Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 12 Desemba 2016

UEFA : Arsenal wapewa Bayern Munich , Leicester

UEFA: Arsenal wapewa Bayern Munich, Droo kamili ipo hapa
KAMGISHA BLOG / 5 hours ago

Arsenal wamepangwa kucheza na Bayern Munich, Leicester City watakutana na Sevilla nao Manchester City wakabiliane na Monaco katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Gunners wamecheza dhidi ya mabingwa hao wa Ujerumani mara nne katika misimu mitano iliyopita.
Walimaliza wa pili nyuma ya Bayern katika hatua ya makundi msimu uliopita.

Leicester City, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England, wana kibarua dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi ndogo ya Ulaya, Europa League Sevilla ya Uhispania.

Wapinzani wa Manchester City Monaco walilaza Tottenham mara mbili katika Kundi E.

Droo kamili:

Manchester City (Uingereza) v Monaco (Ufaransa)

Real Madrid (Uhispania) v Napoli (Italia)

Benfica (Ureno) v Dortmund (GER)

Bayern (Ujerumani) v Arsenal (Uingereza)

Porto (Ureno) v Juventus (ITA)

Leverkusen (Ujerumani) v Atlético (Uhispania)

Paris (Ufaransa) v Barcelona (Uhispania)

Sevilla (Uhispania) v Leicester (Uingereza)

Jumapili, 11 Desemba 2016

Maswali Muhimu Ya Kujiuliza Leo Katika Maisha Yako

Maswali Muhimu Ya Kujiuliza Leo Katika Maisha Yako
KAMGISHA BLOG / 9 hours ago

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa uko salama na unaendelea vizuri katika maisha yako. Kama uko katika changamoto au wakati mgumu katika maisha yako pole sana endelea kukabiliana nayo na ujue ya kwamba hakuna hali ya kudumu katika maisha yako vumilia tu hilo nalo litapita na utarudia katika hali yako ya kawaida.

Tunamshukuru Mungu pia kwa zawadi ya siku hii ya leo kwa kunistahilisha kuandika makala hii na kukustahilisha wewe kuweza kuwa msomaji wangu kupitia mtandao huu.

Nashukuru sana rafiki yangu kwa kuendelea kuwa pamoja na mimi kupitia mtandao huu hivyo basi, napenda kutumia fursa hii kukualika tena katika makala yetu ya leo.

Katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza maswali muhimu ya kujiuliza leo katika maisha yako. Je ni maswali gani? Karibu mpenzi msomaji tuweze kusafiri kwa pamoja mpaka mwisho wa makala hii ili uweze kujua yale mazuri niliyokuandalia siku hii ya leo. Mwandishi na mwana falsafa jim rohn aliwahi kusema ‘’ if you want to change your result, you have to change your thinking first’’ akiwa na maana ya kwamba kama unataka kubadilisha matokeo yako, unatakiwa kwanza kubadilisha mtazamo wako wa kufikiri. Hivyo basi kama unataka kubadilisha kitu chochote katika maisha yako unatakiwa kubadilisha kwanza namna unavyofikiria mambo.

Mpendwa rafiki, tumia muda wako leo mchache na jiulize maswali yafuatayo katika maisha yako.

1. Hali ya afya yako ikoje kwa sasa? 
Afya yako ndio utajiri namba moja duniani utakaokuwezesha kutimiza malengo yako yote uliyojiwekea hapa duniani. Unakula vizuri vyakula vya kujenga mwili na kuupa mwili kinga dhidi ya magonjwa? Unafanya mazoezi ya mwili? Unapunguza uzito? Unakunywa maji mengi? Unakula matunda? Au unakula vyakula vyepesi vya kuharibu mwili wako kama vile chips na vinywaji kama vile soda.

2. Mtazamo wako juu ya maisha yako ukoje kila siku? 
Maisha yako unayachuliaje je katika mtazamo chanya au hasi. Maisha yako yametawaliwa na furaha au huzuni? Maisha ni furaha na una uamuzi wa kuchagua kuishi kwa furaha au huzuni bila kujali matatizo uliyokuwa nayo. Kama unaishi maisha yako katika mtazamo chanya ni rahisi kuishi katika furaha na mafanikio lakini ukiishi katika mtazamo hasi lazima utaona maisha ni huzuni badala ya furaha na utakuwa mlalamikaji na mtu wa kulaumu.

