Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 15 Januari 2018

Sababu

Sababu kuu 7 za kwanini kila mwanaume anahitaji mwanamke sahihi

Muungwana Blog 5 · Yesterday



Kwangu kipindi ambacho kilinivutia sana ni kipindi cha kampeni za uchaguzi nchini Marekani. 

Ni pale Obama akiwa katika kampeni kwenye moja ya majimbo kugombea duru ya pili ya uraisi aliposimamisha hotuba yake na kutambua uwepo wa mkewe Michelle. 

Obama alisema, "Mke wangu amekuwa bega kwa bega na mimi tokea niko chuo, kuna kipindi nilishindwa kulipa ada ila yeye ndiye aliyenilipia" 

Obama akaenda mbali zaidi na kukiri mbele ya jamii ya kimataifa kwamba asingekuwepo hapo alipo kama sio mke wake Michelle. 

Hivyo basi, nashauri kwamba mwanamke ambae mwanaume atakua nae huenda akawa chachu ya mafanikio na baraka kwake au anaweza akamrudisha nyuma kabisa katika mipango yake. 

Sababu kuu 7 za kwanini iwe isiwe mwanaume lazima upate mwanamke alie sahihi. 

1. Kila mwanamke anao uwezo wa kukuridhisha kimapenzi ila mwanamke sahihi na bora pekee ndiue anaeweza kuku-challenge kiakili na kuwa 'intellectually inspired'. 

2. Mwanamke yeyote anaweza kukuteka kihisia, ila yule sahihi pekee ndiye mwenye uwezo wa kukuteka kiroho na ukamtumikia Mungu wako. 

3. Mwanamke yeyote anaweza akakushawishi muandike mpango wa harusi (wedding plan), ila mwanamke sahihi peke yake ndie mwenye uwezo wa kukuandikia na kukushauri mpango wa biashara (business plan) 

4. Kila mwanamke anaweza akakubusu tena 'French kiss' ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukutamkia maneno yaliyojaa busara na hekima. 

5. Kila mwanamke anaweza akakupenda sana tu tena kama una pesa, ila mwanamke aliye bora pekee ndiye anaeweza kusimama na wewe hata kukuinua pale utakapokuwa huna kitu. 

6. Mwanamke yeyote anao uwezo wa kukushibisha kwa kukupikia chakula kitamu, ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukulisha chakula cha ubongo. 

7. Kila mwanamke anao uwezo wa kukushawishi chumbani ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukushawishi umrudie Mungu wako. 

Mwisho ngoja nihitimishe kwa kusema hivi ukisoma vitabu vya kihistoria kuhusu Winstom Churchhill mpaka Abraham Lincoln, na kutoka kwa Nelson Mandela mpaka kwa Martin Luther King Jr lao moja kwamba “No matter how strong a Man is, he is only as strong as the Woman he marries” Kwa tafsiri yangu ya kuunga unga isiyo sahihi sana Wanamaanisha "haijalishi ni kwa kiasi gani mwanaume una nguvu, nguvu zako zina athiriwa kwa kiasi kikubwa na mwanamke utakaemuoa"

Jumatatu, 8 Januari 2018

King mafla misemo ya ukweli

M


MandagoJF-Expert Member

#1Oct 5, 2010Joined: Feb 8, 2008Messages: 238 Likes Received: 80 Trophy Points: 45

Baadhi za Hekima na Methali za Kiarabu

1) Si vigumu kujitolea kwa kumsaidia rafiki yako,lakini ni vigumu kupata rafiki ajitolee kwa ajili yako.

2) Usiache ulimi wako ukafuata macho yako kwa kueleza aibu za watu, kumbuka kuwa watu nao wana macho na ulimi kama wewe.

3) Mambo yasiyokuwa na umuhimu huzungumzwa kwa muda mrefu kwani sote tuna yafahamu kuliko mambo muhimu.

4) Ikiwa una mikate miwili kula mmoja na mwingine utowe sadaka.

5) Mtu akisifiwa watu wachache huamini,lakini akikashifiwa wengi huamini.

