Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 9 Julai 2017

Lukaku anashikiliwa na Polisi nchini Marekani / 5 hours ago  

Lukaku anashikiliwa na Polisi nchini Marekani

MUUNGWANA BLOG / 5 hours ago

 

 Pamoja na kuwa gumzo kuhusiana na uhamisho wake kwenda Manchester United, ’Romelu Lukaku atapandishwa kizimbani nchini Marekani.J

Mshambulizi huyo wa Everton aria wa Ubelgiji atapamba kizimbani Oktoba 2, mwaka huu katakana na usumbufu uliosababishwa na kelele zilizotoka katika jumba alilokodi katika eneo la Beverly Hills.
Amekamatwa wikiendi iliyopita baada ya majirani kulalamika kutokana na kelele hizo.

Kwa mujibu wa Polisi wa Beverly Hills, Lukaku alionywa mara tano kabla ya polisi hao kumuweka chini ya ulinzi.

Kwa Marekani na nchi za Ulaya, majirani wanaweza kushitaki kama mwingine anawasumbua kwa kelele.

Jumamosi, 8 Julai 2017

Siri Ya Kudumu Katika Mahusiano Ya Ndoa

Siri Ya Kudumu Katika Mahusiano Ya Ndoa

MUUNGWANA BLOG / 10 hours ago

Zipo changamoto ambazo zinazosababisha ndoa nyingi kufa.  Hata hivyo kufa kwa ndoa hizo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu wengi wamekuwa hawavitilii maanani.  Hata hivyo siku ya leo nimeona ni vyema nikujuze siri ya kudumu katika mahusiano ya ndoa. Je ni vitu gani? Twende sawa:

1 mapenzi ya kweli.
Ili uweze kudumu katika ndoa yako ni lazima uwe na mapenzi ya kweli kwa mwezi wako. Upendo wa kweli mara kadhaa huwa haupimwi kwa maneno tu bali ni kwa vitendo. Hivyo katika kuhakikisha unafurahia maisha ya mahusiano hakikisha unajua ni kipi kitokachomfanya mpenzi wako ajue ya kwamba unampenda. Hilo ni suala la msingi ambalo ni vyema ukalijua.

2. uvumilivu.
Kitu ambacho pia kitakusaidia kuweza kukaa kwa muda katika ndoa yako ni kuhakikisha unalijua lile somo la uvumilivu. Kama ambavyo siku ya ndoa yenu mliampa ya kwamba mtadumu katika ndoa yenu katika shida na laha.  Hivyo ili kuweza kulitimiza hilo ni lazima ukumbuke kiapo chenu.  Hii itawasidia sana kuweza kutengeneza maelewano ndani ya nyumba.

3 hofu ya mungu.
Ndoa yeyote ile ambayo inataka kuwa imara ni lazima iwe na hofu ya Mungu ndani yake.  Kama mliapa ya kwamba mtaishi pamoja mpaka kifo kitakapo watenganisha, hivyo ili yote hayo yawe kweli ni lazima Mungu atawale katika ndoa yenu ili muweze kutimiza lile ambalo mlikuwa mmeliahidi mbele ya Mwenyezi Mungu pamoja na mashaidi wengine.

4 uwezo wa kujishusha.
Hakuna kitu muhimu katika  mahusiano kama hiki. Kuwepo na uwezo wa kujishusha katika mahusiano kunafanya mahusiano hayo kuimarika. kwani ndoa    nyingi hufa kwa sababu ya kutokuwa na mtu mmoja ambaye anajishusha. Hata ugomvi wa wanandoa wengi hutokea kwa sababu ya kutokuwepo kwa kitu hicho.  Hivyo ili uweze kudumu katika ndoa ni kazima uwe na uwezo kujishusha hasa pale unapokosea.  Pia katika suala la kujishusha ni lazima ujue matumizi ya samahani. Neno samahani lina thamani kubwa katika kuongeza upendo kwa mwenzi wako.

5 Matumizi mazuri ya pesa.
Hili ni la muhimu kwa wanandoa. Kwa upande wa wanaume ili uweze kuwa bora, ni lazima uweze kuepuka matumizi mabaya ya fedha ambayo kwa mkeo yatakuwa ni kero.  Na pia kwa mwanamke ili kumfurahisha mwanaume ni lazima awe na nidhamu ya fedha,  hapa nikiwa na maana ya kwamba fedha za matumizi ambazo unaachiwa au kutafuta mwenyewe ni lazima uweze kuzitumia katika mpangilio.

6. Uchaguzi mzuri wa marafiki.
Ukiwa katika ndoa ni lazima uwe na marafiki sahihi ambao mwezi wako watampendeza kitabia, kwani wapo baadhi ya marafiki wao kazi yao ni kuvunja ndoa za watu.  Watu hawa kazi yao ni kichwa maneno kutoka upande A kwenda upande B.

Marafiki wa aina hii hawafai hata chembe. Hivyo ili kudumu katika mahusiano ya ndoa lazima ufanye uchaguzi sahihi wa marafiki.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada tukutane hapa hapa tunazungumzia kuhusu elimu ya mahusiano.