3. Mahusiano yako kiujumla katika idara hizi zifuatazo yako? 
i. Mahusiano yako na familia yako ya koje? Mara ya mwisho ni lini ulimwambia au uliwaambia watoto wako kuwa unawapenda au nakupenda? Mara ya mwisho ni lini uliwakumbatia na kuwabusu watoto wako? Watoto wanahitaji upendo na kuhisi kuthaminiwa je watoto wako au katika familia yako wanaonja falsafa ya tunda la upendo? Au umeshakufa siku nyingi katika mioyo ya watoto wako wanakusubiri tu wakuzike? Unapata muda wa kukaa na familia yako?

ii. Mahusiano yako na mpenzi au mwenza wako yakoje? Falsafa ya upendo ipo? Uaminifu, kuvumiliana, furaha , amani ipo katika mahusiano yenu? Kama ipo au hakuna unachukua hatua gani kurekebisha hiyo hali? Vuta picha ya nyuma mlivyokutana wakati mko katika uchumba jinsi ulivyokuwa unaonesha upendo na kujali ni sawa na sasa? Kama siyo nani ni kiini cha kosa na umechukua hatua gani baada ya kujua kama wewe au yeye ndio kiini cha kosa kinachowafanya mwendelee kuishi maisha ambayo hayastahili kuishi kama wapenzi?

iii. Mahusiano yako ya koje na marafiki wako, ndugu, jamaa na jirani zako? Umekuwa ni faraja au kikwazo kwa watu hawa wa karibu kwako? Marafiki zako na watu waliokuzunguka wananufaikaje na wewe, wanajifunza nini kutoka kwako au wewe ndio umegeuka kuwa adui wa kurusha makombora ya kusengenya, umbea, wivu, chuki na kutokusamehe na kulipa visasi? Jitafakari leo na uchukue hatua chanya.

4. Ni kwa namna gani unailisha akili yako chakula? 
Unatakiwa kuilisha chakula akili yako na chakula cha akili au ubongo wako ni maarifa na siyo kitu kingine. Jiulize katika taaluma uliyosomea umeshasoma vitabu vingapi vya kuongeza maarifa tofauti tofauti na vitabu vya darasani yaani ambavyo haviko katika mtaala wa darasani? Tokea umalize shule au chuo ni mara ngapi umesoma kitabu kwa ajili ya kuona akili yako? Ni mara ngapi unasoma makala chanya za kujenga na kusikiliza sauti zilizorekodiwa za watu makini duniani? Au wewe ndio unakomaa na kufuatilia udaku katika magazeti, mitandao ya kijamii kujua Fulani kafanya nini na mengine mengi je unafikiri hiyo ndio njia ya kuongeza maarifa kwa fuatilia udaku? Soma vitabu rafiki na jifunze kwa watu utalisha ubongo wako maarifa mapya kila siku.

5 .Maisha yako yana msaada kwa watu wengine? 
Unaishi maisha ya kushawishi watu au unaishi maisha ya kugeuka kuwa mwalimu mzuri wa kukosoa na kukatisha tamaa watu au unaishi maisha ya kuwaaminisha watu kuwa mambo yanawezekana kama mtu akiamua kuchukua hatua. Jiulize swali hili leo.

6. Malengo yako uliyojiwekea mwaka huu au wiki hii umefanikiwa kiasi gani?
Jiulize maswali muhimu yote uliyojiwekea kuhusu malengo yako na halafu utachukua hatua je umefanikiwa kiasi gani? Kama unaishi bila malengo basi wewe ni mtu ambaye huna mwelekeo na mwelekeo wowote utakuchukua katika maisha yako kama hujajiwekea malengo.

7. Maisha yako ya kiroho yakoje? 
Hapa angalia katika imani yako angalia mahusiano yako na Mungu wako yakoje? Imani yako ikoje imekua au imelala na kumbuka kuwa imani ni zawadi kutoka kwa Mungu huwezi kuishika wala kuiona.

8. Unatumiaje zawadi ya muda uliyopewa bure? 
Muda ni mojawapo ya zawadi ya kipekee sana tuliyopewa bure. Je unautumiaje muda wako? Mwanafalsafa na mwandishi Seneca aliwahi kusema ‘’ life, if well lived, is long enough’’ akiwa na maana ya kwamba maisha ni marefu kama ukiishi vizuri au ukitumia muda wako vizuri hapa duniani. Je unatumiaje muda wako ili kuacha alama hapa duniani? Jiulize swali hili muhimu sana katika maisha yako. Tumia muda wako vizuri na muda ndio maisha yako rafiki. Tumia muda wako kuacha alama ya wewe kuendelea kuishi hata kama hutokuwepo duniani.