6) Hakuna mtu ambaye hakufanikiwa kabisa,bali ameanzia na sifuri akabakia hapohapo. 

7) Binaadamu ambaye amefaulu ni yule anaye nyamaza kabla ya watu hawaja ziba masikio yao, na anafunguwa masikio yake kabla ya watu hawajafunguwa midomo yao. 

8) Kabla ya kuzungumza chaguwa neno la kusema, na uchukuwe muda wa kusema ili maneno yako yachipuwe kama linavyo chipuwa tunda.

9) Jihadhari na mtu ambaye ni mkarimu ukimdharau,na mtu mbaya ukimkarimu,na mwenye akili ukimkosowa na mjinga ukimrehemu.

10) Ukifikia kilele mwangalie jambazi ili upate mtu wa kukusaidia,na angalia mbinguni ili Mwenyeezi Mungu akuweke imara usianguke. 

11) Si kufaulu kugunduwa mambo wanayo yapenda watu,lakini kufaulu ni kuwa na ujuzi wa kuwafanya watu wakakupenda.

12) Shujaa anaye jitahidi kutatuwa matatizo yake,anafaidika na uwezo wake

13) Ukipanda jabali angalia kilele chake,wala usiangalie upande wowote na ulipande kwa makini,wala usiruke ukavunja mguu wako.

14) Shujaa ni yule ambaye anauwezo wa kukuza ujuzi wake,na kuweza kukuza ujuzi wa watu na pengine kuwabadilisha.

15) Usiache utajiri ukakufanya ukakosana na watu,kwani kuwa pamoja na watu ndio njia ya kuupata utajiri.

16) Badali ya kukaa na kutukana kiza,jaribu kutengeneza umeme. 

17) Ukitabasamu tabasamu kwa mtu masikini, kwani kunakuongezea malipo mema kwa Mwenyeezi Mungu.

18) Mwanamke humsubiria mume wake kwa umasikini wake,ubaya wake na kutokumjali kwake ,lakini hamsubirii kwa tabia mbaya yake.

19) Mtoto ni kama udongo(wa ufinyanzi) tuna mlea kwa jinsi tunavyo ona sisi. 

20) Watendee watu kama wao ni binaadamu si kwa sura zao wala pesa zao wala vyeo vyao. 

21) Uzuri wa mtu ni ndani ya nafsi yake,si sura yake. 

22) Ukisema neno litakumiliki,na usipolisema utalimiliki.

23) Anaye ishi na sura mbili,hufa bila ya sura

24) Adui yako akikuomba ushauri mpe nasiha,kwani ukimpa ushauri ataondosha uadui wake kwako na kukusaidia.

25) Ukizungumza wakati ukiwa na hasira,utasema neno ambalo utajutia maisha yako.

26) Usijadiliane na mtu mjeuri wala asiyekuwa na haya, kwani jeuri hutomuweza na asiye na haya atakuudhi.

27) Tabia njema ina sitiri mambo mengi mabaya,na tabia mbaya ina ziba mambo mengi mazuri.

28) Mwenye kumuamini Mwenyeezi Mungu humpa,mwenye kutawakal kwake humtosha,mwenye kumuogopa huacha aliyo yakataza na mwenye kumjuwa humuenzi.

29) Kunyamaza ni dalili ya kukubali jambo.

30) Jihadhari na ulimi wako,usiiponze shingo yako. 

31) Fimbo ya muongo ni fupi.

32) Si kila wakati mtu husalimika na jirani.

33) Ulimi wako ni kama farasi wako,ukiuchunga vizuri nao utakuchunga na ukiuachia nao utakuponza.

34) Ndege mmoja aliye mkononi mwako ni bora,kuliko kumi waliyoko katika mti.

35) Kila kimya kina jambo lake.

36) Ukitaka kutiiwa,amrisha mambo yanayo weza kufanywa.

37) Wezi wawili wakigo mbana ,vitajulikana vitu vilivyo ibwa.

38) Jihadhari na shari hata kwa mtu uliye mfanyia mema.

