimbe kwa mammograms huja kuwa chini ya upande wa pili wa sarafu’’                               

Uchunguzi au matibabu ya kanza ya matiti kwa kutumia miale (Mammograms) hakutakufanya usipatwe na kansa ya matiti, na tafiti mpya kabisa za mwisho zinaonesha mammograms husaidia kidogo sana nafasi ya wewe kuendelea kuishi. Njia zenye ufanisi za kuskrini kansa ni mhimu ziwepo, lakini kuskrini kansa kwa miale ya eksirei (mammography) SI jibu.

Nini kingine unaweza kufanya
Zipo njia zingine za kuchunguza kanza ya matiti ambazo haziwezi kusababisha kanza. Moja ya njia hizo ni tibajoto ya matiti (breast thermograph).

Tibajoto ya matiti hutumia teknolojia ya kamera ya miale isiyoonekana (infrared technology) ambayo hugunduwa mabadiliko katika tishu za matiti kupitia mkondo wa joto. Kompyuta huibadilisha mikondo hiyo katika rangi mbalimbali na katika rangi nyeupe na nyeusi (black and white). Daktari sasa ataweza kuona ikiwa kuna tofauti yoyote katika ulinganifu wa joto kutoka sehemu moja ya mwili na nyingine na tofauti yoyote katika mkondo wa mishipa ya damu. Ni njia salama kwa asilimia 100, haitumii miale na haileti maumivu bila madhara. Inaweza kutumika kwa watu wa umri wowote.

Tafadhari jifunze umhimu wa madini joto (iodine). Wanawake wengi nchini Japani hawapati kansa za matiti kwa sababu ya matumizi yao makubwa ya madinijoto, madini joto yanapatikana kwa wingi katika vyakula vya baharini.

Maji, mazoezi na lishe sahihi (kula kwa afya) ni mhimu kwa kina mama wa siku hizi.

Ijumaa, 30 Desemba 2016

Hizi ndio sehemu 10 zenye msisimko Mkali zaidi kwenye Mwili wa Mwanamke

Hizi ndio sehemu 10 zenye msisimko Mkali zaidi kwenye Mwili wa Mwanamke
KAMGISHA BLOG/ 9 minutes ago

Kila mwanaume anapenda kua fundi wa tendo la ndoa akiwa faragha na mke au mchumba wake lakini bahati mbaya sana hakuna kanuni maalumu ya kumsisimua mwanamke kwani kila mwanamke ana eneo lake ambalo likiguswa anakua taabani hivyo ni wajibu wa mwanaume kulitafuta na kuligundua eneo hilo.

Mazoea ya kufanya mambo yaleyale kila siku kwa muda mrefu hufanya tendo hilo la ndoa lianze kua baya na huenda ikawa chanzo  cha mtu kuchepuka kutafuta ladha zingine.

Kitaalamu katika sayansi ya binadamu kuna maeneo kadhaa ambayo wanawake wote wakiguswa hupata msisimko mkali lakini msisimko hutafautiana kutokana na mwanamke husika kama ifuatavyo.

1. Kichwani; juu ya kichwa cha binadamu kuna mishipa mingi ya damu na ile ya fahamu hivyo maeneo haya yakishikwa homoni kama oxytocin na serotoinin huachiwa mwilini na kuleta msisimko mkubwa.

Jinsi ya kufanya; mshike kwanzia nyuma ya sikio kisha ingiza vidole katikati ya nywele kama unamkuna kichwa bila kutumia nguvu.

2. Sikio; sikio ni sehemu yenye mishipa ya fahamu inayoenda kwenye ubongo, mara nyingi sikio watu hua wanalipuuza sana na kuzani halihusiki lakini naomba nikwambie ni moja ya sehemu inayoweza kumfanya mtu achanganyikiwe.

Jinsi ya kufanya; anza kwa kumnong'oneza kwa sauti nzito, kisha libusu sikio lake baada ya hapo unaweza kulamba sehemu ya sikio la nje na baadae kuingiza ulimi ndani ya sikio kabisa. hapa msisimko ni mkali sana na anaweza kukukwepa na kutoa sauti kali ya kimahaba.

3. Ulimi ; ulimi ni sehemu ya mwili ambayo ina mishipa mingi mara mia moja zaidi kuliko ile mishipa ya fahamu ya viganja vyetu. msisimko wa ulimi unasababishwa kumwagika kwa homoni ambazo zinatuletea furaha ya mioyo yetu.

Jinsi ya kufanya; busu tu  inatosha kusisimua ulimi wa mtu wako, bahati mbaya kuna watu hawajui kubusu. ukiwa unabusu mtu usipanue mdomo mzima kama samaki mfu... fungua mdomo wako kidogo kisha nyonya lips za juu wakati mtu wako ananyonya za chini na hii ndio busu linavotakiwa kua.

4. Shingo; hii ni sehemu ya mwili yenye ngozi laini sana ambayo inasisimka hata kwa kuipumulia tu na pua. ni moja ya sehemu nzuri sana kunyonya, kulamba na kubusu.

Jinsi ya kufanya; ukiwa umemkumbatia mtu wako basi busu upande wa kulia au wa kushoto wa shingo huku ukinyonya ngozi la eneo hilo.

5. Chuchu; wanaume wengi wanatumia sehemu hii kama sehemu kuu kumsisimua mwanamke, ni kweli kabisa tafiti zinaonyesha kwamba sehemu ya ubongo ambayo husisimuka chuchu za mwanamke zikiguswa ni sehemu hiyohiyo ambayo inasisimka kinembe na uke vikiguswa. kwa hiyo ni moja ya sehemu muhimu sana.

Jinsi ya kufanya; tomasa matiti yote ya mwanamke kwa kutumia mikono yako miwili kisha nyonya chuchu yake taratibu huku kama unaing'ata na kuiachia. badilisaha kwa kuchocha chuchu ya kulia na kushoto.

6. Kiuno au mgongo wa chini; kama umechunguza ni kwamba wanawake wengi husisimka sana wakiguswa viuno vyao ghafla hata wakati wa kukumbatiwa tu. hii ni sababu ya mishipa ya fahamu inayoenda hadi kwenye sehemu zake nyeti hupita huko.

Jinsi ya kufanya; tomasa kama unafanya masaji sehemu ya chini kabisa ya kiuno kabla makalio hayajaanza. hii itamfanya arelax sana lakini pia kuongeza damu kwenda sehemu zake nyeti tayari kwa tendo la ndoa.

7. Tumbo; tumbo ni sehemu ambayo watu wengi hawaitilii manani sana lakini misuli ya tumbo imeungana na uke moja kwa moja ndio maana baadhi ya wanawake hufika kileleni kwa kufanya mazoezi ya tumbo kitaalamu kama core exercises..

Jinsi ya kufanya; tomasa tumbo lake kwanzia juu kabisa ya tumbo na kwenda tumbo la chini na kisha busu taratibu maeneo mbalimbali ya sehemu ya tumbo na unaweza kumalizia kwa kunyonya kitovu.

8. Katikati ya mapaja; hii ni sehemu yenye msisimuko mkubwa kwenye mwili wa mwanamke, watu wanaondesha magari wanajua siri hii kwani wakimpakia mwanamke wanatumia njia hii kumsisimua kwa kuweka mkono mmoja kwenye mapaja yake.

Jinsi ya kufanya; shikashika sehemu za katikati ya mapaja kwanzia magotini kwenda mpaka karibu na uke.unaweza fanya hivyo wakati ukiwa unambusu.

9. Nyayo za miguu; nyayo za miguu zikiguswa hata kwa mtu ambaye sio wa kike zina msisimko sana kama wa kutekenywa hivi na sina msisimko mkubwa kuliko sehemu nyingi nilizotaja.

Jinsi ya kufanya; shika nyayo moja ya mguu kisha kwa kutumia viganja viwili tomasa katikati ya mguu kwanzia kwenye kisigino mpaka kwenye vidole.usitumie nguvu nyingi...

10. Kinembe [critoris]; hii ni sehemu ya mwanamke ambayo kazi yake ni kuleta msisimko tu na raha kwa mwanamke..eneo hili linazaidi ya mishipa ya fahamu 8000, ni eneo dogo sana lakini shughuli yake sio ndogo. naweza kusema ndio eneo lenye msisimko mkali kuliko yote niliyotaja hapo juu na likiguswa tu mwanamke analoana kabisa.

Jinsi ya kufanya; kidole chako kikubwa cha kinganyani bonyeza na kuachia sehemu hiyo kama mtu anayekagua parachichi pia sugua kwenda chini, juu na pembeni kuangalia muhusika anapenda wapi zaidi pia kama una uhakika na usafi au afya ya muhusika unaweza lamba lwa kuzungusha ulimi sehemu hiyo.

Mwisho; sehemu zote nilizotaja hapo juu ni muhimu sana kwa ajili ya kumuandaa mwanamke japokua kila mwanamke anapata msisimko zaidi kutokana na yeye mwenyewe alivyo yaani mwingine shingo linaweza kua na msisimko wa kawaida likiguswa lakini mwingine ikawa 

Jumatano, 28 Desemba 2016

Ukitegemea Kupata Kitu Penzi Utaliona Chungu

Ukitegemea Kupata Kitu Penzi Utaliona Chungu.
Kamgisha blog12 hours ago

Si jambo la kushangaza kuwaona au kusikia mwanamke na mwanaume wanapendana. Yaani kila mmoja anampenda mwenzake na hivyo kuanzisha uhusiano.