Hatua ya kuchukua leo, kaa chini na tenga muda wako halafu jiulize maswali yote muhimu katika maisha yako na chukua hatua chanya mara moja leo.

Mwisho, somo letu la leo lilitualika kuweza kujiuliza maswali muhimu katika maisha yetu ili tuweze kupata matokeo tofauti. Ili tubadilishe maisha yetu ni lazima kwanza tubadilishe namna ya kufikiri kwanza na njia nzuri ya kufikiri ni pamoja na kujiuliza maswali muhimu na makini kwenye maisha yako. Nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyoweza kujifunza leo. 

Mambo 6 ya kuzingatia katika mahusiano ya kimapenzi

Mambo 6 Yakuzingatia Katika Mahusiano Ya Kimapenzi
MUUNGWANA BLOG / 9 hours ago

Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu.  Wanawake wengi wanalalamika kuwa  hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.

Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika,  muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala.

Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.

Njia za kukusaidia

1. kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote.  Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu.  Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea.  Kama utaanza kujizoeza  hivi ukiwa nyumbani, taratibu  utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.

2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake.  Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo.  Onyesha heshima katika vitu hivyo pia.  Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu.  Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.  Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo.  Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua  na sisi pia.

3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote.  Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.  Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili.   Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au dhambi?

Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.

Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa  tendo la ndoa katika  mahusiano yenu.

4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano.  Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao.  Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu.  Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu.  Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu.  Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.

5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu.  Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia.  Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu.  Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu.  Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.

6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko.  Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano  wetu lazima ume halisi na sio feki.  Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi.  Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu.  Ukianza kupata  ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe kuvitafuta vile vyote  mpenzi wako alivyonavyo ambavyo  hukuza ukaribu wenu.  Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi

Mambo ya kuzingatia kabla ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi
KAMGISHA BLOG / 5 hours ago

Mapenzi ni moja ya mahitaji muhimu ya wanadamu, kila mmoja wetu ahahitaji kupenda na kupendwa, hapo hamna majadiliano ndio jinsi tulivyoumbwa. Katika enzi za mababu zetu, watu walikuwa wanaishi kwa raha, amani na upendo japokuwa walikuwa wanachagulia wake au waume wa kuishi pamoja kama mke na mume, enzi hizo zimepitwa na wakati siku hizi watu wanajitafutia wenza wao wenyewe, ila siku hizi watu ndio hawana amani, ndoa zinavunjika kila siku na wanaobakia kuteseka zaidi ni watoto ambao wanaishia kuishi bila mama na baba.

Ukweli ni kwamba inachukua muda mrefu kumfahamu mtu vizuri, kikubwa zaidi watu wanabadilika jinsi wanavyokuwa, hela zinaongezeka au kupungua na wanajikuta wanavutiwa na watu wa aina tofauti. Kwa wale ambao hawajabahatika kupata wenza wao kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kabla hujajizamisha katika dimbwi la mapenzi, ukizingatia mambo haya, hata kama mtu uliyenaye atabadilika , uwezekano wa kuvumiliana na kuweza kuishi pamoja ni mkubwa zaidi.

1. ni lengo (ambition),
kama mmoja kati wa wapenzi (nazungumzia wapenzi ambao wanampango wa kuishi pamoja kama mke na mume) ni mtu wa kuwa na malengo na anataka kufanya kitu fulani au kuwa mtu fulani katika maisha yake na mwenzake anachukulia siku kama inavyokuja (laid back), huyu ambaye ana malengo atamchukulia ambaye ni “laid back” kama ni mvivu. Wapenzi wanatakiwa wasipishane sana katika malengo yao hata kama wana kazi mbali mbali.

2. ni uwazi (openness), 
kama mpenzi wako ni “open minded” anapenda kujifunza vitu tofauti, kujaribu vyakula tofauti, kusafiri n.k. Yule ambaye anapenda kujifunza mambo mapya kila siku atamuona mwenzake anaboa.

3. wapenzi wanaweza kuwa tofauti katika ujuzi wa hisia (emotional intelligence). 
Hapa kama tofauti sio kubwa, watu wanaweza kuvumiliana na kuishi pamoja, ila kama tofauti ni kubwa sana, yule ambaye hana ujuzi wa hisia, atakuwa anamburuza na kumharibia mudi yule ambaye amesimama imara kwenye mambo ya hisia. Onyo kwa wanaume ambao wana ujuzi au utaalam wa kusoma hisia za wanawake, wanawake ambao wana F katika ujuzi wa hisia huwa wanavutiwa sana na watu kama ninyi.

