Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 12 Aprili 2020

Je Yesu alikuwa Mwislamu?

DiraElimu

Ni mwangaza wa maisha yako

 Nyumbani ▼

Jumapili, 7 Februari 2016

Je Yesu alikuwa Mwislamu?

Yako madai ya baadhi ya wanaharakati wa kiislamu wanaodai kuwa Eti bwana Yesu alikuwa Muislamu kwa madai kuwa alikuwa akiingia katika Masinagogi (yaani misikiti ya wayahudi) Luka 4;16,Pia kwa sababu alikuwa anaomba akiwa anasujudia (Mathayo 26;38-44) Maandiko haya kwa waislamu ndio kigezo kikuu cha kuwa Yesu ni mwislamu.Madai haya ni ya ajabu sana kwani yanapingana na ile kweli iliyomo katika quran na Khadithi za Kiislamu Kulazimisha kuwa Yesu alikuwa muislamu kunaanza kutufanya tukubali kuwa Qurani ni kweli kuwa si kitabu kinachoongoza katika kweli kwani ni Qurani yenyewe ndiyo inayosema kuwa Muhamad aliamuriwa awe wa kwanza miongoni mwa waliosilimu soma (Surat al-anaam 6;14)……. “Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu……” ayah ii inathibitisha wazi kuwa Muislamu wa kwanza katika wanaume aliyesilimu alikuwa Muhamadi mwenyewe, aidha katika  kitabu cha cha historia ya Maisha ya nabii muhamad uk 18 kifungu cha pili cha shekh Abdulla Saleh Farsy kinasema ….Basi Mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke akimaanishwa bi khadija unaona sasa linakuwa jambo la kushangaza kuona wana mujahidini wakipingana na maulamaa wao au wanazuoni wenzao au hata quran aidha wanaharakati hawa wa kiislamu kumbe wanataka kutuambia kuwa wayahudi nao ni waislamu? Na kama hivyo ndivyo je quran inafundisha nini kuhusu wayahudi? Soma  Surat al maida-5;51 inasema hivi….. “Enyi mlioamini msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa rafiki zenu (wa kuwapa siri zenu) wao kwa wao ni marafiki.Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki nao basi huyo atakuwa pamoja nao na hakika allah hawaongozi watu madhalimu….” Qurani inaonyesha kuwa Hakuna uhusiano wa waislamu na wayahudi wala wakristo Yesu alikuwa Myahudi na hivyo kuingia katika msikiti wa wayahudi ilikuwa ni desturi yao. Je muhindu akiingia kwenye msikiti wa wahindu ni mwislamu kwa sababu hiyo?