Hapa nazungumzia upendo wa umoja na si wa wingi. Yaani wale wanaopendana huku kila mmoja akiwa hana mwenza mwingine. Inapotokea mtu ana mwenza halafu akapenda kwingine, huo ni usaliti na si mada yangu ilipolalia wiki hii.
MADA YENYEWE

Mada yangu inajieleza hapo juu; ukitegemea kitu penzi utaliona chungu.
Wapo watu ambao wanaingia kwenye mapenzi kwa sababu ya kupenda kutoka kwenye sakafu ya mioyo yao. Yaani mfano, mwanamke anatokea kumpenda mwanaume fulani pasipo na sababu yoyote. Huo ndiyo upendo unaoitwa wa dhati!

Lakini wapo wanaopenda kwa sababu ya kitu. Mfano, mwanamke anatokea kumpenda mwanaume kwa sababu ana gari, ni msomi, ana pesa,  ni mfanyabiashara, ana cheo serikalini, ni staa wa mpira wa miguu, ni mwimbaji mzuri wa Bongo Fleva au ana umaarufu sana mitaani.
HATA MBWEMBWE ZINA UPENDO?

Katika hili, nimewahi kushuhudia dereva wa bodaboda akipendwa na msichana kwa sababu tu ya uendeshaji wake wa bodaboda mitaani. Akiingia watu wanajua huyo ni Yusuf kwani mlio mkubwa, mwendo kasi akiwakwepa watoto wa mitaani, honi nyingi, breki za ghafla, sehemu nyembamba anapita kwa spidi na watu wanamsema vibaya kila siku; ‘huyu Yusuf huyu, iko siku.’

Kwa tabia hiyo tu, msichana mmoja aliondokea kumpenda sana Yusuf. Nilibaini hilo kwani Yusuf alipokuja kunyang’anywa pikipiki na bosi wake akawa hana mbwembwe tena na uhusiano wake na yule msichana ukafa.

Yusuf hakuwa na pesa za kumhonga huyo msichana, kwani yeye alikuwa akifanya biashara zake, sanasana yeye Yusuf ndiye aliyekuwa akipigwa tafu ya vijisenti.
LAKINI KUNA KUNDI HILI

Kundi ninalopenda kulizungumzia kwa leo ni lile la wanawake hasa, ambao wanaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume kwa dira zao.

Utakuta mwanamke anamkubali mwanaume kwa sababu tu amehisi atakuwa akipewa pesa nyingi. Au kama mwanaume ana duka, anategemea akimkubali atakuwa akipewa bidhaa za dukani bure.

Wengine ni wale wanaoingia kwenye uhusiano kwa sababu wanaume hao wana vyeo vikubwa au ni mastaa, hawa ndiyo ninaosema mimi kwamba, inapotokea pesa zimekata, hapewi kama zamani, inapotokea cheo kimeisha, inapotokea hali ya biashara inayumba hivyo hapewi mchele kama zamani ndiyo hujuta na kuliona penzi ni chungu.
KUWA KATIKA KUNDI HILI

Siku zote unapotaka kuingia kwenye uhusiano kubali kwa mwanaume ambaye kila ukipima upendo wako kwake unauona hauna sababu yoyote. Yaani humpendei pesa, humpendei cheo wala ustaa, bali unampenda tu! Ndiyo maana wahenga walisema penye penzi la kweli, mwenye chongo huonekana ana makengeza!

Ukipenda kwa mtindo huu, huwezi kuteseka kwani hali yoyote utakubaliana nayo.
VISIT WEBPAGE

Jumatatu, 26 Desemba 2016

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
KAMGISHA BLOG / 8 hours ago

LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300,000 toa sh.69,500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69,500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20,000 gunia la pumba lina kilo 70.

Paraza kilo 25 = 700x25 =17,500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10,500
layer's consetraite

Kilo 25 kifuko. = 21,500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69,500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170,000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15,000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20,000.

Jogoo 1 = 20,000
Majike 10 x15,000= 150,000 jumla 170,000.
Itakuwa imebaki shs. 60,500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10,000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.

Mbinu za Kupata Mtaji wa Biashara

Mbinu za Kupata Mtaji wa Biashara
KAMGISHA BLOG / 4 hours ago

Watu wengi wanatamani kumiliki biashara siku moja na huenda wana mipango mizuri juu ya bishara zao. Mipango hii inaweza ikawa vichwani tu au mingine katika maadishi lakini inapofika wakati wa utekelezaji wa mipango hii ukosefu wa mtaji wa biashara hiyo ni kipingamizi kwa wengi.

Lakini kuna jinsi kadhaa ambazo zinaweza kusaidia upatikanaji wa mitaji kwajili ya biashara.

 Aina Za Mitaji
Kuna aina mbili ya mitaji kwaajili ya biashara au uwekezaji wa aina yoyote.

Mtaji wa Mkopo
Mtaji wa Mmiliki

 Mtaji wa Mkopo unakuwezesha kukopa toka kwa taasisi za fedha au mtu binafsi wakiwemo ndugu ,jamaa na marafiki na kuhitajika kulipa katika kipindi maalumu ikiwa pamoja na riba au bila riba.

Aina hii ya mtaji inakuwezesha kufanya biashara lakini ni lazima uwe makini katika utunzaji wa fedha zako na uzalishaji wake kwani mwishowe utahitajika kurudisha fedha zote pamoja na riba pengine kila mwezi.

 Mtaji wa Mmiliki ni mtaji toka kwa mtu au kampuni ambayo inahitaji kuwa na umiliki wa sehemu ya bishara. Hawa wanataka kupata faida kutokana na uwekezaji katika kampuni au biashara yako.

Kama uko tayari kutoa sehemu ya umiliki wa biashara yako basi mtaji wa aina hii utakusaidia kuanzisha au kuboresha bishara yako.

Changamoto Za Kupata Mitaji:
Kupata mtaji wa biashara ni changamoto kubwa kwa wajasiriamali kote duniani. Japo fedha za mikopo zinapatikana katika mabenki lakini bishara nyingi hazina miundo mizuri na mifumo ya fedha kuwezesha kupata mikopo. Benki zimekuwa na masharti magumu sana kiasi kwamba bishara nyingi haziangalii huko kama sehemu ya kupata mikopo.

Mikopo toka kwa ndugu na jamaa pia ina changamoto zake,si rahisi ndugu au rafiki akakuamini au akaamini kuwa biashara yako itafanikiwa,tunajua asilimia 90 za biashara zinazoanza zinakufa kila mwaka. Hili linawapa wasiwasi sana wakopeshaji.

Mambo Ya Kuangalia Kabla Ya Kupata Mtaji

Mtaji Toka Kwenye Mikopo:
Ili kupata mikopo kunahitajika dhamana kuwahakikishia wakopeshaji wako kuwa kama hutafanikiwa basi ni kwa jinsi gani fedha zao zitarudi.

Na utakutana na msharti mengi magumu,dhamana inaweza kuwa kama ifuatavyo:

Nyumba
Kiwanja
Shamba
Gari
Mali za nyumbani au ofisini(biashara yenyewe)
Ni lazima ujiulize mapema kama uko tayari kuweka mojawapo ya vitu hivi kuwa dhamana.

Kwa namna hii ni rahisi kupata mkopo na ni lazima urudishe deni vinginevyo utapoteza.

Huu ndio ujasiriamali wenyewe, uthubutu wa kufanya mambo ya hatari katika harakati za kufanikiwa katika biashara.

Mtaji Toka Kwa Wawekezaji:
Kama utaamua kuingiza wawekezaji wengine katika biashara yako basi pia nilazima ufikirie mapema kuwa kutakuwa na taarifa ambazo watahitaji kujua juu ya mwenendo wa biashara yako.

Je unapata faida kwa sasa?
Muelekeo ukoje,unapanda na bidhaa au huduma zinahitajika?
Ni kwa namna ipi fedha zinzohitajika zitawekezwa ili kuboresha biashara na kuleta faida kwa haraka n.k
Waekezaji nao wanaangalia hatari ya kupoteza fedha zao na pia muda wa kurudisha fedha wanazowekeza na faida itakayozalishwa.

Kama biashara yako haiwezi kuonyesha haya kabla,ni ngumu kupata wawekezaji katika bishara yako.

Mpango Bishara na utunzaji mzuri wa mahesabu ya biashara yako yatasaidia sana kutoa taarifa hizi na hivyo kukusaidia kupata wawekezaji.

Taarifa Za Fedha Na Mpango Wa Bishara Ni Nyenzo Muhimu Kupata Mtaji Wa Biashara
Kama ni niashara mpya ,kutahitajika kuwa na mpango wa biahsara,andiko ambalo linaelezea jinsi ambavyo biashara yako itafanyika ,kiasi cha fedha kinachohitajika, bidhaa na huduma utakazo toa ,masoko,na wafanyakazi.

Andiko hili litasaidia kushwawishi wawekezaji na watoa mikopo.
Kama biashara yako iko tayari na unataka kuongezea mtaji, basi utahitaji kuwa na taarifa za hali ya fedha ya bishara yako, pia unaweza ukaandaa mpango wa biashara unaoelezea mwelekeo wa biashara katika miaka kadhaa mbele.

Wafanyabishara wengi wa kati na wa chini hawafanyi haya, ndio maana kunakuwa na ugumu kupata mitaji ya kuanzia au kukuza biashara.

Huenda ukahitaji msaada toka kwa wataalamu wa biashara na upate usaidizi wa kitaalamu,andaa fedha kidogo kwajili ya huduma hizi. Kuna makampuni mengi tu sasa hivi ambayo yanatoa huduma kwa wafanyabiashara kwa gharama ndogo.

