Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 21 Julai 2019

Mambo yatakayo mfanya mwanamke akupende zaidi

N/A · 6 hours ago

Hakuna kitu chenye thamani kubwa kwa msichana yeyote yule  kama kumfanya mtu huyo afurahi, hivyo kila wakati mwanaume unatakiwa kumfanya mpenzi wako afurahi ili uwezo kuongeze asilimia nyingi za upendo kutoka kwake kuja kwako. 

Yafautayo ndiyo mambo ya kufanya ili kufurahisha mwanamke katika mahusianao ya mapenzi; 

Mtanie  
Unapoongea na msichana, ni rahisi sana kumfanya na yeye aongee na wewe hatakama hakupenda mwanzo. Lakini hiyo haitoshi. Kama unataka kujua ni jinsi gani ya kuongea na msichana/mwanamke, utapaswa kumfanya yeye ajisikie huru na mwenye kujiamini(confortable), lakini pia mfanye ajue kuwa unampenda hatakama haujamwambia. 

Kumbuka, kama utaongea nae kama rafiki, lazima awaze na ajue kuwa wewe ni mwanaume noma sana(great guy), lakini hatahisi kwamba wewe ni mwanaume unaeweza kumchangamsha au kumfurahisha. Ili kuonekana kama mwanaume anayefurahisha kwa mwanamke yeyote, inatakiwa akuone kama mtu muhimu wa kukutana nae, na ili kufanya hivyo, msukume sukume hata bega katikati ya maongezi. Lakini usizidishe sana utaishia kumboa, fanya hivyo pale tu anapoongea jambo linalochekesha au lenye utani ndani yake. 

Ila usiende na kumwambia maneno ya kawaida kama “unamuonekano mzuri”, “wewe ni mzuri sana”, au maneno yenye kufanana na hayo. Inawakera sana na haioneshi utofauti na watu wengine wa mtaani. Badala yake, jaribu kuwa specific wakati unamuambia jambo fulani mnapokutana. Mwambie maneno kama “umependeza sana leo. Huo ni mtindo mpya wa nywele?”, Hayo ni maneno mazuri sana kwa mwanamke kwa sababu ni wanaume wachache sana huyatumia kwao. Kwa hiyo unavyosema “leo umekua mrembo zaidi” inamfanya ajue ni jinsi gani unamaanisha mpaka umevunja ukimya. 

Kwa kumtania huko  unaweza kufanya mambo matatu. Unaweza kumshtua na kumfanya atabasamu. Unaweza kumfanya ajue kwamba wewe unamuona mtu wa tofauti sana. Au tatu, unaweza kumfanya atambue kwamba umemwona wa kuvutia sana. Kumbuka hayo yote unamfanya yeye aone ni mtu mzuri ambaye anaweza kudate na wewe. 

Kuwa mcheshi 
Baada ya kumfanya atabasamu na kuyafurahia maongezi yako na yeye, ni muda wa kumuingia ndani zaidi kidogo. Kila mmoja wetu ana mambo yake ya siri ambayo hatupendi watu wote wajue labda mtu ambaye tunamwamini sana. Ili kumfanya ajiamini kwako, unatakiwa kumfanya awe na good time sana na wewe. Sasa hatuwezi kukuambia kabisa jinsi ya kumfanya mwanamke acheke. Lakini tunaweza kukupa mambo mawili ya kutumia. Usimwambie utani wowote wakati unaongea nae. Kuwa mwenye furaha muda wote unaoongea nae. 

Hii inaweza kukutatiza kidogo. Kwanza kuongea utani wa moja kwa moja kama mtu aliyekariri ni ujinga. Badala yake, ongea nae maongezi yatakayomfanya aone unamtania, na hapo naye ataanza utani. 

Jitahidi kuonesha unafurahia maongezi wakati unaongea nae kama unataka kumchangamsha. Ukiwa na furaha, dunia nzima inatabasamu pamoja nawe!. Kama unatabasamu na kujisikia furaha, naye atatabasamu pia na kuwa na furaha. Lakini kama unauoga, utamfanya naye awe  mwoga (unconfortable). 