 Musa na Harun pia hawakuwa waislamu wala hawakuanzisha Dini

      Tukumbuke kuwa Yesu alikuja kutafuta  na kuokoa kile kilichopotea hivyo ilikuwa ni lazima aingie kwenye majengo ya watu waliopotea ili apate kuwafundisha Luka 4;17-30, hata hivyo mara nyingi watu hao wa kenye masinagogi walijaa ghadhabu na walimtoa nje ya mji wakimpeleka katika ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa wapate kumtupa chini.Luka 19;45-47 Yesu aliingia katika Hekaluni akaanza kuwatoa nje wale waliokuwa wakifanya biashara akawaambia imeandikwa nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi naye akawa akifundisha kila siku hekaluni je alikuwa dini   gani? Aidha ikumbukwe pia kuwa Paulo mtume pia aliingia katika masinagogi hayo Matendo 17;1-2 na pia ilikuwa ni desturi yake je wanaharakati wa kiislamu wanataka kutuambia kuwa Paulo naye pia alikuwa mwislamu? Kwa kuwa tu aliingia katika sinagogi? Mbona huwa hawadai kuwa Paulo mtume ni mwislamu? Aidha ni Muhimu kukumbuka kuwa mafundisho ya bwana Yesu yalikuwa yakipingana vikali na watu wa Masinagogi Yesu alikemea tabia zao za kupiga panda watoapo sadaka yaani walikuwa wanafiki Mathayo 6;2.,aliwakemea kwa kupenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pande za njia ili waonekane na watu hii nayo ilikuwa tabia ya kinafiki (Mathayo 6;5-15) aidha Bwana Yesu alifundisha kusali kwa kupitia sala ya bwana Baba yetu uliye mbinguni……….  Jambo ambalo waislamu hawalifuati kabisa,Mwishoni watu wa masinagogi walimfukuza Yesu kabisa wakiwa wamejaa ghadhabu ikiwa Yesu alikuwa mwislamu mwenzao iweje walimfukuza? Quran inasema  Wanafiki wamejenga msikiti wa kuleta udhia na kutia nguvu ukafiri……… Hivyo aya hii inathibitisha kwamba misikiti ni ya watu wanafiki,Pia quran  inayataja Masinagogi kuwa ni nyumba tofauti na Misikiti ona Surat al-hajj 22;40 Ambao wametolewa majumba (mjini)mwao pasipo haki ila kwa sababu wanasema  mola wetu ni mwenyezi mungu na kama mwenyezi Mungu asingali wakinga watu baadhi yao kwa wengine bila shaka yangalivunjwa MAHEKALU (Swaamiu) na MAKANISA (Wabiya-unw) na nyumba nyingine za ibada MASINAGOGI (Wasalawatunw) na MISIKITI (Masaajidu) ambamo jina la mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi…….. jambo linalo shangaza ni kuwa Qurani inataja masinagogi tofauti na misikiti kulikoni basi kama sinagogi ni msikiti?

    Biblia haitufundishi kuwa Yesu alikuwa Mwislamu inatuambia Yesu ni mwana wa Mungu soma (Mathayo 3;16-17,Yohana 17;1,8;54,)aidha Tunafundishwa kuwa Bwana Yesu ndiye mwanzilishi wa kanisa katika Mathayo 16;18 anasema  “Nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda”Yesu aliyasema hayo kabla Muhamad hajazaliwa wala uislamu haujaanza aidha ufunuo wa Yohana sura ya pili yoote  Yesu anazungumza na kanisa na anatofautisha na sinagogi. Hivyo Kanisa limeanzishwa na Bwana. Maadui wakubwa wa waislamu ni mayahudi Surat al maida 5;82 na Yesu alikuwa myahudi leo Mujahidina wanasemaje Yesu alikuwa Mwislamu? Na Quran inasema maadui zao ni wayahudi na biblia inasema Yesu alikuwa Myahudi soma (Yohana 4;9).

kwa Februari 07, 2016


Maoni 5 :

Unknown4 Desemba 2016 09:45

Unaona una matongotongo

Jibu


Unknown4 Desemba 2016 09:46

Muhammad aliposema kuwa ni wa kwanza alikua nakusudia wa kwanza kwa umma wake na sio wa kwanza kwa umma zote usikurupuke.

Jibu


Unknown4 Desemba 2016 09:47

Muhammad aliposema kuwa ni wa kwanza alikua nakusudia wa kwanza kwa umma wake na sio wa kwanza kwa umma zote usikurupuke.

Jibu


Unknown4 Desemba 2016 09:50

Unaona una matongotongo

Jibu


Raphael Kimaro9 Julai 2019 07:35

we kafir muhammad ndio wa kwanza kusilim. hiyo haya kwamba ndionwa kwanza kwa uma mbona hujatoa.

acha ujinga. elimu hiyo fundisha msikitini maana ndiko utaposema uongo ili mjifurahishe.

ukija huku sema ukweli tunataka andiko kama sisi tulivyotoa. na kwanza hata muhammad mwenyeww hakusilim maana hakuna haya aliyokubali. 

ndio maana wa kwanza kusilim akawa bi adija. muislam wa kwanza duniani sasa wewe leta mdomo badala ya andiko. mti mzima kutumia hisia badala ya akili ni hatari

Jibu



Nyumbani

Ona toleo la wavuti

Kunihusu

Mkuu wa wajenzi mwenye HekimaTazama wasifu wangu kamili

Inaendeshwa na Blogger.