4.  ni usosho,
kama mmoja wenu ni mtu wa watu anapenda kuongea na watu na anamarafiki kibao, utamkwaza ambae ni mtu ambaye anapenda maisha “private” na ya utulivu. Mwenzako atakuwa bize anaweka picha zenu na status zinazowahusu facebook wakati wewe unataka mambo ya ndani yawe ya ndani tu. Kama tofauti si kubwa sana mnaweza vumiliana kama tofauti ni kubwa, muda si mrefu mtashindwana

5.  ni wivu.
Wivu ni kitu kibaya sana, kama mpenzi mmoja ana wivu ni ngumu kuekewana na ambaye hana wivu. Kama wote mna wivu, sawa kwani kila mmoja ataepuka kufanya mambo ambayo yanamuumiza mwenzake, ila kama mmoja ndio ana wivu ataona mwenzake hajali, basi ukimuona mwenzako anaongea na classmate wake wa zamani au ukiona mtu amepiga picha na mpenzi wako ameshikwa bega basi inakuwa fujo tupu. Kama upo tayari kwenye uhusiano, na mwenzako ana wivu, jaribu kumuelewesha kwamba kum-kumbatia rafiki yako sio kwamba ndio una mipango mingine ya siri.

Kikubwa katika yote ni uaminifu, kama hamna uaminifu katika mapenzi au ndoa. Usipasue kichwa, ondoka na tafuta mtu ambaye anakuamini au kama haupo tayari kuwa mwaminifu usijiingize katika mahusiano, utajiumiza mwenyewe na mwenzako. Msome mwenzako kabla ya kuanza kuitana wachumba, kama tangu siku ya kwanza mwenzako ana wasiwasi na wewe ukikaribia simu yake, ni afadhali umuulize mapema, kulikoni? Kama umepoteza uaminifu katika mahusiano yako, usihofu, muonyeshe mweza wako kwamba umebadilika na jinsi muda unavyoenda atajifunza kukuamini tena.

Hizi sifa zilizotajwa hapo juu sio za kina sana, lakini ni moja wapo ya mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenza wako wa maisha(kama basi mapenzi yana macho) kabla ya kujizamisha katika mapenzi. Je wewe unaona ni mambo gani ya kuzingatia katika mahusiano na ni mambo gani yanasababisha ndoa kuvunjika? Usisite kuandika maoni yako.

Jumamosi, 10 Desemba 2016

SIFA 10 ZA MTU MWENYE MAPENZI YA KWELI KWAKO

Sifa 10 za mtu mwenye mapenzi ya kweli kwako
Kamgisha blogg/ 4 hours ago

Vijana wengi ambao wanapendana leo mapenzi yao hayadumu kiasi cha kubatizwa jina la utamu wa bazoka. Lakini yote hii inatokana na ukweli kwamba elimu ya mapenzi ambayo ni muhimu kwa binadamu haitolewi ipasavyo.

Ipo zana potofu kwamba kumfundisha mtoto mapenzi ni kumharibu, jambo ambalo si kweli bali inategemea mtoto huyo anafundishwa nini na kwa wakati gani. Lakini cha kushangaza zaidi hata watu wazima ambao ni wadau wa mapenzi hawayajui, matokeo yake wanajiingiza kwenye uhusiano wakiwa bumbumbu na hivyo kuteshwa na changamoto zinazowakabili.
Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu. Sifa hizo ni hizi zifuatazo.

1.Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.

2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .

3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri

4.Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.

5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha maisha yako, atakulinda daima.

6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)

7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine, hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.

8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.

9.Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .

10.Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.

Jumatano, 7 Desemba 2016

AINA YA MWANAMKE AMBAO WATU FANYA MAISHA YAKO KUWA MAGUMU

Aina ya Wanawake Ambao Watafanya Maisha Yako Kuwa Magumu.
Editor 2 hours ago

Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo hazifurahishi. Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.
Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mwanamke anayekuganda nguoni

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.

2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi

Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.
Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani…nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?

3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

4. Mwanamke asieomba msamaha

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

5. Mlalamishi

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

6. Asiyejielewa

Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

7. Anayetawala na kutotosheka

Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote

Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

9. Nusa Nusa

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

10. Asiye na maono

Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

11. Mcheza ndondi

Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

12. Mtoto wa mama

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hii ni baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanamume yeyote anafaa kuwa chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu kutatua.

