ASIKUCHOSHE NA MANENO YAKE YA SHOMBO ANGEKUA NA UWEZO WA HAO WAZURI ASINGEKUFUATA WEWE!
Akikuambia sijui kwanini nilioa mwanamke kama wewe tabasamu na muambie ni kwakua hukua na uwezo wa kupata mwingine bora zaidi yangu hivyo si kwamba wewe umenizidi chochote bali nikwakua tunaendana! Hata kama huna ujasiri wa kumuambia hivyo lakini jiambie wewe mwenyewe, jiambie ukijua kua kama angekua ni bora kuliko wewe kama anavyojinadi kila mara basi angeoa hao anaowaona kama ni bora kuliko wewe.
Ukiona mwanaume kila mara mnapogombana maneno yake ndiyo hayo basi jua kuwa tatizo si wewe bali tatizo ni yeye, hajiamini ndiyo maana analazimika kukushusha ili ahisi kama vile mko sawa. Acha kushuka na kuwa kama yeye, acha kuumia na kujiona kama takataka mbele yake kwani ukweli nikua mpaka anakuja kukutongoza au mpaka anakubali kuwa na wewe basi alikupenda au wewe ni wa aina yake. Kama usingekua wa aina yake usingemvutia na asingekufuata!
Asikuchoshe na maneno yake ya shombo kwani kama angekua na uwezo wa hao anaowaona ni wazuri mbona angewafuata wao lakini hakua nao na akabaki na wewe! Mwisho kumbuka kuwa jinsi ulivyo ndivyo ambavyo Mungu alitaka uwe hivyo, angetaka kukuumba kivingine angefanya hivyo na alikua na uwezo huo lakini hapana, aliamua uwe hivyo na huna sababu ya kujichukia na kujiona takataka kisa tu una mwanaume ambaye hajiamini!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni