Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 12 Aprili 2020

Je Yesu alikuwa Mwislamu?

DiraElimu

Ni mwangaza wa maisha yako

 Nyumbani ▼

Jumapili, 7 Februari 2016

Je Yesu alikuwa Mwislamu?

Yako madai ya baadhi ya wanaharakati wa kiislamu wanaodai kuwa Eti bwana Yesu alikuwa Muislamu kwa madai kuwa alikuwa akiingia katika Masinagogi (yaani misikiti ya wayahudi) Luka 4;16,Pia kwa sababu alikuwa anaomba akiwa anasujudia (Mathayo 26;38-44) Maandiko haya kwa waislamu ndio kigezo kikuu cha kuwa Yesu ni mwislamu.Madai haya ni ya ajabu sana kwani yanapingana na ile kweli iliyomo katika quran na Khadithi za Kiislamu Kulazimisha kuwa Yesu alikuwa muislamu kunaanza kutufanya tukubali kuwa Qurani ni kweli kuwa si kitabu kinachoongoza katika kweli kwani ni Qurani yenyewe ndiyo inayosema kuwa Muhamad aliamuriwa awe wa kwanza miongoni mwa waliosilimu soma (Surat al-anaam 6;14)……. “Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu……” ayah ii inathibitisha wazi kuwa Muislamu wa kwanza katika wanaume aliyesilimu alikuwa Muhamadi mwenyewe, aidha katika  kitabu cha cha historia ya Maisha ya nabii muhamad uk 18 kifungu cha pili cha shekh Abdulla Saleh Farsy kinasema ….Basi Mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke akimaanishwa bi khadija unaona sasa linakuwa jambo la kushangaza kuona wana mujahidini wakipingana na maulamaa wao au wanazuoni wenzao au hata quran aidha wanaharakati hawa wa kiislamu kumbe wanataka kutuambia kuwa wayahudi nao ni waislamu? Na kama hivyo ndivyo je quran inafundisha nini kuhusu wayahudi? Soma  Surat al maida-5;51 inasema hivi….. “Enyi mlioamini msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa rafiki zenu (wa kuwapa siri zenu) wao kwa wao ni marafiki.Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki nao basi huyo atakuwa pamoja nao na hakika allah hawaongozi watu madhalimu….” Qurani inaonyesha kuwa Hakuna uhusiano wa waislamu na wayahudi wala wakristo Yesu alikuwa Myahudi na hivyo kuingia katika msikiti wa wayahudi ilikuwa ni desturi yao. Je muhindu akiingia kwenye msikiti wa wahindu ni mwislamu kwa sababu hiyo?



 Musa na Harun pia hawakuwa waislamu wala hawakuanzisha Dini

      Tukumbuke kuwa Yesu alikuja kutafuta  na kuokoa kile kilichopotea hivyo ilikuwa ni lazima aingie kwenye majengo ya watu waliopotea ili apate kuwafundisha Luka 4;17-30, hata hivyo mara nyingi watu hao wa kenye masinagogi walijaa ghadhabu na walimtoa nje ya mji wakimpeleka katika ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa wapate kumtupa chini.Luka 19;45-47 Yesu aliingia katika Hekaluni akaanza kuwatoa nje wale waliokuwa wakifanya biashara akawaambia imeandikwa nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi naye akawa akifundisha kila siku hekaluni je alikuwa dini   gani? Aidha ikumbukwe pia kuwa Paulo mtume pia aliingia katika masinagogi hayo Matendo 17;1-2 na pia ilikuwa ni desturi yake je wanaharakati wa kiislamu wanataka kutuambia kuwa Paulo naye pia alikuwa mwislamu? Kwa kuwa tu aliingia katika sinagogi? Mbona huwa hawadai kuwa Paulo mtume ni mwislamu? Aidha ni Muhimu kukumbuka kuwa mafundisho ya bwana Yesu yalikuwa yakipingana vikali na watu wa Masinagogi Yesu alikemea tabia zao za kupiga panda watoapo sadaka yaani walikuwa wanafiki Mathayo 6;2.,aliwakemea kwa kupenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pande za njia ili waonekane na watu hii nayo ilikuwa tabia ya kinafiki (Mathayo 6;5-15) aidha Bwana Yesu alifundisha kusali kwa kupitia sala ya bwana Baba yetu uliye mbinguni……….  Jambo ambalo waislamu hawalifuati kabisa,Mwishoni watu wa masinagogi walimfukuza Yesu kabisa wakiwa wamejaa ghadhabu ikiwa Yesu alikuwa mwislamu mwenzao iweje walimfukuza? Quran inasema  Wanafiki wamejenga msikiti wa kuleta udhia na kutia nguvu ukafiri……… Hivyo aya hii inathibitisha kwamba misikiti ni ya watu wanafiki,Pia quran  inayataja Masinagogi kuwa ni nyumba tofauti na Misikiti ona Surat al-hajj 22;40 Ambao wametolewa majumba (mjini)mwao pasipo haki ila kwa sababu wanasema  mola wetu ni mwenyezi mungu na kama mwenyezi Mungu asingali wakinga watu baadhi yao kwa wengine bila shaka yangalivunjwa MAHEKALU (Swaamiu) na MAKANISA (Wabiya-unw) na nyumba nyingine za ibada MASINAGOGI (Wasalawatunw) na MISIKITI (Masaajidu) ambamo jina la mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi…….. jambo linalo shangaza ni kuwa Qurani inataja masinagogi tofauti na misikiti kulikoni basi kama sinagogi ni msikiti?

    Biblia haitufundishi kuwa Yesu alikuwa Mwislamu inatuambia Yesu ni mwana wa Mungu soma (Mathayo 3;16-17,Yohana 17;1,8;54,)aidha Tunafundishwa kuwa Bwana Yesu ndiye mwanzilishi wa kanisa katika Mathayo 16;18 anasema  “Nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda”Yesu aliyasema hayo kabla Muhamad hajazaliwa wala uislamu haujaanza aidha ufunuo wa Yohana sura ya pili yoote  Yesu anazungumza na kanisa na anatofautisha na sinagogi. Hivyo Kanisa limeanzishwa na Bwana. Maadui wakubwa wa waislamu ni mayahudi Surat al maida 5;82 na Yesu alikuwa myahudi leo Mujahidina wanasemaje Yesu alikuwa Mwislamu? Na Quran inasema maadui zao ni wayahudi na biblia inasema Yesu alikuwa Myahudi soma (Yohana 4;9).

kwa Februari 07, 2016


Maoni 5 :

Unknown4 Desemba 2016 09:45

Unaona una matongotongo

Jibu


Unknown4 Desemba 2016 09:46

Muhammad aliposema kuwa ni wa kwanza alikua nakusudia wa kwanza kwa umma wake na sio wa kwanza kwa umma zote usikurupuke.

Jibu


Unknown4 Desemba 2016 09:47

Muhammad aliposema kuwa ni wa kwanza alikua nakusudia wa kwanza kwa umma wake na sio wa kwanza kwa umma zote usikurupuke.

Jibu


Unknown4 Desemba 2016 09:50

Unaona una matongotongo

Jibu


Raphael Kimaro9 Julai 2019 07:35

we kafir muhammad ndio wa kwanza kusilim. hiyo haya kwamba ndionwa kwanza kwa uma mbona hujatoa.

acha ujinga. elimu hiyo fundisha msikitini maana ndiko utaposema uongo ili mjifurahishe.

ukija huku sema ukweli tunataka andiko kama sisi tulivyotoa. na kwanza hata muhammad mwenyeww hakusilim maana hakuna haya aliyokubali. 

ndio maana wa kwanza kusilim akawa bi adija. muislam wa kwanza duniani sasa wewe leta mdomo badala ya andiko. mti mzima kutumia hisia badala ya akili ni hatari

Jibu



Nyumbani

Ona toleo la wavuti

Kunihusu

Mkuu wa wajenzi mwenye HekimaTazama wasifu wangu kamili

Inaendeshwa na Blogger.