Unaweza kumsukuma kidogo kati kati ya maongezi  
Najua unaelewa ninaposema kusukumana, hii utokea mara nyingi pale mvulana na msichana wanapukua wamezoeana, kwa hiyo kuifanya na mwanamke kwa mara ya kwanza inatakiwa uwe mwangalifu na makini ili usije kuharibu. Unapofanikiwa kufanya hivyo, jitahidi isiwe kila saa maana utamkera kama nilivyosema hapo awali. 

Ili uweze kufanya hivyo inatakiwa uwe wa kawaida, chukulia kama ni mtu wa kawaida japo wewe unajua ni special. Muulize alifanya nini weekend au baada ya kutoka kazini, muulize anapenda kwenda wapi akitoka out au ni mgahawa gani anaupenda au anatamani kwenda au kitu kingine chochote ambacho ni binafsi(very personal). 

Mshike.  
Huu ni uwanja hatari sana, lakini ni kitu unachopaswa kujifunza kwa sababu unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, si ndiyo? Hivyo kumshika katika muda muafaka inakamilisha point ya hii ya mambo ambayo unapaswa kuyajua wakati unataka kumfurahisha mwanamke. Kama utafanikiwa kulifanya hili kwa usahihi, utakua umejichukulia point kubwa sana. 

Sasa kumshika msichana ni kama kucheza na moto. Ukiushika fasta hauwezi kusikia joto, lakini ukiushika muda mrefu utaungua! Unaona ilivyo hatari?  Unaweza kumshika bega au mikono kama tayari ushamfurahisha vya kutosha. Lakini kumbuka hili, mshike tu pale unapokua na sababu ya kumshika, mfano mshike masikio kama unayasifia masikio yake au nywele kama unazisifia nywele zake, au mfute koti lake kama kuna kauchafu hatakama hana hako kauchafu, au mshike begani kama unatembea nae barabarani/ mtaani. 

Kumbuka kumshika mtu ni very personal, hivyo inabidi uwe makini sana na uangalie anamuitikio gani wakati unamshika kabla haujamshika tena. Kama unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, yatumie haya mambo matano wakati utakapokutana na mwanamke next time. Na baada ya hapo utaona ni jinsi gani unavyoweza kumfurahisha mwanamke na kumfanya ayapende maongezi yako kwa mara ya kwanza!.

Jumatatu, 15 Julai 2019

Orando-Malaika-Audio download

Download-orlando-Malaika Audio free


  

 
Size 3.96 Mb
N/A · 34 minutes ago


Watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mbalimbali ambayo yanahusiana na masuala ya kibiashara. Na miongoni mwa maswali ambayo wamekuwa wakiniuliza ni kuhusu ni nini faida ya kutangaza biashara kwa sehemu kubwa? 

Swali hili ndilo limenifanya nishike kalamu yangu ili niweze kulijibu. Nakusihi twende sambamba ili niweze kueleza kwa kinagaubaga, kwa nini unapaswa kuitangaza biashara yako tena kwa nguvu zote. 
Matangazo ni usambazaji wa taarifa  sahihi  kuhusu bidhaa au huduma kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. Matangazo ndiyo roho ya biashara, kwani bila kufanya biashara yako bila matangazo ni sawa na bure. 

Nafikiri pia utakubaliana nami ya kuwa ili uweze kufanya biashara  yenye tija ni lazima uitangaze biashara yako, kwani " biashara ni matangazo".  Matangazo ndiyo yatakuyokufanya uweze kuongeza mauzo ya kibiashara kila wakati. 

Kwa kuzingatia hilo unaweza kuitangaza biashara yako kwa njia ambayo itakuwa ni rahisi kwako. Na sababu kubwa ya kuitangaza biashara yako ni kuongeza wateja wapya. 

Leo na dhumuni kubwa la kutangaza biashara yako ni kukutana na na watu wapya,  ukiona umetangaza biashara yako na hakuna mteja mpya hata mmoja ujue fika kuna mahala ambapo umekosea. 

Hivyo fanya tathimni upya na ujipange upya na kuona ni jinsi gani unaweza kuitangaza biashara hiyo. Vile vile katika upangaji wa malengo ya kibiashara hakikisha ya kwamba unapanga na mbinu za kukutana na watu wapya kila siku. 