Mbinu 5 Za Kupata Mtaji Wa Biashara:
Aina hizi zote za kupata mitaji zinaingia katika makundi mawili yaliyotajwa hapo awali aidha ni mkopo au uwekezaji.

1. Mkopo Toka Benki Au Tasisi Za Mikopo
Benki zote hutoa mikopo kwaajili ya biashara ila taarifa za muhimu zinahitajika kuhusu mwenendo wa biashara kama tayari imeshaanza au Mpango wa biashara unaoelezea jinsi ambavyo biashara itaendeshwa na jinsi ambavyo deni litalipwa.

Benki huhitaji vitu vya thamani kwajili ya dhamana ya fedha watakazokupa kama mtaji.

Iwapo fedha hazitarudishwa kama ambavyo iliwekwa katika masharti ya mkopo basi mali hiyo itauzwa ili kufidia deni.

Hili limekuwa ni changamoto kwa wengi kupata mikopo toka benki. Hasa kwa biashara anbazo zinaanza na hazina uhakika wa kufanya vizuri na uwezo wake wa kurudisha deni.

Aina hii ya mikopo inaweza ikawasaidia wale ambao bishara zao zimeshasimama na wanafanya kwa faida. Pia kwa zile biashara ambazo mzunguko wa fedha ni mkubwa na hawatahitaji muda mrefu wa kulipa deni.

Benki mpya mara nyingi huwa na msharti rahisi kuliko benki kongwe.
Aina nyingine ya mikopo ambayo inafanana na ile ya benki ni toka katika taasisi za mikopo. Taasisi hizi zinatoa masharti nafuu kido kuliko yale ya benki. Nchini Tanzania kuna tasisi maarufu kama FINCA,Blue ,Branc na nyingine nyingi ambazo zinatoa mikopo ya biashara.

Mara nyingine utahitaji kuwa katika vikundi ili kupata mikopo kwa urahisi au kuwa na biashara iliyosajiliwa kisheria.

2. Mkopo Toka Kwa Ndugu, Jamaa Au Marafiki
Ndugu na Marafiki ni sehemu nyingine ambayo unaweza kufikiria unapohitaji mtaji wa biashara.

Ni watu wanaokupenda na kukuamini na wako tayari kukusaidia katika harakati zako za kufanikiwa kibiashara. Wako tayari kukusaidia kama wana uwezo wakufanya hivyo. Lakini bado wanahitaji uhakika kuwa fedha zao zitarudi. Watapenda kujua mpango wako na ni lazima uwe tayari kuwajulisha,sio tu kabla hata baada ya kupata mkopo ili wajue mwenendo wa fedha zao.

Kumbuka dhamana hapa haitakuwa mali bali uaminifu wako kwao. Ukishindwa kufanya ulichoahidi utavunja uhusiano wenu mzuri uliojengeka kwa muda mrefu.

Ni vyema kufikiria kwa makini kama utahitaji kuchagua njia hii,vinginevyo si njia nzuri sana.

3. Toka Katika Vikundi Vya Kuweka Na Kukopa
Vyama vya Kuweka na Kukopa vinatoa mikopo kwa wanacama wake. Katika vyama hivi wanachama wanatakiwa kuweka fedha katika akaunti zao. Mwanachama anaruhusiwa kukopa kulingana na kiasi alichoweka. Baadhi ya vyama vinaruhusu mwanachama kuchukua mkopo kufikia mara nne ya kiasi alichoweka. Mkopo huu huwa na riba ndogo ulilinganishwa na benki.

Pia masharti yake si magumu na ya hatari kama ya benki.

Kuna vikundi vingine vya kijamii ambavyo wanachama wamekuwa wakifanya hivyo na vinatoa fursa kwa wanachama kupata mitaji kwa kukopa.

Vikundi vya Kuchangiana:
Pia kuna mtindo wa kuchangiana kila mwezi ambapo wanachama katika kikundi watachanga kiasi fulani cha fedha na kumpa mmoja wao ili afanya kitu fulani muhimu ambacho asingeweza kwa kuwekeza binafsi.

4. Mtaji Toka Kwa Wawekezaji Binafsi Wa Nje
Kuna watu binafsi na makapuni ambayo tayari yanafedha na yanahitaji kuwekeza katika biashara yenye kupata faida ili fedha zao ziongezeke. Watu hawa wanaweka fedha benki ambako hazizai kwa riba nzuri kulinganisha na biashara.

Watu hawa wanahitaji taarifa za kutosha kuwashawishi kuwa fedha zao ziko katika mikono sahihi. Pia hata baada ya kuwekeza watahitaji taarifa za mara kwa mara juu ya maendeleo ya biashara. Kama biashara ni mbaya huenda wakatoa fedha zao ili wasipate hasara.

Hii ni sehemu nyingine ambayo huwa haiangaliwi sana na wajasiriamali wadogo kwani ile dhana ya kufanya biashara kwa kushirikiana bado haijakubalika na kufuatwa. Lakini njia hii inatoa nafasi kwa wale ambao wanabiashara yenye mfumo mzuri na inakosa mtaji tu kufanikiwa.

Lakini hata kwa biashara zinazoanza, kama kuna mpango mzuri na wazo lenyewe la bishara linaonyesha kufanikiwa basi wawekezaji hawa watakuwa tayari kuwekeza katika biashara yako.

Hii ni njia nzuri kwa wale wenye uwezo wa kubuni biashara nzuri zenye kutoa huduma kwa watu na yenye nafasi kubwa ya mafanikio lakini wanakosa fedha za kuanzia. Hawa wanaweza wakaanza hata bila kuwa na shilingi moja,mpango wa biashara pekee ndio wanachohitaji.

Kisha ongea na matajiri katika mji wako(angalia usitoe taarifa zote za mpango wako mpaka upate uhakika kuwa utapata fedha-kuzuia kuibiwa mawazo).

5. Uwekezaji Binafsi (Kuweka Akiba)
Inasemekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya bishara ndogo zonazoanzishwa huanza kutokana na akiba binafsi ya wamiliki.

Mmiliki kupitia nyenzo zilizopo za kupata kipato kama ni kazi au biashara nyingine iliyosimama tayari anaweka akiba maalumu kwajili ya kuanzisha biashara mpya. Kiasi cha kuanza kikifikiwa basi fedha hizo zinaingizwa katika biashara mpya.

Fedha hizi zinaweza zikaingizwa kama mkopo binafsi ambapo baadae zitarudishwa katika akaunti binafsi ya mmiliki au zikaingia kama uwekezaji katika biashara ambapo mmiliki atapata faida tu itakayozalishwa.

Vyovyote vile njia hii ni nzuri kwani hakuna madeni toka nje na unaweza ukawa na amani sana katika uendeshaji wake.

Kama wewe ni mwajiriwa na unafikiria kuwa na bishara yako basi njia hii ya kuweka akiba kwajili ya bishara yako ni njia sahihi.

Unaweza ukafungua akaunti nyingine nje na ile ya kawaida na kuhamisha asilimia fulani kila mwezi kwenda katika akaunti hiyo ya biashara (10-25% ni kiwango kizuri)

Ukitaka Mafanikio Ni Lazima Uchukue Hatua Za Haraka
Imesemwa kuwa usisubiri hadi kila kitu kikamilike ndio uanze,katika biashara hiyo inaweza kuwa ngumu au ikakufanya usianze kabisa.

Kama tayari una mpango wa bishara unaovutia usisite kuanza kwa kukosa mtaji,chagua njia mojawapo ya kupata mtaji na uanze.

Ukitaka kupanda jengo la ghorofa ndefu,anza ngazi ya kwanza na utajikuta uko juu .
Ukisubiri kufanya yote kwa mara moja huenda usifanye kabisa. Unapoanza kufanya kitu unapata urahisi kwa jinsi ambavyo unaenda mbele na njia inakuwa wazi kwako katika kila hatua unayochukua.

Jumatano, 14 Desemba 2016

Madhara ya kutofanya tendo la ndoa mda mrefu

Madhara ya Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu
KAMGISHA BLOG / 34 minutes ago

Habari zenu, nimeona niwaletee hili nina imani mtajifunza hasa kwa wale wasiofahamu,Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya:

Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,
kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
Kusahausahau,
Kupendelea story za mapenzi,
Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),
Kuumwa na kichwa,
Kukakamaa mgongo (wanaume),
Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),
Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala

kama ulevi n.k.

Jumanne, 13 Desemba 2016

Je, umekosea Tumaini

Je, Umekosa Tumaini La Kufanikiwa? Jifunze Kupitia Mambo Haya
KAMGISHA BLOG / 19 minutes ago

Kipo kipindi katika safari yako ya mafanikio kutokana pengine na changamoto za kimaisha, unajikuta unakata tamaa na matumaini yote yanapotea.

Katika kipindi hiki, kila unachokifanya kinakuwa hakileti matokeo na mbele yako unakuwa unaona giza na hakuna hata njia wala mwanga wa matumaini. Je, kwa hali  kama hii inapokutokea unafanyaje?

Kwa mfano, tuchukulie umeanzisha mradi fulani, lakini umejitahidi sana ili ukuletee angalau faida imeshindikana, hapo inapokuwa hivyo unawaza nini au unachukua hatua gani?

Najua kuna mambo mengi yanakuwa yanapita kichwani mwako, ikiwa nia pamoja na kuachana kabisa na kitu hicho ambacho sasa unaona hakifai tena na hakina manufaa kwako.