39) Upanga umeshinda kanuni.

40) Mwanzo wa mavuno ni tone la mvuwa.

41) Kuwa na haya ni katika imani.

42) Mazungumzo mazuri huwa mafupi na yanayo eleweka.

43) Mwaka ni kama siku mbili,siku kupata na siku kukosa.

44) Huto pata hasara ukimshauri mtu.

45) Haraka hutokana na shetani.

46) Kila kiongozi,na hotuba yake.

47) Mwenye kuingilia jambo lisilo muhusu,husikia yasiyo mridhisha.

48) Wakati ni kama upanga usipo ukata utakukata.

49) Haurushiwi mawe,isipokuwa mti wenye matunda.

50) Mwenye kuwachunguza watu hufa kwa kiroro(hamu). 

51) Watu bora zaidi ni wale wanao towa daawa kwa vitendo vyao kabla ya maneno yao.

52) Uwezo wa kuathiri nyoya za watu,na kupata pendo lao la kweli hutuletea furaha kubwa katika maisha yetu.

53) Nia nzuri ni kufanya ujuzi wa kuwafanyia watu mambo ya ibada,kwani hukukurubisha na Mwenyeezi Mungu(huwa karibu na Mweyeezi Mungu) 

54) Usifikirie watu wote ni sawa,kwani kuna watu wenye tabia tofauti kuliko aina za rangi

55) Zungumza na watu kwa mambo ambayo wana penda kuyasikia,siyo kwa mambo ambayo unaya penda wewe.

56) Mkutano wa kwanza huchukuwa asilimia thamanini ya tabia ya mtu anavyo onekana, wafanyie watu wote kama kwamba huo ni mkutano wa kwanza na wa mwisho kati yenu.

57) Kuijuwa tabia ya mtu ndio kuna kupa uwezo wa kupata pendo lake.

58) Kila mtu ana ufunguo wake,kwa kujuwa tabia ya mtu ndio kujuwa njia ya kuelewana nae.

59) Binaadamu hufanya mambo yote kwa moyo wake siyo kwa mwili wake.

60) Ukimiliki nyoyo za watu hupendeka

61) Mtu kujitahidi kutoingilia mambo yasiyo muhusu ni vigumu lakini humpumzisha.

62) Kuwa kama nyuki anatuwa juu ya kitu kizuri na kujiepusha na kitu kibaya, usiwe kama inzi kutuwa juu ya vidonda.

63) Huwezi kula asali bila ya kuvunja nyumba ya nyuki.

64) tukifanya watu wajuwe kwamba tunaangalia mazuri yao kabla ya mabaya yao watakubali kupokea nasiha.

65) Ni bora mtu kujuwa kosa lake si sharti kulisahihisha mbele ya watu.


R

ReasoningMember

#2Oct 6, 2010Joined: Mar 7, 2009Messages: 57 Likes Received: 0 Trophy Points: 0

Asante Mandago. Hakika ni misemo iliyojaa hekima sana. Chukua tano!!!


myao wa tunduruJF-Expert Member

#3Oct 6, 2010Joined: Mar 9, 2010Messages: 613 Likes Received: 20 Trophy Points: 0

ubarikiwe mkuu Mandago....nimejifunza kitu


MahmoodJF-Expert Member

#4Oct 7, 2010Joined: Feb 9, 2008Messages: 7,851 Likes Received: 1,336 Trophy Points: 280

Asante sana ndugu Mandago kwa haya maneno yenye hekima kubwa, nimejifunza mengi katika meneno haya ya hekima.


(You must log in or sign up to reply here.)

 Facebook


 Twitter


 LinkedIn


 Google+


 Pinterest


 Email


WHO ARE WE?


JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic. You are always welcome!

Read more...


WHERE ARE WE?


We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually. For anything related to this site please Contact us.

Contact Us Now...


DISCLAIMER


JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

Read more...


FORUM RULES


JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you. You MUST read them and comply accordingly

Read more...


PRIVACY POLICY


We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one. Read our Privacy Policy.

Proceed here...



Contact Us


Help