Nasisitiza juu ya kukutana na watu wapya, kwa sababu nimegundua ya biashara nyingi zimekuwa hazifanyi vizuri kwa sababu zimekuwa na watu ambao wanaizunguka biashara ile ni wale wale kila siku. Hivyo kila siku fanya tathimini juu wateja wapya ambao wamekuja katika biashara yako. 

Asante kwa kutembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio,  usisite kumshirikisha na mwingine ili aweze kujifunza.

Download

https://www.mediafire.com/download/astemzzag9g21b4

Orando montana x man piro x spero spera malaika

https://www.youtube.com/watch?v=238tsWknd_g&feature=share

Jumamosi, 13 Julai 2019

Jinsi ya kumfanya mumeo awahi kurudi nyumbani


KAMGISHA BLOG· 5 hours ago




Inawezekana ukawa upo kwenye mahusiano yenye changamoto ya Mume wako kuchelewa kurudi nyumbani, Zifuatazo ni njia ambazo zinaweza kukusaidia kumrejesha mapema nyumbani. 

Jambo la kwanza ni vizuri ukajiuliza kama kweli upo katika ndoa sahihi, kwa kutizama chanzo cha mahusiano yenu ni kitu gani kilichowaunganisha lakini Pia ukajiuliza bila kujidanganya wewe na Mumeo mnafahamu maana halisi ya mapenzi ? 

Baada ya maswali hayo naomba ufahamu kwamba mapenzi yoyote yale lengo lake kubwa ni kuleta utulivu na kuhurumiana. 

Je ndoa yako inakupa utulivu na mnahurumiana?, kama mnahurumiana iweje Mumeo achelewe kurudi nyumbani huku akijua fika kwamba wewe Mkewe hupendi achelewe kurudi nyumbani na kuchelewa kwake kunakuondolea utulivu ?.

Hatua Zifuatazo zitakusaidia kumrejesha Mumeo nyumbani mapema: 

Je wewe sio chanzo cha Mumeo kuchelewa kurudi nyumbani? Na kama wewe unachangia kwa namna yeyote ile basi rekebisha yale asiyoyapenda Mumeo na hapo utakuwa umemaliza tatizo. 


Pambana na tatizo na sio Mtu, tambua tatizo, tafuta elimu ya tatizo husika ili upande daraja. 


Kuwa mvumilivu, mwenye hekima, busara, msikivu, mwenye kusamehe na kusahau. 


Kiri makosa yako na omba msamaha. 


Kubali kushindwa na usiwe mshindi kila siku hata kama umeshinda. 


Penda kabla hujapendwa. 


Toa kabla hujapokea. 


Japo inauma lakini usimuulize alikuwa wapi na kwa nini amechelewa kurudi. 


Mkaribishe kwa bashasha na mpe pole ya huko alikotoka. 


Hakikisha anakukuta ukiwa msafi na mwenye mvuto kama vile umerudi kutoka matembezi. 


Mpe chakula na kaa ule pamoja nae na kama ulishakula kaa karibu yake. 


Onesha kama vile unafurahia yeye kuchelewa kurudi, japo unaumia kwa ndani. 


Usioneshe kama vile una wivu wa yeye kuchelewa kurudi, bali onesha kuwa unahofia usalama wake anapochelewa kurudi. 


Usimnyime tendo la ndoa hata kama kachelewa kurudi na furahia tendo hilo kama vile ulikuwa ukimsubiria kwa hamu. 


Anapotoka onesha kama vile na wewe utatoka lakini usitoke bila ridhaa yake.


Mambo ambayo wanawake wanapaswa kuyazingatia kabla na baada ya kuolewa


N/A · Yesterday




Naomba kuleta kwenu mambo ambayo naamini ni muhimu kuyatafakari na kuyapa uzito wenye kustahili. 