Lakini leo hapa kwa kupitia makala haya, naomba nikushirikishe mambo ya msingi ya kujifunza hasa inapotokea pale umekata tamaa na kukosa matumaini  kwa kile unachokifanya.

Jambo la kwanza unalotakiwa kujifunza na kulitambua  ni kwamba hakuna mafanikio ya mara moja. Hapa hii yote inatuonyesha ili tuweze kufanikiwa inatakiwa tujaribu tena na tena hadi kufikia mafanikio.

Inapotokea unaona kama umekosa tumaini unaonyeshwa kwamba sasa huu sio wakati wa kutulia na kujiona mnyonge uliyopotezakila kitu, bali ni wakati wa kunyanyuka tena na kujaribu njia zingine za kukupa mafanikio yako.

Jambo la pili unalotakiwa kujifunza ni kwamba katika maisha hakuna kukata tamaa. Ni kweli, unakuwa unajiona umekosa matumaini na huna chako tena, lakini ni wakati wako wa kijiamini tena na kushikiria ndoto yako mpaka kufanikiwa.

Hata kama unaona dunia na kila hali kama imekutenga, jifunze hapo ulipo sio ndio mwisho wa mafanikio yako ipo nafasi ya kufanya tena na ukafanikiwa sana kuliko unavyofikiri.

Jambo la tatu la kujifunza hasa pale unapokosa matumaini tena ni panga mipango yako upya. Hiki hasa ndicho kitu ambacho unachokuwa uanaambiwa na maisha.

Badala ya kukaa chini na kulia na kunza kulalamika kwa kushindwa kwako kufanikiwa, lakini unachoambiwa na maisha panga mipango yako upya, tafuta njia nyingine na tumia akili yako vizuri hadi ufanikiwe.

Tambua ili kufanikiwa inatakiwa ujue hakuna mafanikio ya mara moja, hakuna kukata tamaa na inabidi kila wakati kupanga mipango upya.  Hayo ndiyo mambo ya msingi  unayotakiwa ujifunze hasa pale unapokata tamaa na kukosa.

Jumatatu, 12 Desemba 2016

ASILI YA USLAMU

YUDA 3 Ndugu wapenzi, wakati nimo katika jitihada ya kuwaandikieni juu ya ule wokovu tunaoshiriki sote, nimeona lazima ya kuwaandikieni na kuwahimizeni mwendelee kupigana kwa ajili ya imani ambayo Mungu amewajalia watu wake mara moja tu kwa wakati wote.

Wednesday, December 8, 2010

Asili ya Uislamu

IJUE DINI YA UISLAMU NA ASILI YAKE

Na Mwalimu Eleutary H. Kobelo.

Utangulizi

Kwa miaka mingi waislamu duniani, wanatuhimiza sana sisi Wakristo tuache imani na dini yetu, ili tuingie katika dini yaoya uislamu. Waislamu wanasema dini yao ndio ya haki, mbele ya Mwenyezi Mungu, na tena wasema manabii wote walikuwa waislamu, wanaendelea kusema kuwa hata Bwana Yesu naye alikuwa mwislamu, waislamu wanaendelea kusema kwamba dini ya Islamu haikuchukua au kurithi hata chembe (kidogo) ya tabia ya mafundisho ya ibada za kikafiri, kushirikina na ujahili (yaani ujinga), kwani wanasema Uislamu ni dini safi kuliko zote. Swali la muhimu ni hili. Je, ni kweli kwamba dini ya uislamu haikuchua tabia na mafundisho ya ibada za kikafiri, kushirikina na ujahilia? Ili kujua yote hayo fuatilia kwa makini somo hili lililoandikwa na Mwalimu wangu Mwinjilisti Kobelo na kupitiwa upya nami Mwalimu Chaka.

Sehemu kuu tano za somo

Je, manabii wote walikuwa waislamu?Nani aliyekuja na dini ya kiislamu?Je, dini ya kiislamu imechua ibada za waarabu za zama ujahilia (yaani ujinga)?Wajibu wa mkristo baada ya kujua Uislamu.

1. Je, Manabii wote walikuwa waislamu?

Hoja kubwa ya waislamu ni kule kutuhimiza wakristo tukubali kuwa waislamu kwa kusema kwamba manabii wote wa Mungu walikuwa waislamu, hivyo wanataka tuache imani yetu tuwe waislamu. Lakini inafaa kwanza kuvichunguza vitabu vya kiislamu kuhusu ujio wa Qurani inafundisha nini? Na je, ni nani aliyeleta dini hiyo? Qurani ya Allah Mungu kama wanavyoamini waislamu inasimulia hivi;

Qurani 6:14 Suratul An-Am (Wanyama)

Sema: hakika nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu.

Katika aya hii tunaona Muhammad ndiye mtu wa kwanza kuamrishwa asilimu.

Imesimuliwa pia ya kwamba Muhammad S.A.W. alisema, “Sisi waislamu ndiyo wa mwisho kuja” hayo tunayasoma katika Sahih Al-Bukhari vol. ix Hadithi na 587.

Muhammad vilevile aliwaambia wafuasi wake wafuate njia ya waliowatangulia. “nchi kwa nchi, hatua kwa hatua hata kamaikiwa waliingia katika shimoni mwa mjusi” masahaba zake wakauliza “Layahud waal Na-swara? Yaani wayahudi na wakristo?Akawajibu Farman? Yaani nani zaidi? Hayo tunayaona katika Sahih Muslim vol. iv katika Al-lim, hadithi na 6448. Kutokana na jibu hili la Muhammad (S.A.W.) ni dhihiri kuwa dini ya Uislamu ilitanguliwa na dini yetu Wakristo na hata ile dini ya Kiyaudi.

Manabii wa Mungu Yehova walifuata dini (njia) hii.

Tunaposoma maandiko matakatifu ya Biblia yanatufundisha kuwa manabii waliongozwa na huyu.

1 Petro1:10-11

katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta tafuta na kuchunguza chunguza ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakati upi na wakati wa namna gani ulioonywa na roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao.

1 wakorintho 10:1-4

kwa maana ndugu zangu,sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu. Wote wakapita kati ya bahari,wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingi na katika bahari; wote wakala chakula kilekile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata na mwamba ule ulikuwa ni kristo.

Katika aya hizi tunaona wazi wazi kuwa manabii wote waliongozwa na roho wa Kristo Yesu ambaye alikuwa ndani yao.Musa pamoja na watu wake pia walifuatwa na kristo naye aliwalisha na kuwanywesha.Wote waliongozwa na Bwana Yesu yeye mwenyewe aliwaita “watu wa Kristo” Soma Marko 9:38-41 hii ni kwasababu Bwana Yesu ndiye kiongozi wetu. Tazama Mathayo 23:9, tena Bwana Yesu ndiye njia (dini) ya kweli na uzima Yohana 14:6 hivyo manabii wote walikuwa ni watu wa Kristo kwasababu roho yake Yesu ulikuwa ndaniyao ikiwaongoza.

Maana ya neno Islam

Neno islam ni la lugha ya Kiarabu. Maana yake ni “Utii” au “Amani” katika Qurani neno Islam limetajwa mara 38. ijapokuwa neno Islam limetajwa mara nyingi lakini neno hilo ni tofauti na dini ya uislamu hii ni kwasababu dini a Uislamu maana yake ni kujisalimisha chini ya amri za Allah au amani chini ya sheria za Allah. Qurani ya Allah Mungu kama wanavyoamini waislamu inasimulia kumhusu Muhammad (s.a.w.) hivi.

Qurani 6:163 Suratul Al-An-Am (Wanyama)

Na haya ndiyo nilivyoamrishwa na mimi ni wa kwanza wa wanaojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu).

Qurani 39:12 Suratul Az-zumar (Makundi/Vikosi)

“Na pia nimearishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu.”

Nani aliyekuja na dini ya kiislamu?

Tunaposoma katika ufafanuzi wa aya ya 19-20 kati ka suratul Yusuf ulio ndani ya Qurani juzuu ya 12 chapa ya tatu ya kiswahili ukurasa wa 311 kuna maneno ambayo yanaelezea mtu aliyekuja na dini ya kiislamu hapa duniani na maneno yenyewe ni haya…

Unaona kwanza kulikuwako zaidi ya miaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo Nabii Muhammad khalafu wakausingizia Uislamu kuwa ndio ulikuja na kuuza watu.

Kadiri ya ufafanuzi huu uliomo ndani ya qurani, na ushahidi wa vitabu maarufu vya hadithi za muhammad katika sahih Al-Bukhari na sahih muslim. Na vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na masheikh wa dini ya kiislamu, inathihirika waziwazi kuwa dini ya uislamu imeletwa na kuanzishwa na Muhammad (s.a.w.) mfano mzuri wa mwanzo wa dini ya uislamu tunauona katika kitabu kiitwacho maisha ya nabii muhammad (s.a.w.) kilichotungwa na aliyekuwa kadhi mkuu wa zanzibar na baadaye nchi ya kenya marehemu sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy. Katika ukursa wa 18 kuna maneno yanayo husu mke wa muhammad aliyeitwa khadija binti khuweylid nayo yanatuhadithia hivi…

Akarejea kwa mkewe bibi khadija, akamsimulia habari hii. Palepale bibi huyu akamwamini, akawa ndiye mtu wa awali kabisa kushehedusha shahada ya uislamu.Basi mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke.