Kusoma Maujanja Zaidi Kuhusu Mapenzi Download App yetu Bofya Hapa
VISIT WEBPAGE

Kwa nini mwili wangu unabadilika


yp2 sura 6 kur. 58-66
Sura ya 6
Kwa Nini Mwili Wangu Unabadilika?
“Nilirefuka haraka sana. Nilikuwa na maumivu mengi. Ingawa nilipenda kuwa mrefu, nilikuwa na maumivu ya miguu. Hilo halikunifurahisha hata kidogo!”—Paul.

“Unajua kwamba mwili wako unabadilika, hata hivyo hungependa yeyote atambue. Kisha, mtu fulani anakuambia kwamba una kiuno cha mwanamke aliyekomaa—unatamani dunia ipasuke na kukumeza!”—Chanelle.

UMEWAHI kuhamia eneo lingine pamoja na familia yenu? Yalikuwa mabadiliko makubwa, sivyo? Uliacha kila kitu ulichokuwa umezoea—nyumba yenu, shule yenu, na marafiki wako. Yaelekea ilikuchukua muda mrefu kuzoea mazingira yako mapya.

Mwanzoni mwa kipindi cha kubalehe—wakati ambapo mwili wako unaanza kukomaa—unaingia katika kipindi cha baadhi ya mabadiliko makubwa zaidi maishani. Ni kana kwamba unahamia “eneo” jipya. Bila shaka ni jambo lenye kusisimua! Lakini kuingia katika kipindi cha utu uzima kwaweza kukutatanisha na huenda isiwe rahisi kwako kuzoea hali hiyo. Ni nini kinachotukia katika kipindi hicho kigumu maishani?

Mabadiliko ya Wasichana

Kipindi cha kubalehe ni wakati wa mabadiliko makubwa. Mabadiliko mengine yataonekana wazi. Kwa mfano, homoni zitasababisha nywele ziote kwenye maeneo ya viungo vyako vya uzazi. Pia, matiti, kiuno, mapaja, na makalio yatakuwa makubwa. Mwili wako utaanza kubadilika na kuchukua umbo la mwanamke mkomavu. Usiwe na wasiwasi. Hupaswi kushangazwa—mabadiliko hayo ni mambo ya kawaida kabisa. Na yanaonyesha kwamba mwili wako unajitayarisha kwa ajili ya wakati ambapo utaweza kupata mtoto!

Muda fulani baada ya kuanza kubalehe, utaanza kupata hedhi. Usipojitayarisha vya kutosha, badiliko hilo kubwa maishani mwako linaweza kuogopesha. “Nilipoanza kupata hedhi, sikuwa tayari hata kidogo,” asema Samantha. “Nilijiona kuwa mchafu. Nilikuwa nikijisugua sana nilipokuwa nikioga. Nilijiona kuwa ‘mwenye kuchukiza sana.’ Niliogopa sana nilipofikiria kwamba kwa miaka mingi nitakuwa nikipata hedhi kila mwezi!”

Hata hivyo, kumbuka kwamba kupata hedhi kunaonyesha kwamba nguvu zako za uzazi zinakua. Ijapokuwa miaka mingi itapita kabla hujawa mzazi, unaendelea kukomaa na kuwa mwanamke. Vyovyote vile, kuanza kupata hedhi kunaweza kuwa jambo la kuhangaisha. “Jambo kubwa zaidi nililolazimika kukabili ni kubadilika-badilika kwa hisia,” asema Kelli. “Nilifadhaika sana kwa kuwa sikujua kwa nini ningeweza kuwa na furaha mchana kutwa, na kulia kwelikweli usiku wa siku hiyohiyo.”

Ikiwa hivyo ndivyo unavyohisi sasa, uwe na subira. Baada ya muda utazoea. Annette, mwenye umri wa miaka 20, anasema: “Nakumbuka wakati nilipofikia hatua ya kukubali kwamba ili niwe mwanamke mkomavu mabadiliko hayo lazima yatokee na kwamba Yehova amenipa zawadi ya uzazi. Inachukua muda kukubali jambo hilo, na inakuwa vigumu sana kwa wasichana fulani; lakini baada ya muda unajifunza kukubali mabadiliko hayo.”

Je, umeanza kujionea yoyote kati ya mabadiliko hayo ambayo yamezungumziwa? Katika nafasi zilizo hapa chini, andika maswali yoyote uliyo nayo kuhusu mabadiliko yanayokupata.

