Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 22 Aprili 2017

Mama kuwa makini House Girl Yaweza Kuwa Mke Mwenzio KAMGISHA BLOG / 3 hours ago

Mama kuwa makini House Girl Yaweza Kuwa Mke Mwenzio KAMGISHA BLOG / 3 hours ago

Ivi ni vibaya House girl kuolewa na baba mwenye nyumba?

Ndugu msomaji wa Muungwana Blog, karibu kwenye makala hii maalumu, nimeamua kuandika habari hii ili kujaribu kupunguza mifarakano kwenye familia zetu especially familia zenye wafanyakazi wa ndani wanaojulikana kama house girl.

Katika mada hii nimekuwa nikikutana na maswali mengi sana ambayo mda mwingine yalikuwa yakituchanganya hata sisi wenyewe katika kuwajibu wahusika, maswali haya malanyingi yalikuwa yakiulizwa na akina mama.

Na kwa upande wa akina baba maswali yao sio mengi ukilinganisha na akina mama, sasa napenda nianze kwa kusema mambo yafuatayo ili wote twende sawa.

WAJIBU WA MWANAUME KATIKA FAMILIA: 
Mwanaume anawajibu wa kutimiza mahitaji yote ya msingi katika familia yake, moja ya majukumu hayo ni pamoja na kutoa pesa za matunzo ya familia yake kadri ipasavyo, kuonyesha upendo wa dhati kwa mama pamoja na watoto wake, na mambo mengineyo nk.

WAJIBU WA MWANAMKE KATIKA FAMILIA: 
Mwanamke ndiye mtendaji mkuu wa familia kwa upande wa nyumbani ukiachilia mbali ya kwamba baba ndiye kichwa cha familia, mwanamke anamajukumu mengi kwa upande wa nyumbani moja ya majukumu yake ni pamoja na kupika chakula cha familia, kufua nguo za mumewe pamoja na nguo za watoto, kuakikisha nyumba pamoja na eneo linaloizunguka nyumba ni safi, kuonyesha upendo wa dhati kwa mumewe pamoja na watoto wake, nk.

Ndugu msomaji wa makala hii, nadhani mpaka hapo tayari umeisha anza kupata mwanga kuhusu jibu la swali la makala yetu, sasa twende kuona wajibu wa mfanya kazi wa ndani kama house girl.

House girl wajibu wake ni kuakikisha anafanya usafi wa kuizunguka eneo la  nyumba kwa nje na kufanya usafi huo kwa upande wa ndani kwa baadhi tu ya maeneo ya nyumba hiyo pamoja na kuwaogesha watoto, kufua nguo za watoto, na kufanya kazi ndogo ndogo za nyumbani.

House girl hatakiwi kufanya usafi chumbani kwa mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kufua au kupiga pasi nguo za mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kumuandalia chakula au chai mume wa mama mwenye nyumba, nk.

Sasa ukiona house girl anafanya kazi zote nilizosema kuwa hatakiwi kuzifanya pindi awapo nyumbani kwako, ukiwa kama mama mwenye akili timamu jua kabisa tayari umeamua kumuletea mumeo mke mdogo na pia usipige kelele wala kulaumu maana jitihada zote za kumuandaa mke mwenzio umezifanya wewe mwenyewe.

Ushauri wangu kwenu akina mama na akina dada nikwamba, hatukatai kuwa wafanyakazi wa ndani hawafai, ila jitaidi mfanyakazi wako awe na mipaka ya kazi, mwanaume anaamua kumuoa house girl kwa sababu yeye amechukua majukumu yote ya mama mwenye nyumba, sasa wewe mama usianze kumtupia maneno mtoto wa watu pamoja na mumeo maana yote hayo umeyataka wewe mwenyewe.

Jumatatu, 10 Aprili 2017

Jinsi ya kucheza paM-Bet Perfect12 - Ni jinsi TICKET PRICE: 1.000 Tzs

12:02:04

Language: Kiswahili

 Remember me

Forgotten Password?

Register

English

Toggle navigation

 Download Android APPMenyu

     

Ni jinsi

Tiketi

Your bet slip is empty. Please select odds from seventeen matches to start playing.

Dau: 1,000 Tsh

 Tigo Pesa
 Pochi
 M-Pesa
 Airtel Money

Idadi ya bashiri: 0

M-Bet Perfect12

Jinsi ya

M-Bet Perfect12 - Ni jinsi

TICKET PRICE: 1.000 Tzs

MECHANICS

Kuna orodha ya michezo 12 pamoja na 4 hifadhi michezo kutoka mashindano tofauti ( EPL , la liga , Ligi ya Mabingwa, Kombe la Euro . Kombe la Dunia nk nk, ).

Wateja wanaombwa kutabiri Matokeo ya michezo yote 12 , kuchagua 1x2 ( Nyumbani kushinda, sare , ugenini kushinda ), pamoja na Outcome ya 4 hifadhi michezo.

Orodha 4 za ziada itakuwa zikitumika kwa ajili ya mchakato wa sare wakati moja ya mchezo ya 12 orodha kuu ikifutwa (kutokana na hali ya hewa au sababu haitabiriki nyingine yoyote).