Katika kitabu hicho hicho cha maisha ya nabii muhammad ukurasa wa 18 kifungu c. wametajwa waislamu wa awali kabisa nao ni hawa…

(i) Mwislamu wa kwanza

Bibi Khadija bint Khuweylid

Mtume aliamrishwa kufundisha dini siku ya jumatatu na bibi huyu alisilimu siku hiyo hiyo akafanya ibada na mtume usiku ule ule kabla ya mtu yeyote ulimwenguni huyu ndiye aliyefuzu kwelikweli.

(ii) Mwislamu wa pili

Sayyidina Ali bin Abi Talib bin Abdul Muttalib

Alipomwana mtume na bibi Khadija usiku ule wanafanya mpya aliwauliza, “hii ni ibada gani?” mtume alimfahamisha na akamtaka awe pamoja nao lakini yeye alikataa kwanza akasema mpaka niende nikamshauri baba yangu”. Mtume akamkataza kuitoa siri ile nje. Mara asubuhi ya usiku ule ule, kijana huyu akaja kwa mtume akampa habari kuwa yeye yu pamoja nao. Akawa ndiye islamu wa pili duniani. Aliposilimu alikuwa kijana wa miaka 10 hivi.

(iii) Mwislamu wa tatu na wa nne.

Zayd bin Haritha Al Ka’bi na Bibi Aymana.

Huru wa mtume na mwanawe wa kupanga alikuwa akikaa pamoja na mtume na akasilimu kama sayyidina Ali mchana wa jumane. Alisilimu yeye na mkewe, bibi ummu Aymana yaya wa mtume.

Hawa wote ndio waislamu wa awali kabisa ambao walisilimu mara baada ya muhammad s.a.w. kuleta dini ya uislamu ambayo alianzisha rasmi hapa duniani jumatatu ya siku ya 17 ya mwezi wa ramadhani sawa sawa na 27th december ya mwaka wa 610 baada ya kristo. Kabla ya muhammad dini ya kiislamu haikuwepo kabisa duniani.

Je, dini ya uislamu imechukua ibada za waarabu wa zama za ujahilia (yaani ujinga)?

Wakati wa ujahilia (ujinga) kabla ya dini ya uislamu makureshi ambalo ni kabila la muhammad s.a.w. na waarabu wenzao, walikuwa wakiabudu miungu mingi yapata 360 hivi. Kawaida hiyo ya kuabudu kwao miungu mingi kumesimuliwa waziwazi katika quarani na vitabu mbalimbali vya kiislamu. Vitabu hivyo vimeandikwa na masheikh na wanachuoni wengi, nitawataja baadhi yao nazo ni hawa…

(i) Maulamaa sayyid Abul A’la Maududi

Katika kitabu chake kiitwocho katika kuufahamu uislamu ukurasa wa 42-44 kuna maneno haya…”Bara Arabu mwina wa kiza wafanya biashara waarabu walijikokota masafa marefu ilikuwa vigumu kwao kupata hata chembe ya elimu wachache waliojua kusoma na kuandika walikuwa wakiabudu mawe, miti, masanamu, nyota na pepo, kwa ufupi kila kilichowapitia akilini mwao, hawakujua hata kidogo mafunzo ya mitume waliowatangulia.Walikua na dhana kuwa ibrahimu na ismail walikuwa babu zao, lakini walikuwa hawajui kitu kuhusu mafunzo yao ya dini na Mungu waliyemwabudu.

(ii) Sheik Abdullah saleh Al-Farsy ambaye alikuwa kadhi mkuu zanzibar na baadaye nchini Kenya

Katika kitabu chake kiitwacho maisha ya nabii muhammad s.a.w. ukurasa wa 6 kuna maneno haya… “Hata ilipokuwa karibu atadhihiri mtume mapadiri wa kinasara na makuhani wa kiyahudi waliokuwa wakikaa bara arabu walikuwa wakiwataharisha majirani zao wa kiarabu waliokuwa wakiabudu masanamu;

Qurani imetaja miungu mbalimbali iliyoabudiwa na makureshi na waarabu wenzao zama za ujahilia

(i) Waliabudu maandazi.

Qurani 25:43-44 Suratul Al;- furqan (Qurani)

Je umemuona yule aliyefanya matamanio yake (kile alichokipenda). Kuwa mungu wake? Basi je, utaweza kuwa mlinzi wake (ukamhifadhi) na haya, na hali ya kuwa hataki?) au je, unafikiri ya kwamba wengi katika wao wanasikia au wanafahamu?Hawa kuwa hao ila ni kama wanyama bali wao wanapotea zaidi njia.

Ufafanuzi wa aya ya 43 ulio katika qurani juzuu ya 19 ni huu, “waarabu kwa ujinga wao wa kuabudu chungu ya miungu walikuwa baadhi yao wakiona chochote kile kikawapwndeza hukiabudu hata andazi lililokaa kwa sura nzuri.

Hapa tunaona kuwa qurani inasimulia wazi wazi kwamba waarabu waliabudu hata andazi na tena ni wajinga “yaani majahalia”

(ii) kuabuduwa kwa miungu ya sanamu.

Qurani 71 22-23 Suratul Nuh (Nuhu)

Na walifanya hila kubwa kubwa za (kubatilisha dini). Na waliwaambia (wafuasi wao): “Msiache miungu yenu wala msiwaache waddi wala suwa’a wala yaghuta wala ya’uqa wala Nasra”. (Majina ya waungu wao wa kisamu).

Hii ni miungu ya uongo ya sanamu ambayo iliabudiwa na waarabu mungu waddi alikuwa na umbo la mwanamke yaghuta umbo la simba, ya’uga umbo la farasi hayo yanapatikana katika kitabu kiitwacho “history of Islam kilichoandikwa na Pro. Masudul Hassan ukurasa wa 43

(iii) kuabudiwa kwa miungu iitwayo lata, uzza na manata

Qurani 53:18-20,23 suratul An-najm

kwa yakini aliona nabii muhammad mambo makubwa kabisa katika alama (Qudra) za mola wake.je mume waona lata na uzza? Na manata mungu wenu mwingine wa tatu, kuwa ndio waungu hao badala ya mwenyezi mungu? Hayakuwa hayo majina ya lata mungu mwanamke, na uzza mungu mwanamke mwenye enzi na manata, mungu mwanamke anaye neemesha ila ni majina tu mliwapa nyinyi na baba zenu…

(iv) kuabudiwa kwa Allah (s.w.) na majahilia (wajinga)

makureshi pamoja na waarabu wenzao ambao walikuwa wakabudu miungu mingikama tulivyoona huko juu. Vilevile miongoni mwa hiyo miungu walimuabudu Allah (S.W.) ambaye ndiye aliyekuwa mungu mkubwa, na miungu ya hata na uzza na manata wakawaitakadi kuwa mi waungu wanawake ama wake zake Allah au watoto wake. Hayo tunayaona katika ufafanuzi wa aya ya 180 katika Qurani suratul Al- A’raf na pia katika kitabu kiitwacho history of isalmu kilichoandikwa na pro masudul hasan ukurasa 43. ushahidi wa wazi zaidi wa kuonyesha kuwa waarabu majahilia walimuabudu Allah tunaupata katika vitabu vifuatavyo…

(i) kuzaliwa kwa Muhammad S.A.W. mtume wa waislamu

maombi na dua ya abdul mutalib kwa Allah.

Tunaposoma kitabu cha maisha ya Muhammad S.A.W. kilitangwa na sheikh Farsy ukurasa wa 5 kuna maneno hayo…

Pale pale alfajiri alipokwisha kuzaliwa mtume alikwenda kuitwa babu yake kuja kumwona mjukuu wake. Babu huyu alifurahi sama na akamfunika manguo mjukuu wake, na akamfunika manguo mjukuu wake, akajikongoja naye mpaka kwenye Al-ka’ba akafungua mlango akaingia ndani, akasimama, akamwombea dua kwa mashairi mazuri ya kiarabu aliyoyatunga mwenyewe wakati ule ule, kisha akarejea naye na jua bado halikuchomoza.

Ushahidi wa wazi unaothibitisha kuwa baba yake Muhammad Abdul muttalib aliomba dua kwa Allah tunaupata tunaposoma utangulizi wa suratul al-fyl ulio katika juzuu ya ukurada wa 946 Qurani iliyotafsiriwa kwa kiswahili chapa ya nane tunasoma maneno hayo. “chifu mkuu wa makka zama hizo alikuwa Abdul muttalib, alikwenda al ka’ba pamoja na baadhi ya machifu wa kikuraish na akilishika komeo la chuma la mlango wa al-ka’ba, akamwambia Allah (S.W.0 kuilinda nyumba yake pamoja na wahudumu wake. Zama hizo kulikuwa na masanamu 360 ndani na kando ya Al- ka’ba.”

(v) imani ya Abdul muttalib ilikuwa hii.

Katika kitabu kilichoandikwa na mwanachuoni maarufu wa kiislamu aitwae ale muhsin barwani ukurasa wa 153 tunasoma maneno haya; “hapakutokea mwarabu ambaye alipewa jina hilo na babu yake tangu kuzaliwa kwake, na huyo babu hakuwa mkristo bali alikuwa akifuata mila za kishirikina.” Na wala hakujua taurati wala injili.

(vi) himizo la Muhammad (S.A.W.) kwa makureshi wenzie kuhusu mungu aitwae Allah.