Jumanne, 4 Julai 2017

Je waitaji kuwa mke mwema jifunze hapa jinsi ya kufanya

Kanuni kumi '10' za kuwa mke mwema

KAMGISHA BLOG / 9 hours ago

UHALISI WA MAISHA:
Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo;

UVUMILIVU:
Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo.

UPENDO WA DHATI:
Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni Upendo wa dhati na uhalisia.

UTII KWA KWA JAMII:
Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka  ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii  kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa.

UAMINIFU KATIKA JAMII:
Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote.

UNYENYEKEVU WA KWELI:
Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima.

UWAJIBIKAJI WA DHATI:
Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake.

USHIRIKIANO WA DHATI:
Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora.

UTARATIBU WA KAZI/MPANGILIO:
Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako.

KUFANYA TATHIMINI:
Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku, pengine ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima n.k kama mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta faida/hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka. Ukiona faida ni kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka katika nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza wakati.

Hizi ni Fursa 150 za Biashara na Miradi Mbalimbali

Hizi ni Fursa 150 za Biashara na Miradi Mbalimbali

KAMGISHA BLOG / 9 hours ago


Hizi ni Fursa 150 za Biashara na Miradi Mbalimbali.

1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.
5.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k
34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51. Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi
ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo

Hizi Ndiyo Njaa Mbili Zinazowasumbua Wanandoa Katika Maisha Yao Ya Ndoa

Hizi Ndiyo Njaa Mbili Zinazowasumbua Wanandoa Katika Maisha Yao Ya Ndoa

KAMGISHA BLOG / 9 hours ago

Habari rafiki na mpenzi msomaji wa Amka Mtanzania? Na karibu tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza. Katika makala yetu ya leo tutajifunza njaa zinazowasumbua wanandoa katika maisha yao ya ndoa. Kuzifahamu njaa zinazowasumbua wanandoa tafadhali twende sanjari mpaka mwisho wa makala hii.

Kumekuwa na mitazamo hasi sana juu ya maisha ya ndoa. Kabla mtu hajaingia ndani ya maisha ya ndoa tayari akili yake imeshajazwa mitazamo hasi juu ya maisha ya ndoa. Mtu aliyepatwa na matatizo katika maisha yake ya ndoa naye atakwenda kuwaaminisha watu juu ya matatizo yake juu ya ndoa. Siyo kwamba katika maisha ya ndoa hakuna changamoto la hasha zipo kama kawaida kama vile kwenye kazi, biashara, ujasiriamali nakadhalika. Hivyo kwenye jambo lolote changamoto haziepukiki. Kweli itakuweka huru na usipoujua ukweli utapata shida sana.

Maisha ya ndoa unayotaka kuishi unayatengeneza wewe mwenyewe na si vinginevyo hivyo usipoteze muda wa kuhangaika tengeneza yale maisha ambayo unayataka kuishi na usisikilize kelele za watu ambazo zitakuwekea ukungu katika macho yako na kushindwa kuona mbele. Na waswahili wanasema ukiona vyaelea ujue vimeundwa kwa hiyo, hata wewe unaweza kuviunda katika maisha yako ya ndoa.
 
Katika hali ya kawaida hakuna mtu asiyeijua njaa, mtu akiwa na njaa anapoteza kabisa nguvu na hata ufanisi wa kazi aliyokuwa anafanya unapotea, kwa hiyo njaa huwa inalegeza watu kama akikosa kula chakula na kushiba. Vivyo hivyo, kila mwanandoa ana njaa yake yaani mwanaume ana njaa yake katika maisha ya ndoa hali kadhalika kwa mwanamke naye ana njaa yake. Kwa maana hiyo, kila mwanandoa anahitaji ashibishwe njaa yake na mwenza wake.

Ikitokea sasa wanandoa hao yaani wawili hao kutoshibishana njaa zao ndio matatizo huanzia hapo. Na tunajua ya kwamba wawili hao kila mmoja ana njaa yake. Hivi ikitokea mtu ana njaa ya chakula halafu pale anapotegemea kupata chakula ili ashibishe njaa yake hapati ataendelea kusubiri kubaki na njaa yake? Jibu ni kwamba lazima atatafuta sehemu ambayo ataweza kupata chakula ili aweze kushibisha njaa yake.

Ndugu msomaji, kama kila mwanandoa ameshindwa kumshibisha mwenzake basi ujue lazima atatafuta chakula sehemu nyingine ili kuweza kukidhi njaa yake. Hivyo basi, kumbe ni wajibu wa kila mwanandoa kuhakikisha anamshibisha mwenzake njaa yake.
 
Zifuatazo ni njaa mbili zinazowasumbua wanandoa endapo hawatashibishana; 

1. Njaa ya mwanamke ni upendo;
Mwanamke anahitaji upendo kuliko vitu vingine, hata katika vitabu vya dini vinasema; enyi waume, wapendeni wake zenu. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe, mwanaume anatakiwa kujitoa kwelikweli kumpenda mke wake kama tunavyojua upendo ndio falsafa kubwa sana katika maisha ya binadamu, upendo huvumilia, hufadhili, hauhusudu. Hivyo basi njaa ya mwanamke ni kupendwa. Wewe kama mwanaume unatakiwa kumpenda mke wako kwa moyo wako wote bila kujali udhaifu wake. Hii ndio njaa ya wanawake wanahitaji upendo katika maisha ya ndoa.
  