․․․․․
Mabadiliko ya Wavulana

Ikiwa wewe ni mvulana, kipindi cha kubalehe kitabadili sana sura yako. Kwa mfano, huenda mara nyingi ngozi yako ikawa na mafuta mengi na kutokeza chunusi.* “Inafadhaisha na kuvunja moyo sana kuwa na chunusi,” asema Matt mwenye umri wa miaka 18. “Unahitaji kupigana vita vikali na chunusi hizo. Huwezi kujua ikiwa zitakwisha au zitaacha makovu au ikiwa watu watakudharau kwa sababu una chunusi.”

Kwa upande mwingine, huenda ukaona kwamba unazidi kuwa mkubwa na mwenye nguvu na kwamba mabega yako yanaanza kupanuka. Pia, wakati wa kubalehe, nywele zinaweza kuota kwenye miguu, kifua, na uso wako, na pia kwenye makwapa yako. Hata hivyo, kumbuka kwamba kuwa na nywele nyingi hakumaanishi kwamba wewe ni dume sasa; hilo ni jambo linalotegemea urithi tu.

Kwa kuwa sehemu mbalimbali za mwili wako hukua kwa viwango tofauti, unaweza kuhisi kwamba sura yako haipendezi. Dwayne anasema hivi kuhusu wakati alipobalehe: “Nilionekana kama ngamia mwenye miguu ya twiga. Ilionekana kana kwamba ujumbe kutoka kwenye ubongo wangu ungechukua juma moja kabla ya kufika kwenye miguu!”

Katika miaka ya katikati ya utineja sauti yako inakuwa nzito zaidi hatua kwa hatua. Kwa muda fulani, sauti nzito inaweza kukatizwa-katizwa na sauti nyembamba na kali, jambo ambalo linaweza kukufanya uaibike. Hata hivyo, usijali. Baada ya muda, sauti yako itasawazika. Kwa sasa, kujifunza kutohangaishwa na hali hiyo kutakupunguzia aibu.

Mfumo wako wa uzazi unapozidi kukomaa, viungo vyako vya uzazi vitakuwa vikubwa na nywele zitaota kandokando. Pia vitaanza kutokeza umajimaji unaoitwa shahawa. Umajimaji huo huwa na mamilioni ya mbegu za uzazi zisizoweza kuonekana kwa macho, ambazo hupitishwa wakati wa ngono. Mbegu moja inaweza kutungisha mimba yai la mwanamke na kutokeza mtoto.

Umajimaji huo unapoongezeka mwilini, kiasi fulani hufyonzwa mwilini, lakini mara kwa mara, mwingine unatoka usiku unapolala. Hilo ni jambo la kawaida. Hata Biblia hulizungumzia. (Mambo ya Walawi 15:16, 17) Jambo hilo linaonyesha kwamba mfumo wako wa uzazi unafanya kazi na kwamba unaelekea kuwa mwanamume mkomavu.

Je, umeanza kujionea yoyote kati ya mabadiliko hayo ambayo yamezungumziwa? Katika nafasi zilizo hapa chini, andika maswali yoyote uliyo nayo kuhusu mabadiliko yanayokupata.

․․․․․
Kushughulika na Mabadiliko ya Kihisia

Mfumo wa uzazi unapoendelea kukomaa, wavulana na wasichana huanza kuvutiwa na watu wa jinsia tofauti. “Nilipoingia kipindi cha kubalehe, ghafula nilianza kuona wasichana wengi kuwa warembo,” anasema Matt. “Lilikuwa jambo lenye kuvunja moyo sana, kwa kuwa singeweza kufanya lolote mpaka wakati ambapo ningekuwa na umri mkubwa zaidi.” Sura ya 29 ya kitabu hiki itazungumzia zaidi hali hiyo. Hata hivyo, kwa sasa unapaswa kutambua kwamba unahitaji kujifunza kuzuia tamaa zako za ngono. (Wakolosai 3:5) Amini usiamini, unaweza kuamua kutozitosheleza!

Kuna hisia nyingine pia ambazo hutokea katika kipindi cha kubalehe. Kwa mfano, huenda ukajiona kuwa mtu asiyefaa kitu. Vijana wengi huwa wapweke na kushuka moyo mara kwa mara. Pindi hizo, ni vizuri kuzungumza na mzazi au mtu mwingine mzima unayemwamini. Andika jina la mtu mzima ambaye wewe unaweza kuzungumza naye kuhusu hisia zako.