Yafuatayo ndiyo mambo ambayo unapaswa kuyazingatia kabla na baada ya kuolewa: 

1. Kujitambua 
Kila msichana aweze kutambua nini kinamfanya kuwa mwanamke. Kwa maana kama ni maumbile hiyo ni default settings, kama ni kuzaa mwanaume haendi leba, sasa ni nini kinakufanya kuwa mwanamke? Kujitambua, kujiheshimu na kuwajibika. Nyumba yenye mwanamke anayeheshimika ni Baraka na nyota njema. Nyumba yenye mwanamke asiyejiheshimu na kuheshimika huwa haitamaniki, wewe wataka kuwa yupi kati yao? 

2. Kila mwanaume ni tofauti 
'wanaume wote ni wale wale tu'' Ni vibaya sana kumchukulia mwanaume sawa tu na wengine (hata kwa rafiki wa kawaida tu). Kuwa unajua au umesikia sifa mbaya za wanaume flani na flani, au umewahi kuwa na mahusiano na ukaona sifa mbaya kadha wa kadha za huyo, ukaja ukampata mwingine harafu unamchukulia ni sawa na hao wengine tu. (kosa kubwa sana) Kila mwanaume ana sifa zake na mapungufu yake. Sifa na mapungufu ya mmoja sio sawa na mwingine. 

3. kuamua kuolewa au kutokuolewa 
Uamue kama unajiona una wito wa kuolewa au la, tena uamue kwa utashi wako mwenyewe. Usipokuwa umeamua unakosa nafasi adhimu ya kuwa umejianda kuwa chini ya mume na utaona kama unaonewa vile!! Mabaya aliopitia mama au jirani yako kwa mumewe isiwe ndio determinant factor kwa huwa hutaolewa kwani utaolewa na huyo mtesaji au huyu unayemchukia? 

Hakika Utaolewa na mwanaume mwingine mwenye sifa na tabia tofauti na kila kitu tofauti na hao, kwa nini uwatumie hao kama ndio wawakilishi wa wanaume wote na ndio wako hivyo? Kwa nini wengi wenu msijifunze kwa wanawake waliofanikiwa kwenye ndoa kuliko hao role models wa kwenye taarabu na saluni? tunajifunza kutoanguka kwa walioanguka iweje hao walioshindwa ndoa ndio wawe chachu kwako? si unajua ni wanawake wachache sana wanapenda kuona mwenzake akifanikiwa?? wengi wanapenda mabaya au shimbo alioanguka na mwenzake nae aanguke hapo. 

5. Dhana ya haki sawa 
Binafsi naamini kila binadamu ni sawa, ila linapokuja swala la mume na mke huwa nashindwa kuelewa ni haki zipi izo zinazopiganiwa wakati katiba ya nchi haitamki jinsia kwenye haki na stahili?. Au mnataka mke akiwa anakata kitunguu mume awe anakata nyanya?? Mwanamke anapewa heshima ya kuwa msaidizi wa mume. Kuna umuhimu sana wa kutambua na kuchukua nafasi yako kama mwanamke. Beijing waache na wabeijing wenzao. Mwanaume ni Kiongozi wa Mkewe na familia nzima (sifa ya kiongozi- anajali- anawatanguliza wenzake, anasikiliza, anashaurika, anaona mbele, anawajibika, hekima na busara etc) 

6. Kujua kupangilia matumizi 
Kwa pesa ya familia ya yake kwa ajili ya matumizi binafsi "spending wisdom'' sio kila nguo mpya unayo, msuko mpya unao, kiatu kipya unacho, saa mpya unayo, mkufu mpya unao, kulikoni kwani, Kwa kile kingi au kidogo mnachojaliwa, kitumieni kwa hekima na shukrani.

Jumatano, 10 Julai 2019

Unachotakiwa kufanya unapokuwa umeachwa katika mahusiano ya kimapenzi

Unachotakiwa kufanya unapokuwa umeachwa katika mahusiano ya kimapenzi

N/A · Yesterday



Mapenzi yanauma. Yanauma kwelikweli. Unapokuwa umewekeza nguvu, mwili na akili kwa mtu halafu ikatokea amekatisha safari ghafla huwa inauma. Inauma sababu ulikuwa na maono ya mbali na penzi lako. Unaumia kwa sababu hukutegemea kama safari ya uhusiano wenu itaishia katika hatua hiyo. Inawezekana ulifikiri kwamba mngefika kwenye hatua ya ndoa lakini haikuwa hivyo. 