2. Njaa ya mwanaume ni kuheshimiwa; 
Mwanaume njaa yake kubwa ni kuheshimiwa katika maisha ya ndoa. Sasa ikitokea mwanaume anakosa kuheshimiwa na mke wake katika maisha ya ndoa hivyo anakuwa amekosa kushibishwa njaa yake. Na kama akikosa kushiba ndio matatizo huanzia hapo itamlazimu kutafuta kushibishwa njaa yake nje. Hivyo kama wewe ni mwanamke unatakiwa kumshibisha mume wako njaa yake ya kumtii.
  
Kama wanandoa wanashindwa kushibishana njaa zao, hivyo wanajitengenezea shimo wao wenyewe. Watu wanajisahau sana katika kutimiza majukumu yao katika maisha ya ndoa hatimaye wanaruhusu haki za kibinadamu kuingia maisha ya ndoa, kama wanandoa mkishaingiza haki za kibinadamu katika maisha ya ndoa yaani hamsini kwa hamsini kama wanavyodai lazima mtapoteza mwelekeo tu. Kwa hiyo kila mtu ana njaa yake kama tulivyoona hapo juu sasa mkishayaingiza mambo haya ya kidunia mtakosa kushibishana njaa zenu.

Jumatatu, 3 Julai 2017

Stars yapiga 1-0, yatinga nusu fainali

Stars yapiga 1-0, yatinga nusu fainali

KAMGISHA BLOG / 16 hours ago

Taifa Stars imetinga nusu fainali ya michuano ya Cosafa baada ya kuwatwanga wenyeji Afrika Kusini kwa bao 1-0.

Shuja wa mechi hiyo ambaye ameibuka nyota wa mchezo huo amekuwa ni Elius Maguri ambaye amefunga bao hilo pekee katika kipindi cha kwanza.

Kipa Aishi Manula mara kadhaa alilazimika kuokoa michomo mikali ya washambuliaji wa Afrika Kusini.

Safu ya ulinzi iliyoongozwa na Erasto Nyoni na Salim Mbonde ilionekana kukaa imara tokea kipindi cha kwanza lakini Muzamiru Yassin na Raphael Alpha wakaonekana kufanya vizuri zaidi katika.

Simon Msuva aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu na kusaidia kuongeza nguvu ya kupandisha presha kwenye lango la Afrika Kusini.

Tetesi zote za soka ulaya leo julai2

Tetesi Zote za Soka Ulaya leo Julai 2

KAMGISHA BLOG / 15 hours ago

Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 125 ili kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco na kuwazidi kete Real Madrid (Sunday Mirror).

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemuambia Alexis Sanchez, 28, kuwa hatojiunga na Manchester City msimu huu (Mail on Sunday).

Everton wanapanga kutaka kutoa pauni milioni 20 kumsajili mshambuliaji wa Arsnenal Olivier Giroud, 30 (The Sun).

Meneja wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ameonekana kutaka klabu yake kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwa kusema Sanchez ni "mchezaji mzuri" (London Evening Standard).

Manchester City pia wanamtaka Alexis Sanchez, lakini Arsenal hawatoruhusu mchezaji huyo kwenda katika klabu hasimu inayocheza Ligi Kuu ya England (Mail on Sunday).

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, yuko tayari kumruhusu kipa Joe Hart , 30, kuhamia kwa mahasimu wao Manchester United (Sunday Express).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho bado atataka kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 24, hata kama klabu hiyo itamsajili Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid (Sun).

Jurgen Klopp atamzuia Daniel Sturridge, 27, kuondoka Liverpool, kwa sababu itagharimu sana kupata mtu wa kuziba nafasi yake (Mirror).

Kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23, amekataa kusaini mkataba mpya Arsenal na yuko tayari kumaliza mkataba wake wa sasa na kuwa mchezaji huru msimu wa mwakani (Sunday Times).

Mshambuliaji Diego Costa, 28, anakaribia kujiunga tena na Atletico Madrid kutoka Chelsea, lakini hatoweza kucheza mpaka mwezi Januari (AS).

Beki wa Roma Anonio Rudiger, 24, ameonesha dalili kuwa anajiandaa kujiunga na Chelsea katika picha aliyoweka kwenye Instagram (Metro).

Chelsea wanataka kumsajili beki wa Exeter City Ethan Ampadu, 16, na wanajadili fidia kwa klabu hiyo ya daraja la pili (Guardian).

Swansea wanakaribia kumsajili kiungo mchezeshaji wa Las Palmas Roque Mesa, 28, kwa pauni milioni 11 (Sunday Telegraph).

Wakala wa beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin, 22, wameanza mazungumzo na Barcelona ya kumrejesha mchezaji huyo katika klabu yake ya zamani (Sport).

Beki wa Leeds United Charlie Taylor, 23, anakaribia kujiunga na Burnley (Yorkshire Post).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.