Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 13 Februari 2019

Uislamu chanzo chake

Ili kuweza kufahamu chimbuko halisi la Uislam inafaa kuyafahamu mazingira ya Uarabuni kabla ya Uislam, mtu aliyeitwa Muhammad na historia ya mwanzo ya Uislam. Elimu kale (akiolojia), Kurani na Hadithi vina mengi ya kusimlia ambayo watu wengi wanaweza kuwa hawajui.

Maka kabla ya Muhammad

Umeishawahi kujiuliza Maka ilikuwaje kabla Muhammad hajazaliwa? Yaelekea ilikuwa sehemu ya kuvutia, kwani ilikuwa ni kituo cha biashara, mahali penye kusanyiko la tamaduni mbalimbali. Palikuwa na wafanya biashara wenye dini mbalimbali. Watu wa kabila la Kureshi wa Maka walimwabudu Hubal, Al-ilah na mabinti watatu wa Al- ilah. Mwamba mweusi kutoka mbinguni uliheshimiwa sana uliwekwa kwenye kona ya kaaba. Kaaba ilikuwa ni kitovu cha kuabudia miungu/sanamu 360 kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 43 sura ya 33 na.658 uk. 396 na juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 47 na.583 uk. 406.

Ensaiklopidia ya Uislam (iliyohaririwa na Eliade) uk.303 na kuendelea inasema, watu, kabla ya Uislam, waliomba mara 5 wakielekeza nyuso zao Maka na kufunga nusu siku kwa muda wa mwezi mzima. Wakureshi walifunga siku ya 10 ya Myharram/Muharam. Hii nayo Muhammad aliagiza ifanyike, lakini baadaye ikawa hiari. (Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 25 na.172 uk.109), pia Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 24 na.31 uk. 25.

Waarabu kabla ya Uislam walifanya hija (Umrah) Maka. Fiqh us-Sunnah juzuu ya 5 uk.122, na Bukhari juzuu ya 2 kitabu 26 sura ya 33 na.635 uk.371-372 zinasema walidhani kutokufanya 'Umrah ikijuwa ni moja ya dhambi kubwa sana duniani. Walipofika Maka waliifunika kaaba kwa nguo ya Fiqh juzuu ya 5 uk.131, na walikuwa na mwezi mtakatifu uliohitaji kujitenga na vita kabla ya kuja kwa Uislam (Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 23 sura ya 96 na.482 uk.273.

Chimbuko la Neno "Allah"

Kwa ujumla: Neno "Allah" ni kifupi cha neno la kiarabu La-ilah, ambalo maana yake ni "mungu". Wakristo wa kiarabu na wapagani walitumia neno Ilah kwa maana ya Mungu. Hata Biblia za kiarabu na kiindonesia leo hii hutumia neno "Allah" kwa maaana ya Mungu. Wakati wa nyuma neno linalofanana na hilo el lilimaanisha "mungu" wa kweli au uongo katika lugha za mashariki ya kati kama kiugariki, kikaanani na kiebrania. Kabla ya Muhammad, kaaba jengo lililotunza sanamu 360 liliitwa Beit-Allah, au "Nyumba ya Allah". Baba yake Muhammad ambaye alifariki kabla ya Muhammad kuzaliwa, aliitwa Abdullah maana yake, mtumwa wa Mungu. Pia kabila la Wayahudi liliitwa 'Abdullah bin Salam kwenye Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 13 na. 362 uk.241.

Kwa udhahiri: miongoni mwa sanamu/miungu iliyoabudiwa Maka uliitwa "Allah." Huyu alikuwa mungu maalum wa kabila la Wakureshi naye alikuwa na mabinti watatu maalum. Ukilinganisha na nguzo 4 kati ya 5 za Uislam, watu wa Maka kabla ya Muhammad walifunga kwa pamoja siku moja, walitoa sadaka kwa maskini wao, walisali wakielekeza nyuso zao Maka, na walifanya hija ('Umrah) Maka. Kulikuwa na tofauti nyingi pia, lakini inashangaza kuona muendelezo wa matendo yasiyobadilika yaliyokuwa yakifanyika kwenye ibada za kipagani za kikureshi.

Kama ambavyo kifungu hiki kitaonesha, kama ambavyo mungu maalumu wa kiyunani Zeus  alivyotoakana na neno Mungu (theos), jambo kama hilo limetokea miongoni mwa Waarabu kabla ya Uislam.

Wanaomcha Allah

Watu wengi wa kale walimwabudu mungu jua na mungu mke mwezi. Waarabu wa magharibi walikuwa tofauti kwa kumwabudu mungu mwezi na mkewe, mungu mke jua. Kuna sanamu za kabla ya Uislam za alama yake: mwezi mwandamo. Sanamu hii inafanana sana na mwezi mwandamo wa wa Waislam wa Shia, isipokuwa Washia wameongeza nyota ndogo. Wayemen/Sabaeans walikuwa na mungu mwezi kwa mujibu wa Ensaiklopidia ya Uislamu uk.303. Wakureshi wanawezakuwa walimpata mungu huyu kutoka kwao.

Allah alikuwa na mabinti watatu walioitwa Lat, 'Uzza na Manat. Siku moja "Nabii wa Allah" aliafiki na kusema katika Quran (Sura 53:19) kuwa maombezi yao yanapaswa kutumainiwa. Kwa maneno mengine alisema tunapaswa kutumaini msaada wa miungu hawa watatu.

Wafuasi wa Muhammad