Yawezekana ulikuwa na ndoto ya kuwa na familia, uitwe baba au mama. Ulikuwa unatamani kuzaa na mwanaume au mwanamke wa ndoto yako lakini kumbe sio. 
Anaondoka kwenye kipindi ambacho wewe bado unamhitaji. 

Leo nataka nikupe siri ya ushindi kupitia safu hii. Inapotokea umeumizwa penzini, unachotakiwa kufanya ni kutulia. Itulize akili yako vizuri na usiiweke kwenye mawazo hata kidogo. Muhimu ni kukubaliana na kitendo kilichotokea. 

Kama mwanaume au mwanamke wako amekuacha, kubali. Ona kwamba kuna sababu za wewe kukuacha lakini usihangaike nazo sana wakati huo maana zitakutesa bure tu. 
Kuanza kuwaza kwamba labda sijui amekuacha sababu wewe si mzuri, kwamba huna fedha, utaumia tu! 

Kuwaza kwamba sijui una upungufu gani, sijui kwa nini ni wewe kila siku unaumizwa ni makosa makubwa. Kubaliana na matokeo haraka. Ifanye akili yako iwaze vitu vipya hata kama uliyekuwa naye ulimpenda kiasi gani. 

Ameshaamua kukuacha, ana sababu zake hivyo ukiendelea kupigana kuzijua hizo sababu ni kazi bure. Muache aende na wewe utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuingia kwenye uhusiano mwingine hapo baadaye kama aliyekuacha hatajirudi. 

Marafiki zangu, maisha ya uhusiano yana siri kubwa sana. Kila mmoja kwenye historia ya uhusiano na mwenzi wake anapitia mengi hadi kufikia hatua ya kuingia kwenye ndoa. Wakati mwingine inakuwa hata ni vigumu kujua kwamba atakayekuoa au kumuoa ni nani. 

Unaingia na mtu kwenye uhusiano, mnaishi miaka miwili mitatu mnaachana. Unaingia kwenye uhusiano na mtu mwingine, mnaachana. Unarudi kwa yule wa awali, mnakaa kipindi fulani lakini wapi. Kidudu mtu anaingia, uhusiano unayumba tena. 

Unavurugwa mno. Unajiona kama huna bahati na unasahau kwamba maisha ya uhusiano ndivyo yalivyo. Unayekwenda kuingia naye kwenye ndoa wakati mwingine ni vigumu sana kumjua. Akili za kibinadamu mara nyingi zinatudanganya tu. 
Ndugu zangu, licha ya kwamba sisi binadamu tuna macho yetu na akili lakini juu ya nani hasa unakwenda kuingia naye kwenye ndoa huwa ni Mungu ndiye ajuaye. 
Mungu anatujua sisi tangu tukiwa matumboni mwa mama zetu. Anajua mahitaji ya maisha yetu kabla hata hatujamuomba. 

Tunahangaika na dunia yetu hii ya uzuri wa sura. Tunapagawa na mambo ya kidunia lakini unganiko la ndoa alijuaye ni yeye pekee. Unapoona kuna janga limetokea kwenye uhusiano wako, mshukuru Mungu tamka neno hili; ‘hili nalo litapita.’ 

Kama aliyekuacha amepangwa awe wako atakuwa. Kama hajapangwa basi atakuja ambaye ni sahihi. Cha msingi wewe sema tu na moyo wako. Tamka tena maneno haya; ‘ipo siku tu.’ Maneno hayo matatu ni muhimu katika mustakabali wa furaha yako. 

Yatakufariji. Yatakutia nguvu ya kuendelea na maisha upya hata kama umeumia kiasi gani, utasema lazima maisha yaendelee. Kataa kuwa mtu wa mateso kila siku. Usiwaze sababu kama huyo ameondoka na si wako basi amini kwamba ipo siku atakuja mtu sahihi. 

Utashanga atakapokuja mambo yananyooka tu yenyewe bila hata kutumia nguvu nyingi. Mwezi wa kwanza wa pili mambo yanajipa. Mnaingia kwenye ndoa na maisha yanakuwa ni bambam.