NgongosekeJF-Expert Member
#1Nov 15, 2014Joined: Jan 1, 2012Messages: 3,212 Likes Received: 18 Trophy Points: 135
Funguo nimezipenda
Jihadhari na machozi namna tatu:
1-Chozi la aliyedhulumiwa
2-Chozi la yatima
3-Chozi la baba na mama yako
Moja ya machozi haya yakitiririka, umejifungulia jahannam
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Usimuumize aliyekupita umri, na wala usimkatize.. siku moja utakuwa kama yeye
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Kufanya utani kwa maandishi kunaweza kufahamika vibaya kwa sababu ya kukosekana ishara ya uso na mikwaruzo ya sauti.. basi kuwa makini katika kuchagua maneno yako, kwani wengi wa watu ni wanatafsiri vyengine
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Utamu wa maisha ni kuishi kwa staili yako, na si staili ya wengine
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Ni kweli kwamba maji yanarudi kwenye mkondo wake, lakini yakirudi yanakuwa hayafai kuyanywa
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Usijaribu kufuatilia kila kitu, huenda ukafahamu sivyo na ukawapoteza wengi walio karibu yako kwa sababu ya fikra zako.. jambo la kufanya; kuwa na dhana njema kwa walio karibu nawe
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Watu wengi wanazungumzia kutenda na hawafanyi lolote.. na wengine hawasemi watakalofanya na wanafanya na kupata wanayotaka
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Hakuna tofauti kati ya rangi ya chumvi na ya sukari.. vyote viwili ni rangi moja.. lakini tofauti utaijuwa baada ya kujaribu! halikadhalika wanadamu
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Wengi wanaoongelea aibu za watu ni watu ambao hawaangalii aibu zao kubwa, miongoni mwa hizo ni vile wao kuhadithia aibu za watu
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Marafiki hawabadiliki bali sisi tunafanya haraka kuwaita baadhi ya watu marafiki
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Baadhi ya watu watakuacha, lakini hiyo si mwisho wa kisa cha maisha yako, bali ni mwisho wa nafasi yao kwenye kisa chako si zaidi
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Hutaweza kubadilisha umbo lako ili uwe mzuri zaidi kwenye macho ya watu, lakini unaweza kudhibiti tabia yako na kuipendezesha adabu yako ili uwe mzuri kwenye macho ya watu
🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐🔐Sisi ni jamii tukitaka haraka tunasema jambo jema ni bora lifanywe haraka.. na tukitaka kuchelewesha tunasema kuchelewa kuna kheri yake.. masuala ni mizaji, si zaidi
kibobori.1Senior Member
#2Nov 15, 2014Joined: Nov 7, 2014Messages: 168 Likes Received: 0 Trophy Points: 0
Kweli kabisa mkuu
promisemeJF-Expert Member
#3Nov 15, 2014Joined: Mar 15, 2010Messages: 2,715 Likes Received: 29 Trophy Points: 135
Mkuu hayoo machozi nna ya ogopa! Haswa ya yatima kwanza nawaonea huruma..
NgongosekeJF-Expert Member
#4Nov 15, 2014Joined: Jan 1, 2012Messages: 3,212 Likes Received: 18 Trophy Points: 135
promiseme said: ↑
Mkuu hayoo machozi nna ya ogopa! Haswa ya yatima kwanza nawaonea huruma..
Inabidi uogope yote na wazazi pia na ya dhulma usisahau
promisemeJF-Expert Member
#5Nov 15, 2014Joined: Mar 15, 2010Messages: 2,715 Likes Received: 29 Trophy Points: 135
Ngongoseke said: ↑
Inabidi uogope yote na wazazi pia na ya dhulma usisahau
La wa zazi alhamdulillah najitahidi sana na uzuri wazee Wangu wametulea malezi ya dini najua umuhimu wa wazazi, na bila kusahau dhulma, sababu yakusema yatima nalea watoto wa Mtoto wa shangazi yangu wako 3 sasa 1 Kati Yao nimkorofi kupitiliza ananisugua roho Mpaka nalia kwakusema....
NandoJF-Expert Member
#6Nov 15, 2014Joined: Oct 5, 2014Messages: 4,783 Likes Received: 1,453 Trophy Points: 280
Maneno yako yapo vzuri yamenigusa.
(You must log in or sign up to reply here.)
WHO ARE WE?
JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic. You are always welcome!
WHERE ARE WE?
We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually. For anything related to this site please Contact us.
DISCLAIMER
JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..
FORUM RULES
JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you. You MUST read them and comply accordingly
PRIVACY POLICY
We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one. Read our Privacy Policy.