Katika kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu kilichotungwa na sheikh said moosa muhamed al kindy juzuu ya mwanzo na pili chapa ya kumi ukurasa wa 130 tunadoma maneno haya: “katika wakati wa ujaahiliya kabla mtume (S.A.W.) kupata utume alikuwa akiwaambia waru “enyi watu semeni laa ilaha illah laah mtafuzu” yaani hana mola ila Allah mtafuzu.

Huu ni ushahidi wa wazi kabisa ya kwamba Allah aliabudiwa na makureshi ma waarabu wenzao hao watu walikuwa washikina , wapagni na majahilia (wajinga).Kumbuka Muhammad alikuwa ni mkureshi naye aliposema “hapana mola ila Allh” alikuwa yupo za ujahilia na hakuwa anajua kitabu wala imani tazama Qurani 42:52 Suratul shuraa.

(vii) je, mungu anayeabudiwa ba waislamu jina lake ni nani?

Qurani 17:110 suratul ban israil wana waIsrael

sema: “mwombeni mwenyezi mungu kwa jina la Allah au muombeni kwa jina la rahman kwa jina lolote mtakalo mwita katika hayo itaifaa: kwani ana majina mazuri mazuri,” wala usiiseme sala yako kwa sauti kubwa wala usiseme kwa sauti ndogo, bali shika njia baina ya hizo katikati si kwa kelele wala kimya.

Katika aya hii tunaona jina la mungu anayeabudiwa ba waislamu anaitwa Allah.Katika qurani jina hilo limetjwa mara 2,866 kumbuka kuwa makureshi na waarabu wenzao waliokuwa washirikina wapagani na majahilia wajinga kabla ya uislamu walimuabudu mungu huyo aitwae allah swali muhimu je, waislamu hawakutithi mungu wa makureshi? Tafakari kwa makini.

(viii) mji mkuu wa makureshi na waarabu wenzao zama za ujahilia ambako walikuwa wanaenda kuhiji ni huu

Tunaposoma utangulizi wa suratul Quraysh katika juzuu ya 30 ukurasa wa 950-951 chapa ya nane ya Qurani ya kiswahili kuna maneno haya…kabila la kureshi lilikuwa limetawanyika kote hijaz hadi zama za Qusayy bin kilaab mmoja wa mababu wa mababu wa mtume (S.A.W.). kwanza kabisa Qusayy aliwakusanya makureshi pamoja huko makka, na hivyo kabila hili likawa wadhamini wa Al-ka’ba kwa msingi huo, Qusayy alikuwa akiitwa mujammi mkusanyaji wa wartu wa habila lake. Mtu huyu kwa busara yake aliweza kuasisi serikali katika mji wa makka, na akaweka mipango mizuri kwa ajili ya mahujaji wajao toka kote arabuni, na matokea yake ni kuwa makureshi walipata umaarufu mkubwa miongoni mwa makabila ya kiarabu.

Hapa tunaona kuwa zama za ujahilia na upagani kabla ya dini ya uislamu waarabu wote walienda kuhiji katika mji wa makka kwenye nyumba ya Al-ka’ba inayoitwa “Bait-ullah” yaani nyumba ya allah.Kumbuka nyumba hiyo hiyo wapagani wa kiarabu zama za ujahilia (ujinga) waliabudu miungu 360 na Allah ndiye mungu wao mkuu.

Mji mkuu wa hija kwa waislamu ni huu.

Qurani 3:96 suratul Al-aal-imran (watu wa imran)

kwayakini nyumba ya kwanza iliyewekwa kwa ajili ya watu kufanya ibada ni iloe iliyoko makka, na yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote.

Qurani 22:27-29 suratul Al-Hajj. (Hijja)

Na (tukamwambia “utangaze kwa watu habari ya Hijja, watakujia, (wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyekonda kwa machofu ya njiani wakija kutoka katika kila njia ua mbali; ili washuhudee manufaa yao na ili wakushirishe kulitaja jina la mwenyezi mungu katika diku zinazojulikana fadhila zake na juu ya yale aliyowaruzuku, nao mi wanyana wenye miguu mine. Na kuleni katika wanyama hao na mlisheni mwenye shida na fakiri. Kasha wajisafishe toka zao, na watimize hadhiri zao na waizunguke nyumba ya kale (nyumba kongwe Al-ka’ba.)

Tunaposoma ufafanuzi wa aya ya 29 ulio ndani ya Qurani katika juzuu ya 17 kuna maneno haya; “kabla ya uislamu waarabu walikuwa wakiitukuza Al-ka’ba. Na kwa ilivyokuwa ni jingo la zamani sana waliita Al-Baytul’Atiq yaani nyumba ya kale.”

Kama vile waarabu wapagani, makafiri na majahilia mji mkuu wa Hijja ni makka kuleSaudi Arabia ndivyo ilivyo kwa waislamu nao mji wao mkuu ambao wanaenda kuhiji ni makka. Isitoshe Qurani inasimulia kuwa makka ni mama wa miji soma hayo katika Qurani 6:92 suratul Al- An-Am (wanyama) waislamu popote walipo duniani wanaambiwa wanaposali waelekeze nyuso zao mahali maalumu,

Qurani inasimulia hivi

Qurani 7:29Suratul Al- Araf

Sema: mola wangu ameamrisha uadilifu, na ameniambia nikuambieni elekezeni nyuso zenu kwake wakati wa kila sala…

Je mola huyo ambaye anasema kuwaambia wenye kufuata Qurani waelekeze nyuso alipo huko ni wapi?

Qurani 27:91 suratul An-Naml

Bila shaka nimeamrishwa nimwabudu mola wa nji huu wa makka ambaye akadiri ya aya hizi tunaona kuwa qurani inasimulia kuwa mola huyo ni wa mji wa makka ambaye…

Katika ibada zao waislamu huelekeza nyuso zao kibla nako ni katika msikiti wa Al' ka’ba iliyoko makka Qurani 2:144-150 mola wa mji wa makka ndiye Allah ambaye aliabudiwa na waarabu washirikina zama za ujahilia, na ndiye huyo huyo anoyeabudiwqa na waislamu.

(ix) kuzunguka Al- ka’ba wakiwa uchi wakati wa ibada.

Kabla ya dini ya uislamu makureshi na waarabu wenzao walikuwa wakiizunguka Al-ka’ba “bait ullah’ yaani nyumba ya Allah wakiwa uchi wake kwa waume walikuwa wakiitikadi nguo ni kitu kinachopata uchafu kwa hivyo hakistahiki kuvaliwa wakati wa ibada hayo tunayaona katika kitabu cha maisha ya Muhammad ukura wa 4 kilichotungwa na shikh Abdullah saleh Al Farsy ambaye alikuwa kadhi mkuu wa Zanzibar baadaye nchini Kenya. Siyo Farsy peke yake ambaye aliyeandika hayo bali na mwanachuoni maarufu aitwae Abul A’la maududi katika kitabu chake kiitwacho katika kuufahamu uislamu ukurasa wa 43 aliwaelezea waarabu hivi: maisha yaoyalikuwa ya kishenzi. Mambo yao yalikuwa ya kishenzi na wakati wote walisherekea uzinzi kamari na ulevi. Kuteka nyara na kunyang’anya ulilokuwa useni wao, kuu na kutwaa wanawake kwa nguvu ndizo zilikuwa tabia zao halisi. Wakiweza kukao tupu uchi mbele za wenzao pasina haya wala hata kuona wamefanya jambo lolote la fedheha. Hata wake zao walikuwa wakiizunguka al-ka’ba uchi. Kwa ajili ya fikira za ujinga mtupu ati wa kuchunga heshima zao, waliwaua mabinti zao ili asije mtu akawa mkwa wao. Walikuwa wakiwaoa mama zao wa kambo baada ya kufa baba zao. Walikuwa wajinga hata wa mambo madogo ya kula, kuvaa na kunawa.Ama katika imani zao za kidini, walikuwa na ugonjwa ule ule uliotokana na uovu uliokuwa ukipoteza ulimwengu mzima.

Kumbuka Allah ndiye mungu waliomuabudu waarabu hao na nyumbayao ya ibada ni Al-ka’ba jambo la kushangaza maulamaa Abul A’la maududi ana sema kuwa waarabu hao walikuwa na uovu ulioupoteza ulimwengu mzima. Swalli je, kuzunguka Al-ka’ba na kumwabudu Allah ndio kuupoteza ulimwengu?

Je, waislamu wanapoenda Hijja wanaizunguka Al-ka’ba

Kabla ya kujua mambo wanayoyafanya waislamu kule Al-ka’ba inafaa tujue jinsi Al- ka'ba ilivyo. Neno ka'aba ni la kiarabu lina maanisha kitu cha mirabo sita iliya sawa, ka’ba ni la kiarabu linamaanisha kitu cha miraba sita iliya sawa. Ka’aba ni jingo lenye ureru wa meta 12 upana meta 10 na urefu kwenda juu meta 15 jengo hilo lipo makka kule daudi Arabia. Jingo hilo limefunikwa na na mapazia meusi yaliyotariziwa aya za Qurani kwa herufi za kiarabu kwa kutumia uzi wa dhahabu halisi. Katika pembe ya mashariki ya ka’aba kuna jiwe jeusi katika kiarabu jiwe hili linaitwa “hajarul Aswad”.