․․․․․
Ukuzi wa Maana Zaidi

Ukuzi wa maana zaidi si wa kimo, umbo, wala sura yako, bali utu wako, yaani, ukuzi wa kiakili, kihisia na, zaidi ya yote, wa kiroho. Mtume Paulo alisema hivi: “Nilipokuwa mtoto, nilikuwa nikisema kama mtoto, nikifikiri kama mtoto, nikiwaza kama mtoto; lakini kwa kuwa sasa nimekuwa mtu mzima, nimeziondolea mbali tabia za mtoto.” (1 Wakorintho 13:11) Ndiyo, haitoshi tu kuonekana kama mtu mzima. Lazima ujifunze kutenda, kuzungumza, na kufikiri kama mtu mzima. Usijihangaishe sana na mabadiliko ya mwili hivi kwamba umpuuze yule mtu wa ndani!

Pia, kumbuka kwamba Mungu “huona jinsi moyo ulivyo.” (1 Samweli 16:7) Biblia inasema kwamba Mfalme Sauli alikuwa mrefu na mwenye sura nzuri, lakini hakupata mafanikio akiwa mfalme wala maishani. (1 Samweli 9:2) Tofauti naye, Zakayo alikuwa “mfupi,” hata hivyo alikuwa na ujasiri wa kubadili maisha yake na kuwa mwanafunzi wa Yesu. (Luka 19:2-10) Ni wazi kwamba jinsi mtu alivyo kwa ndani ndilo jambo la maana.

Ukweli ni kwamba: Hakuna njia yoyote salama ya kuharakisha au kukawiza jinsi mwili unavyokua. Kwa hiyo, badala ya kuchukia na kuogopa mabadiliko hayo, jipe moyo na usihangaishwe na mambo kupita kiasi. Kubalehe si ugonjwa, wala wewe si mtu wa kwanza kubalehe. Uwe na hakika kabisa kwamba maisha yako hayako hatarini hata kidogo. Dhoruba ya kubalehe itakapokuwa imepita, utaibuka ukiwa mtu mzima aliyekomaa!

KATIKA SURA INAYOFUATA

Namna gani ikiwa hufurahishwi na kile unachoona unajipotazama kwenye kioo? Unaweza kufanya nini ili uwe na maoni yanayofaa kuhusu sura yako?

[Maelezo ya Chini]

Wasichana pia hupata chunusi. Tatizo hilo linaweza kupunguzwa kwa kutunza ngozi ifaavyo.

MAANDIKO MUHIMU

“Nitakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa njia ya ajabu yenye kuogopesha.”—Zaburi 139:14.

PENDEKEZO

Mwili wako unapoanza kukua, epuka kuvalia mavazi yanayochochea hamu ya ngono. Sikuzote, valia kwa “kiasi na utimamu wa akili.”—1 Timotheo 2:9.

JE, WAJUA . . . ?

Kipindi cha kubalehe chaweza kuanza mapema sana, kuanzia umri wa miaka minane hivi, au kinaweza kuchelewa na kuanza mtu anapokuwa katika miaka ya katikati ya utineja. Hata mtu aanze kubalehe wakati gani, haimaanishi kwamba ana kasoro.

HATUA ZA KUCHUKUA!

Ninapozidi kukomaa na kuwa mtu mzima, sifa ninayohitaji kufanyia kazi sana ni ․․․․․

Ili kukua kiroho, nita ․․․․․

Mambo ambayo ningependa kuuliza mzazi (wazazi) wangu kuhusu habari hii ni ․․․․․

UNA MAONI GANI?

● Kwa nini ni vigumu sana kushughulika na mabadiliko ya kimwili na ya kihisia wakati wa kipindi cha kubalehe?
● Ni nini unachoona kuwa kigumu sana katika mabadiliko hayo?
● Kwa nini huenda upendo wako kwa Mungu ukaelekea kupungua katika kipindi cha kubalehe, lakini unaweza kuzuia jinsi gani jambo hilo lisitokee?
[Blabu katika ukurasa wa 61]

Kuna hali nyingi zenye kutia wasiwasi katika kipindi cha kubalehe, na huenda usijue jinsi mwili wako utakavyokuwa siku inayofuata. Lakini kadiri unavyokua, unajifunza kukubali mabadiliko hayo na hata kuyafurahia.’’—Annette

[Sanduku katika ukurasa wa 63, 64]

Ninaweza Kuzungumza Namna Gani na Baba Yangu au Mama Yangu Kuhusu Ngono?

“Nikiwa na swali lolote kuhusu ngono, siwezi kamwe kuwauliza wazazi wangu.”—Beth.

“Siwezi hata kupata ujasiri wa kutaja mambo hayo.”—Dennis.