Kama mchezo mmoja utafutwa, mchezo wa kwanza wa ziada utawekwa badala ya mechi kufutwa. Kama kuna michezo 2 imefutwa, kisha michezo 2 ya kwanza ya ziada zitawekwa badala ya mechi kufutwa na huo utatumika kwakufutwa 3 au 4.

FREQUENCY

Kutakuwa na draw 7 wa Super 1x2 kwa wiki

Mdaa wakufungua super 1x2 itachapishwa Siku moja kabla, wakati mchezo wa kwanza ya orodha ikianza. Mchakato huo utakuwa siku ya pili. Kufunga super 1x2

ZAWADI

Wachezaji walio tabiri mechi zote 12 kwa usahihi watakuwa washindi wa SUPER 1x2 super prize.

Wateja walio tabiri mechi 11, 10 au 9 kwa usahihi pia watakuwa washindi na kupata zawadi nyingine kwa kuzingatia mauzo ya kila mchakato.

Katika Mchezo huo kama hakupatikana mshindi au mtu yeyote katika makundi mbalimbali hatuto kuwa na malipo, yatawekwa na atalipwa kwa mchakato yafuatayo.

Katika Mchezo huo kama kuna mshindi zaidi ya moja katika Kila aina ya mchezo, zawidi zita gawanywa kwa sawa miongoni mwa washindi wa mchezo huo.

Zawadi ya mshindi wa Mchezo wa chini hawezi kuwa kubwa kuliko washindi wa michezo ya juu. Katika kesi hiyo, Jumla ya zawadi ya makundi yote itaongezwa na kusambazwa kwa usawa miongoni mwa washindi wa makundi yote mawili.

Close

Closes on Monday 10 Apr 19:001La LigaREAL SOCIEDAD vs SPORTING GIJON1.45 4.40 6.50 
  2Premier LeagueCRYSTAL PALACE vs ARSENAL4.70 3.90 1.70 
  3PolandKORONA KIELCE vs RUCH CHORZOW2.05 3.30 3.40 
  4PortugalMARITIMO vs CHAVES1.95 3.20 4.02 
  5BulgariaVEREYA STARA ZAGORA vs SLAVIA SOFIA1.90 3.30 3.50 
  6DenmarkAARHUS vs SILKEBORG2.05 3.37 3.40 
  7Bundesliga 2EINTRACHT BRAUNSCHWEIG vs DYNAMO DRESDEN2.20 3.21 3.20 
  8TurkeyISTANBUL BASAKSEHIR vs GALATASARAY2.20 3.45 3.10 
  9SwedenIF ELFSBORG vs AIK2.40 3.30 2.80 
  10Ligue 2AJACCIO vs LENS3.20 3.00 2.30 
  11Serie BNOVARA vs VERONA2.46 3.05 2.90 
  12NorwayKRISTIANSUND BK vs BRANN3.05 3.16 2.30 
  Fixtures reserved for possible cancellationsR13Holland 2JONG PSV vs VOLENDAM2.30 3.40 2.80 
  R14TurkeyKASIMPASA vs KONYASPOR2.10 3.20 3.50 
  R15Holland 2JONG UTRECHT vs FC OSS2.05 3.50 2.99 
  R16RomaniaFC ASTRA GIURGIU vs DINAMO BUCURESTI2.10 3.15 3.52 
  R17PeruCOMERCIANTES UNIDOS vs SPORT HUANCAYO1.90 3.34 3.85 
  

English | Kiswahili

April, 10 2017 - 12:02:04

Kibali/Leseni

Usalama na majukumu/wajibu

Imewezeshwa na

Copyright © 2017 by M-Bet All rights reserved
This web is operated by M-Bet, a company incorporated under the laws of Tanzania, and licensed by the Gaming Board of Tanzania. Gambling can be addictive. Lengo la mchezo 
Namba ya simu ya huduma kwa wateja : 0762 768 500 VODACOM / 0758 833 333 VODACOM ● 0673 15 27 15 TIGO / 0673 15 28 15 TIGO ● 0689 755 999 AIRTEL / 0689 749 999 AIRTEL ● Barua pepe: msaada@m-bet.co.tz

Alhamisi, 6 Aprili 2017

Breaking News: Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande Afariki Dunia

Breaking News: Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande Afariki Dunia KAMGISHA BLOG / 5 hours ago


Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia.

Sir Andy amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge.

Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania).

SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS

Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi.

Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.

Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.

Siyo hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha mafanikio’.

Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.

Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo.

Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.

Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.

“Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.

Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.

Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra Press.

Anaandika: “Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.

Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.

“Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.

Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.

Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Kanuni za Freemason zinafundisha nini?

Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.

“Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika Chande katika kitabu hicho.

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.

Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu, umakini na haki.

Chande anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.

“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:

“Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu, vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason.

Sir Andy Chande akiwa na watu mashuhuri enzi za uhai wake..

 Akiwa na Diamond Platnumz

 Akiwa na JM Kikwete

 Akiwa na BW Mkapa

 Akiwa na A.H. Mwinyi

 Akiwa na JK Nyerere

Akiwa na Wanajumuiya wenzake wa Freemasonry

- Historia yake zaidi, tazama video hii;