Qurani inawaagiza waislamu wafanye ibada zao za Hija hivi…

(i) kuzunguka Al-ka’aba

qurani 22:29 suratul al-Hajj

“Na kasha wajisafishe taka zao na watimize nadhitri zao na waizunguke nyumba ya kale (nyumba kongwe ya Al-ka’ba)

kadiri ya aya hii tunaona kuwa Allah anawaagiza waislamu waizunguke Al- ka’ba huko nyumba tuliona kuwa waarabu wapagani waliizunguka Al-ka’ba wakiwa uchi bila nguo je waislamu wao wanaizunguka Al-ka’ba wakiwa vipi?

Tunaposoma kitabu kiitwacho vipi uhiji kilichoandikwa na mwanachuoni wa kiislamu aitwae A. sulemani ukurasa wa 16 kuna maneno hayo: “ni haramu kuvaa nguo zilizoshonwa kwa mwanamume muhrim anayekwenda kuhiji makka kwenye Al-ka’ba (msikiti). Kushona hapa ina maana kushona kwa ajili ya kuvaliwa siyo kama kiraka, vazi linalozunguka mwili kama shati, suruali na kadhalika anaruhusiwa kufunga kwa pini au mkanda nguo za hiramu ili zisivuke yaani nguo mbili kamamgolole.

Kadiri ya maneno haya waislamu katika hija yao kule ka’ba wazunguka ka’ba wakiwa wanavaa nguo sisizo shonwa zinaitwa “ihram” yaani mashuka mawili meupe.

(x) ibada ya kuomba kubusu na kuliheshimu jiwa jeusi “hajarul Aswad” katika Al-ka,aba msikiti wa makka.

Makureshi pamoja na waarabu wenzao kabla ya uislamu walikuwa wakiheshimusana nyumba ya allah al-ka’ba pamoja na jiwe jeusi liitwalo kwa kiarabu “hajaral Aswad” wakati huo wakiendeleza ibada zao za kishiriki kipagani na zilizojaa ukafiri.Jambo linalotuthibitia kuwa makureshi waliheshimu al kaba na jiwa jeusi tulipata katika kitabu cha maisha ya Muhammad (s.a.w) kilitungwa na sheikh Abdullah saleh Al-Farsy ukurasa wa 15-16 kuna maneno haya: “kujengwa kwa Al- ka’ba mtume alipokuwa na miaka 35 Al-ka’ba mtume alipokuwa na miaka 35 Al-kaba ilifanya nyufa kubwa, na ikakaribia kuvunjika, makureshi wakafanya shauri ya kuivunja na kujenga yote upya, Al-ka’ba ilikuwa haina sakafu…lakini Hajarul Aswad lilipokuwa likitaka kuwekwa mahali pake baina ya ukuta wa kusini na mashariki.Hapo ndipo walipogombana kilaukoo ukitaka mkubwa wao aliweke. Ugomvi ukashika nguvu. Kazi ikazuilika kwa muda wa siku tano, panangojewa vita tu, tumbo litakalo shinda ndilo liweke jiwe la Hajarul Aswad…mara kwa bahati nzuri aliingia mtume, alikuwa hakupata utume bado. Na hapo wote wakasema kwa umoja wao: “Hadhal Amin huyu yule mwaminifu na sote tumekubali” mtume akalichukua lile jiwe akalitia katila shali yake, akamwita kila mkubwa na ukoo; kisha akawaamrisha walichukue kiti mpaka mahjali pake. Hapo mtume akapokea akaliweka yeye kwa mikono wake na kwa radhi yao wote.

Huu ni ushahidi kuwa makureshi na waarabu wenzao kabla ya dini ya uislamu kuja walikuwa wanaihwshimu sana Al-ka’aba na jiwe jeusi lililokuwa ndabi ya msikiti huoj wa la’aba. Ambamo ndiyo sehemu waliokuwe wakizunguka wakiwa uchi wake kea waume, na hata Muhammad tunaoma alishiriki katika Al-ka’ba hiyo kwani na yeye aliweka hilo jiwe keusi na makureshi wote walikubali afanye hivyo.Swali la muhimu la kujuuliza je waislamu hawakurithi ibads hizo za ujahilia? Endelea…

Je, waislamu wanafanya ibada ya kuomba, kugusa, kubusu na kuliheshimu jiwe jeusi “Hajarul aswad”

Tunaposoma vitabu mbalimbali vya kiislamu tunaona namna ambavyo waislamu wanavyo fanya ibada ya kuliheshimu jiwe jeusi lililo katika msikiti mkuu wa makka uitwao Al-ka’ba unaofahamikakuwa ni “bait ullah” yaani nyumba ya Allah. Baadhi ya vitabu hivyo ni hivi…

kitabu kiitwacho mkweli mwaminifu mtungaji sheikh said moosa muhamed al-kindy ya 3-4 chapa ya 14 ukurasa wa 75 kuna maneno haya; kasema mtume (S.a.W.) ya mwenyezi mungu katika Ardhi. Basi atakaye ligusa basi kafungamana na wenyezi.katika kitabu cha hadithi za Muhammad cha sahih al-bukhari vol. Ii ukurasa wa 397 hadithi na 682.kastika hadithi hii tunaambiwa kwamba “kila wakati mtume saw alikuja kwenye jiwe jeusi akalielekezea kikdolw na kusema Takbirt maana yake Allah ni mkuu.swahaba kwa mtume aliyeitwa umar bin khattab alilibusu jiwe jeusi al Al-ka’ba kasha akadema: “bila shaka nafahamu wewe ujiwe lisiloweza kumfaidia wala kumdhuru mtu yeyote.Kama nisingalikuwa nimemwons mtume )S>A.W.) akibusu mimi nisingalikubusuu” kiarabu chepesi cha maneno hayojni hivi; inna alamu annakha hajarul atadhura wala tanalwau. Walaula annahu tahiyyatu rasul Allah (S.A.W.) yakabalka makabul atukha.”kitabu kiitwacho vipi uhiji kilichoandikdwa na A-sulelman ukurasa wa 29-30 kuna maneno haya: Hajar-al Aswad (jiwe jeusi) “kabla ya kuanza kuzu\nguka Al-ka’ba ni uzuri kwanza kuliendea hajar-Al Aswad lililoko Al-ka’aba hapo husogea karibi ikiea inayumkinika kikaribia bila ya kuumiza watu unalikabili Hajar-Al Aswad una lieekea mkona na bila ya kusema unalikabili Hajar-Al Aswad unaliweka mkono na bila ya kusema unalibusu mara tatu na kuligusisha kipaji chako cha uso mara tatu kwa wawake kufanya hivi ni suna ikiwa hapana zogo la dwaru, ikiwa hulifikiri liashire kea mkono. Tena mtu hurudi kwenye Hajar-al Aswad na kuligusa, kulibusu mara tatu na kugusisha kipaji cha uso mara tatu kama vile mwanzo tena utasema Allahu Akbaaar mara tatu (huku ukilashiria hajar kea mikono yote miwili ikisha utaongeza “Alla humma iimana bika wartaddika bikitabika wafaa biahdika wattibaa lisunnat nabiyyika salla ila hu Alayhi wassalim.” Kiwsaili. “ewe mola kwa imani yengu juu yako na kuthibitisha kitabu chako na kutekeliza ahadi yako uya kufuata mwendo wa mtume. Tena hapo utapita kulipita Hajar-Al Aswad ukilielikea huku ukiendelea kuzunguka Al-ka’aba yote nzima.kumbuka tendo la kuzunguka Al-ka’aba lilifanya washirikina na dwapagani wa kiarabu zama za ujahilia kabla ya dini ya uislamu kuanza. Na waislamu noo huizunguka Al-ka’aba swali je, waislamu hawakurithi eneo la ibada za ujahilia tafakari.

Mungu wetu yehova anavyotufundisha kuhusu ibada ya jiwe.

Mambo ya walawi 26:1

Msifanye sanamu yeyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jifee lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kilisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana mungu wenu.

Kadiri ya mafundisho ya mungu wet yehova ambaye wakristo tumuabudu ni kakosa makubwa kuchukua jiwe na kulisujudu.Tafakari kuhusu waislamu na matendo yaokatika jiwe la jeusi “Hajarul Aswad.”

(xi) ibada ya kuzunguka majabali (vilimo) vya safaa na marwa huko makka kabla ya uislamu.

Qurani 2:158 suratul Al-Baaraqh (Ng’ombe jike) hakika safaa na marwa (majabali mawili yana yofanyiwa ibada ya kusai huko makka) ni katika alma za kuadhimisha dini ya mwenyezi mungu basi anayehiji kwenyu nyumba hiyo ar kufanya umra. Si kosa kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili na anayefanya wema (atalipwa) kwani mwenyezi mungu ni mwenye shukrani na mjuzi wa kila jambo.

Ufafanuzi wa aya hiii ya 158 ulio katika qurani ni huu katika ibada ambazo hazisihi kufanywa ila makka ni hizi (a) Hijja na (b) umra. Na takriba zote mbili hizi ni sawa sawa ila zinakhitalifiana. Kidogo to. Moja katika hitilafu zao ni kuwa Hijja haifanyi ila miezi makhususi: na mwisho wa miezi ya Hijja ni kumi la mwanzo la mfungo tatu…ama mengine bi sawa. Nayo ni: (1) kuzunguka Al-ka’aba mara 7 (2) kwenda matiti mara 7 baina ya majabali hayo mawili ambalo moja linaitwa safaa na moja linaitwa marwa (3) kunyoa nywele au kuzikata. Majabali hayo kabla ya uislamu yalikuweka yamewekwa juu yake madanamu na makafiri wakiyaabudu. Basi ulipokuja uislamu. Waislamu wengine waliona labda si vizuri kufanya ibada haopo penye majabali hayo. Basi wakaambiwa kuwa si vibaya.