Ikiwa uko kama Beth au Dennis, uko katika hali ngumu sana. Ungependa kujua kuhusu ngono, lakini watu walio na majibu ndio watu ambao hungependa kuwauliza—wazazi wako! Una maswali mengi yanayokuhangaisha:

Wataniona namna gani?

“Sitaki waanze kunishuku kwa sababu ya kuuliza.”—Jessica.

“Wanataka uendelee kuwa mtoto asiyejua chochote milele, na siku utakapoanza kuzungumza nao kuhusu ngono, mambo kwisha.”—Beth.

Watafikiri nini?

“Naogopa kwamba wazazi wangu watanihukumu na kuanza kunigombeza hata kabla sijamaliza kuzungumza.”—Gloria.

“Wazazi wangu hawajui kuficha hisia zao, kwa hiyo, naogopa kwamba sura zao zitaonyesha kwamba wamevunjika moyo. Kwanza, huenda hata baba yangu akaanza kufikiria jinsi ya kunigombeza huku nikiendelea kuzungumza.”—Pam.

Je, watakosa kunielewa?

“Huenda wakakasirika na kuanza kuuliza maswali kama vile, ‘Kuna mtu anayekushawishi mfanye ngono?’ au ‘Rafiki zako wanakushinikiza?’ Lakini huenda tu unataka kujua.”—Lisa.

“Kila mara nikitaja tu mvulana yeyote, baba yangu huingiwa na wasiwasi. Kisha anaanza kunionya kuhusu ngono. Kisha nawaza, ‘Ni nani aliyesema kuhusu ndoa au ngono? Nimesema tu kwamba ana sura ya kuvutia.’”—Stacey.

Huenda ikakuliwaza kujua kwamba wazazi wako pia wanaona ugumu kuzungumza na wewe kuhusu ngono, kama vile tu unavyoona ugumu kuzungumza nao! Huenda ndiyo sababu uchunguzi mmoja ulionyesha kwamba asilimia 65 ya wazazi walidai kwamba wamezungumza na watoto wao kuhusu ngono, hali ni asilimia 41 tu ya watoto wanaokumbuka mazungumzo hayo kati yao na wazazi wao.

Ukweli ni kwamba, huenda wazazi wako wakasita kuzungumzia ngono. Kama ilivyo katika visa vingi, huenda wazazi wao hawakuzungumza nao kamwe kuhusu ngono! Hata sababu iwe gani, waelewe wazazi wako. Labda hata wewe mwenyewe unaweza kuanzisha mazungumzo hayo. Ingawa kufanya hivyo kunahitaji ujasiri mwingi, ninyi nyote, wewe na wao pia, mtafaidika. Jinsi gani?

Kuanzisha Mazungumzo

Wazazi wako wana hekima na mashauri mengi kuhusu ngono. Unachohitaji tu ni njia ya kuanzisha mazungumzo hayo. Jaribu njia inayofuata:

1 Eleza wasiwasi wako tangu mwanzo. “Nasita kuongea nawe kuhusu habari hii kwa kuwa huenda ukafikiri . . . ”

2 Kisha mwambie mzazi wako kwa nini umemwendea yeye. “Hata hivyo nina swali, na nimeona afadhali nikuulize wewe kuliko kumwuliza mtu mwingine yeyote.”

3 Halafu taja jambo linalokusumbua. “Swali langu ni . . . ”

4 Mwishoni mwa mazungumzo, hakikisha kwamba kuna nafasi ya kuendeleza mazungumzo hayo wakati ujao. “Nikiwa na swali lingine lolote, je, naweza kukuuliza tena?”

Hata ikiwa unajua atajibu ndiyo, kumsikia mzazi wako akisema hivyo kwaweza kufanya iwe rahisi kuzungumzia habari hiyo wakati ujao uhitaji utakapotokea. Basi jaribu njia hiyo! Huenda ukakubaliana na Trina. Sasa, akiwa na umri wa miaka 24, anasema: “Mimi na mama yangu tulipokuwa tukizungumza, nakumbuka nikitamani dunia ipasuke. Lakini sasa, nafurahi kwamba mama yangu aliniambia mambo waziwazi. Huo umekuwa ulinzi kwelikweli!”

[Picha katika ukurasa wa 59]

Kuyaaga maisha ya utotoni ni kama kuhamia eneo lingine—lakini unaweza kuzoea mabadiliko hayo

Machapisho ya Kiswahili (2000-2017)  Mapendezi
Copyright © 2016 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania Masharti ya Utumiaji  Sera ya Faragha   JW.ORG