Alhamisi, 22 Agosti 2019

Kanuni za ndoa

#KANUNI_ZA_NDOA_KWA_WANAWAKE

👉Nakusihi Acha uvivu tenga dkika 3 Soma mpaka mwisho Utapata kituu

✍️#Usinyanyue sauti mbele ya mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima.

#Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako.

#Usitumie mhemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha.

#Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka.

#Usiwatendee vibaya marafiki wa mumeo kwa sababu huwapendi, mtu anayetakiwa kuwa wa kwanza kujitenga nao ni mumeo.

#Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako.

#Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mwenyewe.

#Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na kumshajiisha.

#Usiwe mke mwenye matumizi ya hovyo, jasho la mumeo halitakiwi kutumiwa hovyo.

#Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu.

#Usimlinganishe mumeo na mwanaume wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake.

#Usijibishane na mumeo hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. Hitajio namba moja la mwanaume ni heshima.

#Usimpe changamoto mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye busara hawafanyi hivyo.

#Usisahau kumuandaa mumeo na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani.

#Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo.

#Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na kwenye dressing table. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao wanatumia muda wao kujiremba vizuri bila haraka yoyote ili waonekane maridhawa.

#Wazazi au familia yako hawana uamuzi wa mwisho katika ndoa yenu. Endelea kuwaheshimu, lakini wasiwe na uamuzi wa mwisho kuhusu ndoa yenu.

#Usiegemeze upendo wako kwenye vitu vya pesa. Endelea kumheshimu mumeo licha ya kwamba unapata pesa zaidi yake.

#Usisahau kuwa mume anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha.

#Iwapo mawazo yako yamefanikisha jambo kuliko mawazo yake, usijilinganishe naye. Bali ishini na mfanye kazi kama timu.

#Usiwe msumbufu kwa mumeo. Hakuna mume anayependa mke msumbufu.

#Mke mvivu hajali. Hata hajui kwamba anatakiwa kuoga na kuwa msafi.

#Je, mumeo anapenda chakula fulani? Kuwa makini sana kwenye namna ya utayarishaji wa chakula. Hakuna mume anayefanya maskhara na suala la chakula.

#Usiwe mtu wa kumkamua sana mumeo, ukataka kila kitu uwe nacho wewe. Furahia kile kinachopatikana kulingana na uwezo wake.

#Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho wa kwanza kwa mumeo na kwa kila mgeni anayeingia nyumbani kwenu. Ukarimu maridhawa ndiyo uzuri wa kweli.

#Usisuhubiane na wanawake wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa.

#Ndoa yako itakuwa na thamani kama utaipa thamani. Uzembe na kutojali ni sumu ya ndoa.

#Watoto ni zawadi adhimu kutoka kwa Mungu, wapende na uwafunze mambo mazuri.

#Umri usiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa.

#Mke anayemuabudu Mungu ni mke maridadi, daima muombee mumeo na familia yako.

Ninakutakia ndoa njema. Usisahau ku share na wenzako kusambaza ujumbe huu muhimu kwako na kwa wengine wapenda maendeleo.

Jumapili, 21 Julai 2019

Mambo yatakayo mfanya mwanamke akupende zaidi

N/A · 6 hours ago

Hakuna kitu chenye thamani kubwa kwa msichana yeyote yule  kama kumfanya mtu huyo afurahi, hivyo kila wakati mwanaume unatakiwa kumfanya mpenzi wako afurahi ili uwezo kuongeze asilimia nyingi za upendo kutoka kwake kuja kwako. 

Yafautayo ndiyo mambo ya kufanya ili kufurahisha mwanamke katika mahusianao ya mapenzi; 

Mtanie  
Unapoongea na msichana, ni rahisi sana kumfanya na yeye aongee na wewe hatakama hakupenda mwanzo. Lakini hiyo haitoshi. Kama unataka kujua ni jinsi gani ya kuongea na msichana/mwanamke, utapaswa kumfanya yeye ajisikie huru na mwenye kujiamini(confortable), lakini pia mfanye ajue kuwa unampenda hatakama haujamwambia. 