Maelezo ya aya hii yanafanana na yle yaiyo katika saqhih Al-Bukhari volii ukurasa wa 415-416 hadith no. 710 pale Asim alipomuuliza Anas bin maliki (A.S.) hivi: je, ulikuwa ukichukia kufanya tawaf (yaani kuzunguka) kati ya safaa na marwa? Akasema ndiyo kwaqsababu ni matendo ya kwaida (sherehe) iliyofanyofanyika wakati wa ujinga kutajua kabla ya uislamu kuja.Imesimuliwa pia kuwa Muhammad alifanjya tawwaf ya ka’aba na sa’I ya safa na marwa ili kuonyesha nguvu zake kwa safa na marwa. Hayo yamesimuliwa katika sahih Al Bukhari vol ii hadithi no.711. jambo linaloshangaza ni kuwa ibada hiyo ilifanywa na makafiri zama za ujahilia (ujinga) na waislamu nao wazunguka vilima hivyo isitoshe insshangaza kuona Allah mungu anayeabudiwa ba wislamu anayaita majabali hayo minshahilillah yaani alama za mungu au kwa kiingereza “symbols of Allah” hii ni ajabu kuona vilima vinaitwa hivyo.

Bwana yesu anatufundisha nini kuhusu ibada ya milima? Yohana 4:19-22

Yule mwanamke akamwambia bwana naona ya kuwa unabii, baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko yerusalemu ni mahali patupa sapo kuabudjiwa. Yesu akamwambia mama, unisadiki saa ubajyha ambayi gamtamwabudu baba katika mlima huu, wala kule yersalemu, ninyi mnaabudu msichokijua sisu tunaabudu tukijuacho kwa kuwa wokovu watoka kwa wayahudi.

Katika aya hizi Bwana Yesu anatuambia kuwa wale wanaofanya ibada katika mlima hawajui wachokiabudu. Ndugu tafakqari ibada ya waislamu katika vilima je, wanajua wanachokiabudu?

(xii) mwezi wa ramadhani.

Tunaposoma katika kitabu cha maisha ya muhammaf ukurasa wa 32 kilichotungwa na sheikh Farsy tunaona kuwa miezi iliyotumiwa na waarabu kabla yo dini ya uislamu ndiyo inayotumiwa ba waislamu.Kitabu hicho kinasomeka hivi…”Makka tangu kabla ya uislamu, ilikuwa ni mahali patakatifu kwa waarabu wote. Kila mwaka walikuwa wakija kuhiji miezi hii hii wanayoitumia sasa waislamu katika kuhiju kwao.

Waarabu walikuwa washirikina na wapagani majahilia. Walikuwa na mwezi wa ramadhan nalo ndio mwezi ambao dwaislamu wana amini kuwa Muhammad alipata utume. Tazama kitabu cha maisha ya Muhammad ukurasa 16-17.

Ibada ya kufunga katika mwezi wa Ramadhan kwa waislamu

Qurani 2:183 suratul Al-Baarah (Ng’ombe jike)

Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyoiazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu.

Imeelezwa katika sahih Bukhari volii Hadith 662 vol. Iii Hadith no. 219 na 220 pia vol vi Hadith no.31 ya kuwa Muhammad aliamuru waislamu wafunge siku ya Ashura siku ya 10 ya mwezi kwanza katika mwaka wa kiislamu yaani mweziuitwalo muharram) kufunga huko kaqbla ya uislamu ilikuwa ni desturi katika dini ya Hums na uislamu ukaichukua.

(xiii) kumpiga mawe shetani katika bonde la wadah muhassir.

Miongoni mwa tendo moja kubwa linalofanya na waislamu wanapofika hija huko makka ni kumpinga mawe shetani.Kitabu kiitwacho vipi uhiji ukurasa wa54,55,61 kuna maneno haya…”Mahujaji wanapofika bonde liitwalo wadi ah muhasisi karibu na mina ni suna kunyapuka hao huelikea jamrat al a quba (shetani mkubwa) na hupiga yale mawe saba waliyoyaokota muzdelifa baada ya kupiga mawe jamarati Al-Aqaba hufuatiwa na kuchinja.

Kwa sisi wakristo tunajua shetani ni roho ya uasi waefeso 2:1-5 na ni roho ya udanganyifu 1 Timotheo 4:1-2. Hivyo huwezi kumshinda shetani kwa kumpiga kwa mawe maana ni roho tu. Roho ni upepo au pumzi. Biblia inatufundisha kuwa tunamshinda shetani kwa njia ya imani sahihi ya mungu, kushika neon la mungu, dala, na maombi, hivyo tutamshinda shetani soma waefeso 6:11-18.

Wajibu wa Mkristo baada ya kuujua uislamu.

Ninaamini kuwa imejifunza mengi kuhusu dini ya uislamu, na umeona mambo mengi yuanayotendeka na waislamu kule makka wakati wa hija. Mambo hayo yalifanywa na makureshi na waarabu wenzao kabla ya dini ya uislamu kuja, na tena umeona kuwa mungu tunayemwabudu wakristo hataki ibada zinazoshirikisha mawe na milima.Basi wajibu wako mkristo kuwafikishia injili waislamu na watu wa dini nyingine zisizomuamini Bwana Yesu, ili wamdwamini na wapate kuokolewa.Kumbuka injili ndio uweza wa mungu uletao wokovu Warumi 1:16. na tena injili ndilo neon la kweli Wakolosai 1:5. bwana akubariki sana ni mimi katika utumishi wa Bwana Yesu Mwalimu;

Eleutary H. Kobelo.

mwalimu at 12:12 AM

Share

 

AnonymousOctober 15, 2013 at 6:28 AM

Ukiangalia kwa makini utagundua vitu vifuatavyo;1.Yesu katika Yohana 16:2-4,inatueleza wazi sisi wakristo kuwa siku zinakuja (ambazo ndizo za ujio wa mtume wa waislam),kuwa watadhani wanapo tuua wanamtolea Mungu ibada kumbe ni kazi za shetani ndizo wanazifanya 2;Mungu wa kweli hafurahii kumwagwa kwa dmu zisizo na hatia lakini allah hufurahia hizo na kuwahimiza wafuasi wake kuua wale wasiowaislam eti ndo baraka kama si ushetani ninini na ndio maana mamia ya wanaojua ukweli wanamkimbilia YESU mwana wa MUNGU ,masheikh kwa waumini kwa kuwa wamejua wamedanganywa pakubwa sana na ni njia wazi kwenda jehanamu.

Reply

kufJanuary 2, 2014 at 1:24 AM

amen

Reply

AnonymousFebruary 28, 2014 at 3:33 AM

Dah! Kweli sheikh tani kakamata ndugu zetu waislamu. Mwenyezi Mungu mwenye huruma awanusuru katika jina la Yesu. Amen

Reply

AnonymousJuly 30, 2014 at 11:53 PM

Allah atuepushe na upotoshi wa makafiri hawa. amin

Reply

AnonymousAugust 18, 2014 at 6:28 AM

Jee mnadhani watakuwa sawa wenye kujua na wasiojua? enyi ndugu zangu ktk imaani yatupasa tusome uislamu ili tuepukane na upotoshaji wa makafiri hawa wa kikristo.

Reply

AnonymousAugust 18, 2014 at 6:30 AM

Watafanya kila hila na kuupa uislamu majina yote mabaya lakini kamwe hawataweza kuizima nuru ya Allah nayo ni uislamu, na waislamu wote wataingia peponi ila atakae kataa.

Reply

AnonymousAugust 18, 2014 at 6:32 AM

Kafiri kamwe haogopi kusema uongo maana kwao uono ni kama ibada

Reply

AnonymousMarch 29, 2015 at 8:41 PM

Tatizo wenzenu waislam wanaijua dini yenu wameisoma. Nyie maamuma badala msome mjue uislam ni nini. Mnasikiliza hadithi za uongo. Huyo aliye waandikieni sijui kavumbua wapi hizo story. Mtu akitokea anajidai kuandika porojo zake mnamuunga mkono. Someni mue na uhakika .hapo nduo waislam hamuwawezu kika siku wanawashindeni .hamuwezi kusimama nao kujadili kitu. Wenzenu wanaijua dini yenu kinyumenyume. Nyie mko vilabuni mnakunywa. Yeyote ambae anajifanya anajua dini aseme. Aje mbele yetu kama hata adhirika. Someni kwanza sio maropoka makafir nyie

Reply

FAUZ KHAMISSeptember 27, 2016 at 1:12 PM

Hamna kitu hapo. Kila kilichopo duniani ni alama ya kuepo M/Mungu. Kama huamini hivyo au imani yako haikuambiihivyo utakua huna dini or dini yako sio sahihi. Kwa sababu hakuna Muumba mwengine asiekua Mungu. Sasa kama vilima si sign ya Mungu,ni saini ya nn?

Reply

Links to this post

Create a Link

Home

View web version

About Me

injili timilifuInjili Timilifu (Full Gospel) is a young non-denominational ministry at the Kenyan Coast based in Mombasa that is focused to reach out to Muslims through various channels and strategies. We run on Christian principles. Our primary objective is to carry out evangelism, discipleship and training, in word and deed especially along the coastal strip of Kenya. We have a long way to go before we can say we are settled. We certainly are faced with a steep curve of learning in ministry Development and Outreach to Muslims. We desire to growth within us qualitatively and quantitatively and more so growth in the Christian love for Muslims.View my complete profile

Powered by Blogger.