Kumbuka, kama utaongea nae kama rafiki, lazima awaze na ajue kuwa wewe ni mwanaume noma sana(great guy), lakini hatahisi kwamba wewe ni mwanaume unaeweza kumchangamsha au kumfurahisha. Ili kuonekana kama mwanaume anayefurahisha kwa mwanamke yeyote, inatakiwa akuone kama mtu muhimu wa kukutana nae, na ili kufanya hivyo, msukume sukume hata bega katikati ya maongezi. Lakini usizidishe sana utaishia kumboa, fanya hivyo pale tu anapoongea jambo linalochekesha au lenye utani ndani yake. 

Ila usiende na kumwambia maneno ya kawaida kama “unamuonekano mzuri”, “wewe ni mzuri sana”, au maneno yenye kufanana na hayo. Inawakera sana na haioneshi utofauti na watu wengine wa mtaani. Badala yake, jaribu kuwa specific wakati unamuambia jambo fulani mnapokutana. Mwambie maneno kama “umependeza sana leo. Huo ni mtindo mpya wa nywele?”, Hayo ni maneno mazuri sana kwa mwanamke kwa sababu ni wanaume wachache sana huyatumia kwao. Kwa hiyo unavyosema “leo umekua mrembo zaidi” inamfanya ajue ni jinsi gani unamaanisha mpaka umevunja ukimya. 

Kwa kumtania huko  unaweza kufanya mambo matatu. Unaweza kumshtua na kumfanya atabasamu. Unaweza kumfanya ajue kwamba wewe unamuona mtu wa tofauti sana. Au tatu, unaweza kumfanya atambue kwamba umemwona wa kuvutia sana. Kumbuka hayo yote unamfanya yeye aone ni mtu mzuri ambaye anaweza kudate na wewe. 

Kuwa mcheshi 
Baada ya kumfanya atabasamu na kuyafurahia maongezi yako na yeye, ni muda wa kumuingia ndani zaidi kidogo. Kila mmoja wetu ana mambo yake ya siri ambayo hatupendi watu wote wajue labda mtu ambaye tunamwamini sana. Ili kumfanya ajiamini kwako, unatakiwa kumfanya awe na good time sana na wewe. Sasa hatuwezi kukuambia kabisa jinsi ya kumfanya mwanamke acheke. Lakini tunaweza kukupa mambo mawili ya kutumia. Usimwambie utani wowote wakati unaongea nae. Kuwa mwenye furaha muda wote unaoongea nae. 

Hii inaweza kukutatiza kidogo. Kwanza kuongea utani wa moja kwa moja kama mtu aliyekariri ni ujinga. Badala yake, ongea nae maongezi yatakayomfanya aone unamtania, na hapo naye ataanza utani. 

Jitahidi kuonesha unafurahia maongezi wakati unaongea nae kama unataka kumchangamsha. Ukiwa na furaha, dunia nzima inatabasamu pamoja nawe!. Kama unatabasamu na kujisikia furaha, naye atatabasamu pia na kuwa na furaha. Lakini kama unauoga, utamfanya naye awe  mwoga (unconfortable). 

Unaweza kumsukuma kidogo kati kati ya maongezi  
Najua unaelewa ninaposema kusukumana, hii utokea mara nyingi pale mvulana na msichana wanapukua wamezoeana, kwa hiyo kuifanya na mwanamke kwa mara ya kwanza inatakiwa uwe mwangalifu na makini ili usije kuharibu. Unapofanikiwa kufanya hivyo, jitahidi isiwe kila saa maana utamkera kama nilivyosema hapo awali. 

Ili uweze kufanya hivyo inatakiwa uwe wa kawaida, chukulia kama ni mtu wa kawaida japo wewe unajua ni special. Muulize alifanya nini weekend au baada ya kutoka kazini, muulize anapenda kwenda wapi akitoka out au ni mgahawa gani anaupenda au anatamani kwenda au kitu kingine chochote ambacho ni binafsi(very personal). 

Mshike.  
Huu ni uwanja hatari sana, lakini ni kitu unachopaswa kujifunza kwa sababu unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, si ndiyo? Hivyo kumshika katika muda muafaka inakamilisha point ya hii ya mambo ambayo unapaswa kuyajua wakati unataka kumfurahisha mwanamke. Kama utafanikiwa kulifanya hili kwa usahihi, utakua umejichukulia point kubwa sana. 

Sasa kumshika msichana ni kama kucheza na moto. Ukiushika fasta hauwezi kusikia joto, lakini ukiushika muda mrefu utaungua! Unaona ilivyo hatari?  Unaweza kumshika bega au mikono kama tayari ushamfurahisha vya kutosha. Lakini kumbuka hili, mshike tu pale unapokua na sababu ya kumshika, mfano mshike masikio kama unayasifia masikio yake au nywele kama unazisifia nywele zake, au mfute koti lake kama kuna kauchafu hatakama hana hako kauchafu, au mshike begani kama unatembea nae barabarani/ mtaani. 

Kumbuka kumshika mtu ni very personal, hivyo inabidi uwe makini sana na uangalie anamuitikio gani wakati unamshika kabla haujamshika tena. Kama unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, yatumie haya mambo matano wakati utakapokutana na mwanamke next time. Na baada ya hapo utaona ni jinsi gani unavyoweza kumfurahisha mwanamke na kumfanya ayapende maongezi yako kwa mara ya kwanza!.

Jumatatu, 15 Julai 2019

Orando-Malaika-Audio download

Download-orlando-Malaika Audio free


  

 
Size 3.96 Mb
N/A · 34 minutes ago


Watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mbalimbali ambayo yanahusiana na masuala ya kibiashara. Na miongoni mwa maswali ambayo wamekuwa wakiniuliza ni kuhusu ni nini faida ya kutangaza biashara kwa sehemu kubwa? 

Swali hili ndilo limenifanya nishike kalamu yangu ili niweze kulijibu. Nakusihi twende sambamba ili niweze kueleza kwa kinagaubaga, kwa nini unapaswa kuitangaza biashara yako tena kwa nguvu zote. 
Matangazo ni usambazaji wa taarifa  sahihi  kuhusu bidhaa au huduma kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. Matangazo ndiyo roho ya biashara, kwani bila kufanya biashara yako bila matangazo ni sawa na bure. 

Nafikiri pia utakubaliana nami ya kuwa ili uweze kufanya biashara  yenye tija ni lazima uitangaze biashara yako, kwani " biashara ni matangazo".  Matangazo ndiyo yatakuyokufanya uweze kuongeza mauzo ya kibiashara kila wakati. 

Kwa kuzingatia hilo unaweza kuitangaza biashara yako kwa njia ambayo itakuwa ni rahisi kwako. Na sababu kubwa ya kuitangaza biashara yako ni kuongeza wateja wapya. 

Leo na dhumuni kubwa la kutangaza biashara yako ni kukutana na na watu wapya,  ukiona umetangaza biashara yako na hakuna mteja mpya hata mmoja ujue fika kuna mahala ambapo umekosea. 

Hivyo fanya tathimni upya na ujipange upya na kuona ni jinsi gani unaweza kuitangaza biashara hiyo. Vile vile katika upangaji wa malengo ya kibiashara hakikisha ya kwamba unapanga na mbinu za kukutana na watu wapya kila siku. 

Nasisitiza juu ya kukutana na watu wapya, kwa sababu nimegundua ya biashara nyingi zimekuwa hazifanyi vizuri kwa sababu zimekuwa na watu ambao wanaizunguka biashara ile ni wale wale kila siku. Hivyo kila siku fanya tathimini juu wateja wapya ambao wamekuja katika biashara yako. 

Asante kwa kutembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio,  usisite kumshirikisha na mwingine ili aweze kujifunza.

Download

https://www.mediafire.com/download/astemzzag9g21b4

Orando montana x man piro x spero spera malaika

https://www.youtube.com/watch?v=238tsWknd_g&feature=share